HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KUMI NA SITA,(16)
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430
Sehemu ya kumi na sita (16).
"We Miriam nilikuambia huyu mwanaume atakuua" Anitha aliongea huku akiwa na kazi ngumu ya kumbembeleza Miriam ambae kwa wakati huo alikua akilia machozi kwa kurudishiwa bahasha hata bila kufunguliwa.
Josephat Kwa wakati huo alikua anashangaa jinsi Miriam anavolia,
"kweli kuna wasichana wanaolia uongo ila huyu hatanii ila kapenda kweli" Josephat alisema kwa sauti,
"jaman huyu Genes nimemkosea nini ananifanyia hiviiiii mungu siumfumbue macho jaman huyu wamoyo wangu?" Miriam aligaragara ardhini akilia kwa uchungu,
"haya best acha kulia basi watu wanatushangaa ujue" Anitha alizidi kumsihi Miriam atulie.
"kakaka we ne_ne_nda jumapili tuonane hapa" Miriam alimwambia Josephat na hapo Jesophat aliondoka kuelekea nyumbani kusubiria jumapili ifike.
Baada ya dakika ishirini tayari Miriam alikua nyumbani kwake ambako alienda baada ya kushindwa kuendelea na kazi.
"best unaendealeje?" Anitha jioni alipotoka kazini alimpitia Miriam nyumbani,
"best sina hamu yani heri nife" Miriam alimjibu huku akijizungusha kitandani,
"usiseme hivo mdogo angu mapenzi yanauma sana pale unapompenda mtu ambae hakupendi" Anitha alimjibu huku akimfunika mapaja yaliyokua wazi,
"alafu huyu mwanaume hakuoni ulivyo mzuri nini,cheki mtoto ulivyo laini" Anitha alijaribu kumtania Miriam ili afurahi kama kawaida walivyozoea kutaniana ila Miriam alizidi kuloanisha shuka kwa machozi,
"au hukuandika vizur nini?" Miriam alimuuliza Anitha huku akishikilia ile bahasha,
"hapana mdogo angu niliandika kila ulichokua unanambia" Miriam alijibu,
"sasa dada Anitha nifanyeje maana me nishapenda tayari na sitoweza kumuacha huyu mwanaume aende anaweza kukutana na mwanamke asie na mapenzi ya dhati kwake"Miriam aliongea kwa machungu makubwa.
Anitha alimpikia rafiki yake na kuhakikisha anakula,
" jaman mdogo angu kula tu hata hiki kijiko kimoja tu"Anitha alikua anambembeleza Miriam huku akimlisha kama mtoto.
Hakika lilikua pigio kubwa ambalo Miriam hakuamini kama angerudishiwa barua,
"kweli huyu mwanaume hanipendi ila sikati tamaa nitahakikisha atafaidi penzi langu LA dhati nishaapa kua na msimamo kwake" Miriam alijisemea siku ya ijumaa asubuhi akielekea kazini kwani alipanga jumapili atoke na Josephat ili waende kununua kitabu,
"nikimtumi kitabu atapokea naamini" Miriam aliendelea kujipa moyo.
*********
"We Angel mbona hatukuelewi" kijana aitwae Chris aliekua anasoma kidato kimoja na Genes alikua alifanya mazungumzo na Angel katika njia ya simu ila kila mmoja akiwa chooni, yaani Angel akiwa katika choo cha wanawake na huyo Chris akiwa choo cha wanaume na vyoo hivyo vilitenganishwa na madarasa yenye umbali wa mita hamsini,
"apaan sio kwamba hamnielewi bali jumapili hii namaliza kazi yake" Angel alijibu kwa sauti ya kujiiba uskute kuna mtu anamsikiliza,
"hakikisha unamaliza hiyo kazi basi la sivyo siri zote zitawekwa wazi" Chris aliongea na simu ikakatwa.
**********
"Genes weekend ndio hiyooo" lilikua neno la kwanza siku ya ijumaa pale Angel alivyoingia darasani kwa Genes,
"hata mimi naiona inakuja" Genes alijibu kwa sauti ya chini kwani tayari washakaa na kuegemea meza ambapo waliendelea kupanga mipango yao ya kukutana jumapili iliyokua mbele yao.
"we unapendekeza twende wapi tukapate tunda letu" Angel aliauliza,
"wewe chagua tu popote mimi nipo tayari" Genes alijibu huku akicheka kwa furaha,baada ya kurushiana mpira kwa mda,basi wote waliamua waende mitaa ya Sakina,jirani kabisa na Ngaramtoni ambako ndiko walipoona kunafaa kutokana na kuwa na hali ya utulivu hivyo waliamini hakutakua na magazeti.
*********
"Mdogo angu nakushauri tulia kwanza utapata mwanaume mwingine" Anitha aliendelea kumwimbia Miriam wimbo wa kila siku ambao haukumwingia akilini hata kidogo,
"dada Anitha kupenda ni haki ya kila mtu,mimi siwezi kumsubiri mwanaume anipende wakati kuna niliempenda tayari,mbona mwanaume anakutongoza kwani mimi sina moyo wa kupenda?" Miriam alijibu kwa hasira,
"kwa hiyo kesho ndo unaenda kumnunulia kitabu sio" Anitha aliuliza,
"ndio, kesho yule Jesophat atakuja niende nae kwenye duka la vitabu nikamtafutie kitabu chake kizuri akisome" Miriam alijibu kwa uso wa tabasamu.Anitha na Miriam waliagana.
Siku ya jumapili asubuhi Josephat aliwahi kuamka na kujiandaa tayari kuelekea kumchukua Miriam ili wakatafute kitabu dukani,
"kila siku nasema nataka niende Sakina alafu nakosa nauli, sasa leo nitamwambia huyu demu kua vitabu vizuri vinapatikana Sakina ili niende nae" Josephat alijisema moyoni.
"Sasa dada vitabu vizur kuna duka moja lipo huko Sakina maeneo ya Kwa Iddi pale ndo vinauzwa tena bei rahisi" Josephat alianza kumwambia Miriam alipomfuata Aquline hotel,
"mimi nakusikiliza wewe popote tutaenda" Miriam aliongea huku akijiamini kua yupo vizuri kifedha,
"sawa twende tukatize hapa stand ndogo tupige zoezi hadi Kilombero tupande hice"Josephat aliongea huku wakianza kutembea kwa miguu mwendo wa haraka haraka.
"Hebu nambie ukweli basi Jesophat, vipi huko shuleni Genes ana mademu au mbona ananifanyia mimi hivi" Miriam alimuuliza Jesophat swali wakiwa ndani ya hice,
"wala hana mademu" Jesophat alimtetea Genes ingawa alimjua Angel kua ni demu wake,
"sasa mbona hataki kua na mimi" Miriam aliongea huku machozi yakianza kumshuka kwa mbali,
"atakupenda tu usiogope" Jesophat alimjibu huku akimpa moyo,aliamini kufanya hivo kutamtuliza machozi aliyoona yanaanza kumshuka,
"we mamdogo hapo hebu nigaie hizo silva fasta,mbona unalia au shemela anazingua nini, ?njoo kwangu nitakupa gari hili" kondakta aliongea huku akimnyooshea Miriam mkono kuashiria kutaka nauli,
"hiyo hapo kata wawili tuache Kwa Iddi" Miriam aliongea huku akimkabidhi kondakta noti ya elfu kumi.
"chenchi hiyo mama" kondakta alimshtua Miriam aliejilaza kwenye kiti ila hakushtuka alikua kama kajisahau vile na hapo Jesophat aliipokea chenchi.
"oyo suka dondosha Kwa Iddi" kondakta alitoa sauti kwa dereva kuashiria kuna watu wanashuka.
"sasa duka lenyewe lile pale" Jesophat aliongea huku akinyoosha duka moja la vitabu lililokua pembeni ya barabara, walielekea hapo ila hawakumkuta muuzaji kwa mda huo,
"kaeni hapo kidogo anakuja saivi" walipewa viti vya kukaa na dada mmoja waliyemkuta hapo,walikubali kukaa kumsubiri kwani hawakua na haraka.
********
"sasa bby unajua hiyo lodge iko sehemu gani kabisa?" Angel alimuuliza Genes tayari wakiwa kwenye hice ya kuelekea Sakina,
"nakumbuka ukifika Sakina kituo wanaita Kwa Iddi kuna njia ipo upande wa kulia mwa barabara ndio tunaenda nayo kama mita mia mbili tunakuta kibao kimeandikwa KIMYA KIMYA LODGE,hapo tutafuata huo mshale" Genes alijibu,
"sawa mpenzi leo utanifaidi hadi ufurahi" Angel alimnong'oneza ili abiria wapembeni asisikie,
"we acha tu usiseme saivi zipu isije katika bhana ngoja tufike tu" Genes nae alimnong'oneza.
"Kwa Iddi njooni mlangoni" kondakta alitamka na hapo Angel na Genes walisogea mlangoni.
Itaendelea,
0 comments:
Post a Comment