MIMBA YA JINI -49

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini -49-

#SOON NAACHIA NEW STORY SHARE #LIKE PAGE UWE WA KWANZA KUIPATA #NEW_STORY

"Mustafa usishtuke huyu ndiye Sara."
"Ha! Usishangae, sijawahi kuona kiumbe mwenye kiburi kama huyu mwanamke.
SASA ENDELEA...

Sara yote aliyasikia lakini aliogopa kusema kuomba msamaha kwa kuogopa kubweka na kuwatisha. Machozi yalimtoka na kupiga magoti kuomba msamaha kwani mateso aliyopata asingeyasahau mpaka anakufa. Mustafa machozi ya uchungu yalimtoka kumuonea huruma Sara anavyotaabika.
Shehna alimshika Sara kichwani, ghafla alirudi katika umbile la kibinadamu. Hakusubiri maelezo, Sara alijitupa chini ya miguu ya Shehna kuomba msamaha.
"Shehna shoga yangu najua jinsi gani nilivyokukosea, nipo chini ya miguu yako haki ya Mungu, sitarudia tena kukufuatilia wala kufuatilia mambo yasiyonihusu. Nimeamini sisi wanadamu ndiyo wabaya, pamoja na mabaya yote niliyokutendea, hukuniacha nilale na njaa wala nile jalalani.
Nakuahidi kama utanibakiza na umbile langu la kibinadamu, nitakuwa kiumbe kipya, sitajiingiza tena katika mambo yasiyonihusu."
"Nina imani sasa unanijua, mimi ni nani?" Shehna alimuuliza huku akimtazama kwa jicho kali.
"Shehna."
"Nilipokuja kwako ulinionaje?"
Sara alishindwa kujibu alibakia kimya, Shehna alimuuliza tena.
"Ulikwenda kwa waganga ili kuchunguza kama mimi ni nani?"
"Ji.." hakumalizia, aliogopa kusema.
"Malizia tu, kwani nilipokuja kwako nilikuambia mimi ni nani?"
"Jini."
"Baada ya kunijua?"
"Shehna, nimekukosea naomba unisamehe sitarudia tena, najutia nafsi yangu," Sara alilia kilio cha majuto.
"Mustafa elewaneni na Sara ili likitokea, mimi simo tena," Shehna alijitoa kwenye kiburi cha Sara.
"Sara, ukitoka hapa, ya hapa yaache hapahapa ukiropoka litakalokukuta utalia na nafsi yako."
"Kaka Mustafa sirudii tena, nimejifunza kiburi si maungwana."
"Nina imani mmeelewana leo sitazungumza chochote siku ukinitibua, nitakufanya kiumbe cha ajabu, siwezi kukuua tu ila cha moto utakiona."
"Shehna nakuapia sitathubutu kusema chochote wala kufanya lolote."
"Kesho utaamka asubuhi nyumbani kwako, majirani wakikuona lazima utakutana na maswali mengi, usiwajibu kitu, oga wahi kazini."
"Nimekuelewa shoga yangu."
Shehna alimshika Sara kichwa na kujikuta akipitiwa usingizi mzito, aliwaita wasaizidi wake wamrudishe nyumbani kwake ili asubuhi aamkie kitandani kwake.
Baada ya Sara kuondoka, Shehna alimgeukia Mustafa aliyekuwa ametulia akimtazama na kumwambia:
"Mustafa, kuanzia leo sitaonekana mchana wala kufika kazini kwako."
"Kwa nini?"
"Sina tena uhuru wa awali, najiuliza atakaponiona mchana utanionaje au Sara akiniona ofisini atanionaje?"
"Nina imani kila kitu kimeisha, nimesha kuelewa, siwezi kukushangaa."
"Kwako, lakini kwangu itachukuwa muda kujionesha wazi kwako."
"Sasa nikiwa na shida na wewe?"
"Utaniona mara moja lakini si kama mwanzo."
"Mmh! Sawa," Mustafa alikubali kwa shingo upande.
"Mustafa naomba ukubaliane na mimi ili twende sawa."
"Nimekubali mpenzi."

***
Siku iliyofuata Sara alishtuka asubuhi na kujikuta kitandani kwake, aliamka na kwenda kuoga. Alipotoka nje, majirani zake walimshangaa na kumuuliza alikuwa wapi. Aliwajibu alikuwa safari ila wangezungumza vizuri jioni akirudi kazini. Alikwenda kazini kama kawaida.
Akiwa kazini alijawa na mawazo mengi juu ya maswali ya majirani zake, alijiuliza akirudi atawaeleza alikuwa wapi baada ya kuondoka ghafla. Mawazo yalipokuwa mengi, aliamua kwenda kwa bosi wake kuomba ushauri, baada ya kumsikiliza alimwambia:
"We wanyamazie tu."
"Wasumbufu sana watataka kunichimba, nitashindwa kuwajibu."
"Ulikuwa na wazo gani?"
"Kuhama pale."
"Hakuna tatizo."
Mara simu iliita Mustafa alipoangalia alikuta ni Shehna, alisema kwa sauti.
"Shehna."
"Anasemaje shoga yangu," Sara alisema kwa tabasamu.
Alipokea simu:
"Haloo mpenzi."
"Nipe Sara." Mustafa alimpa simu Sara.
"Haloo shoga," Sara alisema baada ya kuchukua simu.
"Ni hivi, ukitoka hapo usirudi nyumbani, umeshahamishwa."
"Nimehamishiwa wapi?"
"Masaki, nyumba inatazamana na duka la jumla, nina imani hayo yatakuwa maisha yako mapya."
"Asante shoga, ufunguo?"
"Mustafa atakupeleka sehemu yako mpya."
"Asante shoga."
"Haya kwaheri."
Sara alimpa Mustafa simu, baada ya kupokea alipewa maelekezo na Shehna, baada ya kukata simu alimgeukia Sara na kumueleza.
"Ukimaliza kazi nitakupeleka."
"Duh! Siamini nikitoka kazini nakwenda Masaki, siamini nami nimekuwa mtu wa matawi ya juu!" Sara alisema akishika kifua.
"Hongera, ulitaka kumtibua bure kumbe mambo mazuri yalikuwa yakija."
"Mbona nimekoma."
"Nina imani tatizo lako limekwisha, kaendelee na kazi."
"Sawa bosi," Sara alirudi kuendelea na kazi.
Muda wa kutoka Mustafa alimpeleka Msaki kwenye nyumba aliyoelekezwa na Shehna. Ilikuwa nyumba nzuri iliyokuwa na kila kitu ndani, hakukuwa na kitu chochote kutoka chumbani kwake zaidi ya vitu vyake vyote muhimu. Sara aliendelea kumshukuru Shehna na kuona kumbe jini ni umbile lakini wapo wenye roho nzuri kushinda hata wanadamu.
***
Mwezi moja kabla ya kujifungua, Shehna alimweleza Mustafa kuwa muda ule anatakiwa kuwa sehemu maalum ambayo hatakiwi mtu yeyote kuingiza zaidi ya mzazi wake na mkunga tu.
Pia alimweleza kuonana naye itakuwa baada ya miaka mitatu. Mustafa alikubaliana naye, hakuwa na kipingamizi.

Itaendelea

SOON NAACHIA #NEW_STORY KAAA MKAO WA KUPATA BONGE LA STORY ILI USIPITWE #LIKE_PAGE UWE WA KWANZA KUPATA BONGE LA STORY NATUMAI UTAIPENDAAAA

0 comments:

Post a Comment