MIMBA YA JONI -47

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini -47-

#SOON NAACHIA #NEW_STORY LIKE PAGE USIPITWE NA VIPANDE VINAVYOENDELEA #LIKE_PAGE UWE WA KWANZA KUIPATA #NEW_STORY

ILIPOISHIA:
"Baada ya kufanya kosa la kwanza bado umeendelea kufanya kosa lingine la kutaka kutoa siri ambayo ni yako peke yako hatakiwi mtu kujua. Ni kweli mpenzi wako ni jini hilo ulitakiwa kulijua mapema na si kwa kuitoa siri nje."
"Jini?" Mustafa alishtuka."Unashtuka nini wakati matukio yote yalikuwa si ya kawaida, kwa vile bado ilibakia siri, mpenzi wako kila alipozima taa aligeuka kuwa jini kamili na tumbo lile kubwa ni mimba yake."
"Sasa nitafanyaje?"
SASA ENDELEA...

"Kitendo cha Shehna kuja mbele yako wakati unataka kutoa siri nje, amesababisha maumivu makali ya tumbo kwa vile alikurupuka sasa hivi yupo hoi. Msaada wako ni kuendelea kuwa hivyohivyo ili ibakie siri mpaka ajifungue, kama atakufa lazima na wewe utakufa kwa vile tayari kivuli chako kimo ndani ya damu yako ambayo ni wale wanao walio tumboni katika ujauzito ule.
"Hukutakiwa kuona tumbo akiwa katika umbile la kijini, ungeweza kufa muda uleule, lakini mapenzi ya jini yule ni makubwa sana kwako. Kwa vile bado hukutaka kuelewa ukataka kutoa siri ile hapo ndipo ulipopewa adhabu ambayo haitaisha mpaka ajifungue."
"Lini?"
"
Baada ya miezi saba atakapojifungua."
"Mmh! Miezi saba niwe hivihivi?" Mustafa alishuka.
"Hiyo ndiyo faida ya kiburi chako na adhabu hiyo ni ndogo kuliko zote ambazo amezitoa mama yake baada ya Shehna kuingilia kati kitendo chako kile kimemuumiza sana mama yake. Bila hivyo ulitaka kugeuzwa hamnazo."
"Mungu wangu, sasa utanisaidia vipi?"
"Sina msaada wowote zaidi ya kuitumikia adhabu yako, zaidi ya hapo ukitaka chokochoko utapotea wewe na waliokuzunguka."
"Siwezi kuonana na Shehna nimuombe msamaha?"
"Yupo katika uangalizi mkali baada ya kutoka ujinini bila idhini ya wazazi wake ili kukuzuia usiitoe siri yake na kumsababishia matatizo makubwa sasa hivi hana kauli, hajiwezi kwa lolote."
"Kwa hiyo utakuwaje?" Mustafa alishtuka.
"Adhabu yako ni kuitunza siri hii kwa miezi saba, cha kuomba Shehna apone upesi ili uweze kukupunguzia adhabu au kukuondolea ububu."
"Kwa hiyo baada ya mazungumzo narudia katika hali ya ububu?"
"Ndiyo usalama wako."
"Itanibidi nikubali sina jinsi," Mustafa alikubali kwa shingo upande.
Baada ya makubaliano aliitwa Husna mke wa Mustafa na mtu aliyemsindikiza ambao waliamini watakuta mabadiliko ya kukuta akizungumza. Lakini ilikuwa tofauti na mawazo yao, Mustafa alikuwa bado yupo katika hali ya ububu.
"Umefika wapi?" Husna aliuliza.
"Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu imeonesha ugonjwa huu utatoka taratibu bila kutumia dawa yoyote."
"Itachukua muda gani?"
"Sijajua, ila msirogwe kwenda kwa mganga yeyote eti amponye, dawa atakayompa ndiyo itakayomfanya awe bubu milele."
"Kwa hiyo hata panadol tusimpe akiumwa?" Husna aliuliza.
"Dawa zote mpeni, ila si za kutibu ugonjwa huu, msikubali kumpeleka kwenye maombi ya aina yoyote au kwa mganga yeyote. Ukifanya hivyo mtanikumbuka."
"Sawa tunashukuru."
Baada ya kukubaliana na mganga walimchukua mgonjwa wao ambaye ilikuwa vigumu kuamini anaumwa kwani alikuwa kwenye hali ya kawaida na kurudi naye nyumbani.

***
Siku zilizidi kukatika huku Mustafa akiwa katika hali ya ububu na Sara akiwa katika umbile la mbwa. Mateso makubwa yalikuwa kwa Sara ambaye aliendelea kuishi maisha ya kujificha kukimbia watoto kumpiga mawe na kulala kwenye majumba mabovu.
Chini ya bahari, Shehna alipata nafuu haraka sana na kuweza kukaa hata kula mwenyewe baada ya kupoteza fahamu kwa miezi mitatu iliyotishia uhai wake. Kukubali kwa Mustafa kuendelea kuwa katika hali ya ububu na kuyakubali maelekezo ya mganga, ile ilimsaidia sana kuwahi kupata nafuu.
Kama mkewe Mustafa angekuwa mbishi lazima angewapoteza mumewe na Shehna pamoja na watoto waliokuwa tumboni. Baada ya kupata nafuu alitaka kujua Mustafa yupo katika hali gani kwani aliamini hasira za mama yake lazima angemfanya kitu kibaya.
Katika vitu vyote alimkataza mama yake kumuua hata kumpa adhabu kali mpenzi wake.
"Mama mpenzi wangu yupo katika hali gani?"
"Nilimgeuza bubu ili asitoe siri mpaka muongee wenyewe na kukubaliana."
"Nimepona, vipi hali yake kwa sasa?"
"Bado sijamtoa ububu lakini niliyaangalia maisha yake ya siku zote, ila amenifurahisha kutotafuta dawa kwa ajili ya kutibu ububu. Kitendo kile kimesaidia wewe kupata nafuu upesi."
"Mustafa ni msikivu sijui kwa nini siku ile hakutaka kunielewa mpaka akawasha taa."
"Wewe ndiye mwenye makosa, ulitakiwa kujitambulisha mapema kwa vile alikuwa akikupenda sana, angekuelewa."
"Mama nilihofia kumueleza mimi jini, angenikimbia."
"Ona sasa alikuwa anatoa siri nje kwa vile alikuwa hakuelewi, kila kitu kingekuwa wazi, ububu na uelewa wake ndiyo nafuu yako, bila hivyo ungekufa, hali ilikuwa mbaya."
‘Sasa nifanye nini?"
"Aletwe leo aambiwe ukweli lazima atakuelewa tu."
"Sawa mama."
Malkia Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu mama wa Shehna walikubaliana na mwanaye usiku wa siku ile Mustafa apelekwe chini ya bahari.
***
Mustafa alishituka usingizini na kujikuta akiwa pembeni ya Shehna ambaye tumbo lake lilikuwa limeongezeka katika umbile la kibinadamu lililokuwa ndani vazi la kulalia. Shehna alikuwa akimtazama huku macho yakiwa yamejaa machozi na kuongeza uzuri wake.
"Shehna."
"A..abeee," aliitikia kwa sauti ya kilio.
"Nisamehe mpenzi wangu."
"Huna kosa, nisamehe mimi."
"Kwa kosa gani mpenzi?"
"Nimekutia kwenye mateso bila kosa."
"Shehna huna kosa bali mimi ndiye niliyeshindwa kukusikiliza."
"Hapana Mustafa mwenye makosa ni mimi kushindwa kukueleza ukweli mapema."

Itaendelea

SOON NASHUSHA #NEW_STORY ILI UWE WA KWANZA KUIPATA STORY HYO #LIKE_PAGE ENDELEA KUONYESHA UPENDO #SHARE # COMMENT #LIKE NIPOST MWENDELEZO WAKE

0 comments:

Post a Comment