MIMBA YA JINI -44

Author

Hadithi ya kusisimua  #Mimba_ya_Jini-44-

#SOON NAACHIA STORY NYINGNE USICHEZE MBALI NA PAGE HIII ILI UWE WA KWANZA KUISOMA #NEW_STORY  LIKE PAGE HIII NA SHARE KIPANDE HIKI NIPOST MWENDELEZO

ILIPOISHIA:
Mustafa kila alipokuwa kazini alikuwa na maswali mengi juu ya tumbo la Shehna kuwa kubwa kama puto lililojazwa hewa lakini lilikuwa laini na kupenda kulishika muda wote hata kumfanya kila siku alale kwa muda mchache.
SASA ENDELEA...

Kilichomuumiza akili kilikuwa ukubwa wa tumbo kila wakizima taa lakini akiwa na nguo zake za kulalila ilikuwa mimba ya kawaida.
Alijiuliza kwa nini wakizima taa linakuwa kubwa na kingine kwa nini hataki kumruhusu kulichezea tumbo lile kwenye mwanga! Alipanga siku ile usiku amtegee Shehna amelala awashe taa ili kutaka kujua kwa nini usiku tumbo lake linakuwa kubwa sana. Aliendelea na kazi kama kawaida huku taarifa za Sara zikizidi kumchanganya kutokana na kuelezwa hajulikani halipo wala hakuaga.
Mazingira ya kutoweka yalikuwa yakilingana na ya mara ya kwanza kitu kilichomfanya ajiulize Sara ana matatizo gani yanayosababisha kutoweka bila taarifa. Alikumbuka maelezo aliyopewa na Sara siku aliyorudi kazini baada ya kupotea kimiujiza alitoka kwenda kununua chakula cha usiku na kujikuta akiwa katika pori la kutisha na baada ya kutembea bila kujua na kutokea Dodoma.
Kingine kilichomshtua kuambiwa kuna mbwa alikutwa chumbani kwa Sara baada ya kumfukuza alirudi tena usiku na kusimama kwenye mlango uleule. Alijiuliza kipi hasa kimempata Sara na ana siri gani ambayo yeye na majirani zake hawaijui. Alipanga akienda kwa Shehna kumueleza tatizo lile labda angeweza kumsaidia.
Usiku ulipoingia kama kawaida aliposhtuka usingizini alijikuta yupo pembeni ya mpenzi wake Shehna. Kama kawaida tumbo lilikuwa la kawaida lililokuwa katika nguo nyepesi ya kulalia. Baada ya kuliwazana wote walipitiwa usingizi, Mustafa hakulala sana alishtuka mapema na kutulia kitandani alilichezea tumbo la Shehna ambalo lilikuwa haliishi hamu kwa vile lilimpa raha ya ajabu kila alipolipapasa.
Alitulia kwa muda kusubiri Shehna usingizi umkolee, baada ya muda alimsikia akikoroma. Alijua usingizi umemkolea. Aliteremka kitandani taratibu na kuelekea kwenye kandili ya dhahabu, aliiwasha huku akitetemeka aliipandisha mwanga ili aone vizuri.
Baada ya kuwasha taa na kumulika kitandani, alishtuka kuona kiumbe cha ajabu juu ya kitanda. Sura ilikuwa ya mpenzi wake Shehna lakini tumbo lake lilikuwa la ajabu lililokuwa kubwa na pembeni lilikuwa na rangi kama magamba ya nyoka na chini alikuwa na mkia mnene unaoungana na tumbo.
Mustafa alishtuka sana na kuanza kutetemeka, kingine kilichomshtua kuona kitanda walichokuwa wamelalia kilikuwa juu ya maji katika ya bahari. Mshtuko uliompata ulimfannya aanguke chini na kupoteza fahamu.
Baridi kali lilimuamsha Shehna usingizini, alipofumbua macho alishtuka kukuta amelala juu ya bahari. Haraka alijirudisha katika umbile la kawaida, palepale usiku mwili wake ulirudi kama kawaida na kuwa chumbani kwake lakini kandili ilikuwa ikiwaka. Alijiuliza nani aliyeiwasha taa ile, alishangaa kujikuta peke yake na kujiuliza Mustafa alikuwa wapi!
Alipoteremka kitandani alishtuka kumkanyaga mtu, alipoangalia alimuona Mustafa akiwa amelala chini amepoteza fahamu. Alijua tayari siri yake ilikuwa hadharani, alijiuliza atamwambia nini Mustafa amuelewe kuwa yeye ni jini pia alijiuliza akimueleza ukweli atakuwa tayari kuendelea kuwa naye!
Shehna alianza kulia kitu kilichomshtua mama yake baada ya kudondokewa na machozi. Malkia Bi Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu alikwenda katika chumba cha mwanaye. Alipofika alimkuta jasho likimtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi, alishangaa kumuona Mustafa amelala chini.
"Vipi?"
Shehna ilibidi amweleze mama yake kilichotokea aliposhtuka usingizini.

Itaendelea

NOW NAJIPANGA KUACHIA #NEW_STORY ONYESHA UPENDO MTU WANGU WA NGUVU #LIKE PAGE HIII UWE WA KWANZA KUIPATA STORY INAYOFUATIA GONGA LIKE TWENDE SAWA

0 comments:

Post a Comment