MIMBA YA JINI -48

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini -48-

#SOON #NEW_STORY #LIKE_PAGE USIPITWE NA KIGONGO KINACHOFUATAAA

ILIPOISHIA:
“Shehna.”
“A...abeee,” aliitikia kwa sauti ya kilio.
“Nisamehe mpenzi wangu.”
“Huna kosa, nisamehe mimi.”
“Kwa kosa gani mpenzi?”
“NimekutDia kwenye mateso bila kosa.”
“Shehna huna kosa bali mimi ndiye niliyeshindwa kukusikiliza.”
“Hapana Mustafa mwenye makosa ni mimi kushindwa kukueleza ukweli mapema.”
SASA ENDELEA...
“Shehna nimekuelewa, najua una wasiwasi lakini ulitakiwa kunieleza mapema, nilikuwa na wasiwasi wewe labda nani lakini akili yangu ilikataa.”
“Kwa hiyo umenielewa mimi ni nani?”
“Ndiyo.”
“Hutaniacha?”
“Nilikueleza mapema sitakuacha maishani mwangu wewe ni kiumbe muhimu sana. Najuta kutaka kukupoteza wewe, mimi mwenyewe na watoto wetu watarajiwa.”
“Mustafa ukitoka hapa hutaitoa siri hii kwa watu?”
“Sitatoa, nimejua makosa yangu sitarudia, Shehna wewe ni kiumbe mwenye huruma sana na mapenzi mazito.”
“Kesho utarudi katika hali yako, ukiamka rudi kazini kama kawaida, usihoji kitu chochote ukifika endelea na kazi zako.”
“Sawa nimekuelewa.”
“Mustafa nitafanya kila kitu ili maisha yako yawe juu baada ya kujifungua nitakubadilishia kazi nataka uwe mmoja wa matajiri duniani.”
“Asante mpenzi wangu,” Mustafa alimkumbatia Shehna kwa furaha.
“Naomba usiniogope kwa vile ushanijua.”
“Siwezi, nakupenda Shehna.”
“Baada ya kunipa zawadi ya mtoto baada ya mimi kujifungua mkeo naye atapata mtoto. Nisingempa dawa ya ujauzito mkeo kwa sasa kwa vile nisingeweza kujifungua mpaka ajifungue yeye hivyo ningeteseka kwa uchungu kwa muda mrefu.”
“Nimekuelewa mpenzi.”
Baada ya mazungumzo ya kimabaha walilala kwa Shehna kuzima taa na kuondoa nguo zote kumuachia Mustafa kulichezea tumbo lililokuwa zimezidi kuwa kubwa. Ilikuwa ni siku ya furaha kwake. Alipanga siku nyingine amuombee Sara msamaha ili atolewe kwenye umbile la kimbwa.
***
Siku ya pili Mustafa aliposhtuka asubuhi alijaribu kumwita mkewe sauti ilitoka.
“Mke wangu.”
“Ha! Jamani Mungu mkubwa umepona mume wangu?” Husna alikurupuka usingizini baada ya kusikia sauti ya mumewe.
“Ndiyo.”
“Jamani Mungu mkubwa, siamini kama mume wangu leo ukizungumza sauti inatoka!”
“Niandalie maji nioge ili niwahi kazini.”
“Unataka kwenda kazini?”
“Ndiyo.”
“Kwani unajua ulikuwa kwenye hali gani?”
“Najua, si sauti ilikuwa haitoki sasa naweza kuwasiliana na wateja kama kawaida.”
“Si ungeiangalia hali yako kwa wiki ndipo uende kazini?”
“Ni kweli, lakini naamini nimepona.”
“Mmh! Haya.”
Mkewe Husna alinyanyuka kitandani na kwenda kumwandalia maji mumewe, baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa aliondoka kwenda ofisini. Mlinzi alipomuona alishtuka.
“Ha! Bosi.”
“Vipi John.”
“Umepona?”
“Ndiyo, nipo ofisini,” Mustafa hakutaka mazungumzo mengi aliingia moja kwa moja ofisini na aliikuta ipo katika hali ya usafi aliouzoea japo hakuwepo kwa muda mrefu. Hakukuwa na mabadiliko yoyote naye hakuhoji kitu kama alivyoelekezwa na mpenzi wake Shehna. Alifanya kazi kama kawaida mpaka jioni na kurudi nyumbani.
Husna alizidi kumshangaa mumewe na kutaka kujua tatizo lile lilitokana na nini. Baada ya chakula cha usiku wakiwa kitandani alitumia nafasi ile kumuuliza mumewe kilichomsibu.
“Mume wangu pole kwa matatizo, maana asubuhi sikuweza kuzungumza na wewe baada ya kutoka kuwa na haraka ya kuwahi kazini.”
“Asante.”
“Hivi nini kilichokusibu kupoteza uwezo wa kuzungumza mpaka mganga akasema hutakiwi kutumia dawa yoyote?”
“Mke wangu tuacheni na hayo.”
“Hapana mume wangu, ni mimi ndiye nilikuwa nateseka kuishi na wewe muda wote ukiwa bubu. Lazima kuna kitu kilichosababisha hali ile, hata mlinzi alishtuka kuona ukibadilika ghafla wakati mlikuwa mkizungumza.”
“Naomba uachane na hayo mke wangu kwa vile nimepona.”
“Kwa nini?”
“Kuwa mwelewa au unataka nirudi katika hali niliyokuwa nayo?”
“Hapana.”
“Basi tuachane na hayo.”
“Nimekuelewa mume wangu.”
Mustafa aligeukia upande wa pili na kuvuta shuka, mkewe naye alijisogeza karibu na mumewe na kumkumbatia kuitafuta siku ya pili.
***
Kama kawaida Mustafa alishtuka na kujikuta akiwa pembeni ya mpenzi wake, uso wa Shehna ulikuwa na tabasamu pana na kuzidi kuongeza uzuri wake. Alimuangalia sana Mustafa kama anataka kusema kitu na kufanya aulize.
“Vipi mpenzi?”
“Najua kuna kitu kinakuumiza akili siku nzima.”
“Kitu gani?”
“Kuhusu Sara.”
“Ni kweli, nilipanga kumuombea msamaha, nina imani wote tumekukosea.”
“Mustafa wewe hujanikosea lakini Sara kanikosea sana kafikia hatua ya kutaka kuniua!” Shehna alisema kwa sauti ya kilio.
“Adhabu aliyopata nina imani hawezi kurudia tena.”
“Mustafa nitamleta mbele yako aseme siku akirudia sitampa adhabu bali kumuua, nimefanya hivyo kwa ajili ya mapenzi yangu kwako.”
“Nakuahidi kuusemea moyo wake hatarudia tena.”
“Sawa.”
Shehna alinyanyuka na kutoka nje na kupiga makofi, vijakazi na watwana walifika haraka mbele yake kumsikiliza.
“Naam binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu unasemaje?”
“Kamleteni Sara mbele yangu.”
“Sawa binti mfalme.”
Alitoweka ghafla na kumuacha Shehna akirudi ndani, kabla hajaweka makalio chini Sara alikuwa mbele yake katika umbile la kimbwa. Mustafa alishtuka kumuona mbwa mbele yao.
“Mustafa usishtuke huyu ndiye Sara.”
“Ha! Usishangae, sijawahi kuona kiumbe mwenye kiburi kama huyu mwanamke.”
Sara yote aliyasikia lakini aliogopa kusema kuomba msamaha kwa kuogopa kubweka na kuwatisha.
Itaendelea

SOON NAACHIA NEW STORY TUKIELEKEA UKINGONI MWA HII STORY ILI USIPITWE NA STORY INAYOFUATA #LIKE_PAGE UWE WA KWANZA KUIPATA NEW STORY MTU WANGU WA NGUVU ASANTE KWA KUWA NAMI

0 comments:

Post a Comment