Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini -45
#SOON NAACHIA #NEW_STORY ILI USIPITWE NA STORY MPYA FANYA HIVI #LIKE_PAGE HII USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA SHARE STORY UNIPE MOTISHA YA KUPOST VIPANDE VINAVYOFUATAAA
ILIPOISHIA:
Shehna alianza kulia kitu kilichomshtua mama yake baada ya kudondokewa na machozi. Malkia Bi Zaldau, mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu alikwenda katika chumba cha mwanaye. Alipofika alimkuta mwanaye jasho likimtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi, alishangaa kumuona Mustafa amelala chini.
"Vipi?"
Shehna ilibidi amweleze mama yake kilichotokea aliposhtuka usingizini.
SASA ENDELEA...
"Shehna nani kawasha taa?" mama yake alishtuka kuiona hali ile.
"Sijui mama, labda Mustafa."
"Ina maana hukumueleza taratibu zetu?"
"Nilimueleza hata sijui likuwaje mpaka akawasha taa?"
"Ina maana alifanya kiburi cha kibinadamu?" Bi Zaldau aliuliza kwa hasira.
"Mama yaani sijui nimechanganyikiwa, jinsi ya kumuamsha na kumuuliza, lakini naogopa kumueleza mimi ni jini."
"Hivi vitu vyote unavyomfanyia hajashtuka na kukuona kiumbe wa ajabu."
"Huwa anashtuka lakini akili yake ilionekana ngumu kukubaliana kuwa mimi jini."
"Akijua jini?"
"Anaweza kuniacha nami nampenda sana."
"Basi tumfanye hamnazo."
"Hapana mama sitaki awe hivyo, ana familia inamtegemea unafikiri akiwa hivyo atafanyaje kazi?, Lazima atafukuzwa."
"Kila kitu tutaipa familia yake na wewe kuwaeleza masharti ya kukaa naye, hatakiwi kwenda kwa mganga mpaka ujifungue."
"Mamaa, umesahau mimi sitakiwi kutoka huku kipindi hiki."
"Mmh! Hapo ndipo penye tatizo."
"Au nimrudishe kwao."
"Kumrudisha umechelewa, fanya hivi, mtume jini mmoja akachukue nguo zake kwake kisha tumrudishe ofisini ili akishtuka aamini alikuwa amelala na kuota akiwa ofisini."
"Labda tufanye hivyo."
Walimchukua na kumrudishia fahamu kabla hajajitambua walimpuliza na kumfanya apitiwe na usingizi. Waliwatuma vibaraka kwenda kuchukua nguo za Mustafa nyumbani kwake na kuzipeleka haraka kisha walimvisha na kumpeleka ofisini kwake.
Kama kawaida ulifanyika kwanza usafi kisha walimweka kwenye kiti chake na kumuacha amelalia meza na kuondoka.
Mlio wa simu ulimshtua Mustafa kwenye usingizi mzito, alijishangaa kulala ofisini kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kumtokea hata siku moja.
Alipiga miayo na kuangalia saa yake, ilimuonesha ni saa tatu asubuhi. Simu iliyokuwa pembeni yake iliendelea kuita, aliichukua na kukuta inatoka kwa mkewe, alipokea mara moja.
"Haloo mke wangu."
"Mpenzi, vipi leo?"
"Kivipi mke wangu?"
"Imekuwaje leo umeondoka bila kuniaga?"
Swali hilo lilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza aliwezaje kuondoka bila kumuaga mkewe, kila alivyojiuliza alikosa jibu. Ukimya wa kujiuliza maswali ulimfanya mkewe kumuuliza.
"Mume wangu."
"Naam."
"Mbona hunijibu, au ulikuwa na kazi muhimu ofisini?"
"Ndiyo," Mustafa alikubali ili kuepusha maswali asiyoyaelewa kwa wakati ule.
"Hata kama hivyo, basi ungenipigia simu kunijulisha maana nimeshtuka kuamka asubuhi bila kukuona kitandani."
"Yaani simu yako ndiyo iliyonishtua na kuachana na kompyuta toka nilipoingia," alitengeneza uongo unaofanana na kweli japokuwa bado alikuwa hajielewi kwa vile alikuwa hakumbuki kama asubuhi alitokea nyumbani kwake.
"Pole mume wangu, lakini upo salama?"
"Asante nipo sawa sijui wewe mpenzi wangu niliyeondoka bila kukuaga."
"Mi sijambo, hujambo imeongezeka baada ya kuishusha presha yangu."
"Pole sana mke wangu."
"Asante, basi nikuache ufanye kazi."
"Asante mke wangu."
Baada ya kukata simu alijikuta mtu mwenye mawazo mengi sana baada ya kujikuta amelala ofisini bila kukumbuka alifika pale muda gani mpaka kumfanya alale ofisini tena kwa muda mrefu.
Alinyanyuka kitini na kujinyoosha mwili uliokuwa umechoka sana.
Baada ya kujinyoosha na kutengeneza nguo zake vizuri, alitoka nje ili kuzungumza na mlinzi kutaka kujua amefika saa ngapi mpaka kujikuta muda ule amelala. Alikwenda hadi getini, mlinzi alipomuona alimshangaa na kumuuliza kwa sauti ya juu.
"Bosi leo umelala ofisini?"
"Kwa nini?"
"Sijakuona kupita pia macho yamevimba kwa usingizi."
"John, jana nilipotoka hukuniona?"
"Nilikuona, ajabu sijakuona kupita kuingia lakini unatokea ndani ya ofisi."
"Una uhakika hujaniona napita kuingia ofisini?"
"Sijakuona ndiyo maana nakushangaa."
"Mmh! Ipo kazi."
"Kwani vipi, mbona kama huelewi?"
"John hebu njoo ofisini."
Mustafa aliongozana na mlinzi hadi ofisini ili wazungumze vizuri kwani muda ule alikuwa hajielewi. Baada ya kufika ofisini, Mustafa alimweleza mlinzi.
"Kaa chini."
John alikaa kwenye kiti kumsikiliza bosi wake, Mustafa baada ya kukaa alitulia kwa muda kuvuta kumbukumbu kwa yote yaliyomtokea na kutaka ushauri kwa mlinzi kwani alianza kuchanganyikiwa baada ya baadhi ya mambo kuyaona kama mauzauza. Muda wote John alikuwa ametulia akimuangalia bosi wake aliyekuwa ameinama.
"John," Mustafa alimwita huku akinyanyua kichwa kumtazama.
"Naam."
"Kuna kitu kinanichanganya sana."
"Kitu gani bosi?"
"Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya ndotoni au kweli?"
"Mambo gani?"
"Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja hapa?"
"Ndiyo."
"Unamuonaje?"
"Kivipi?"
"Unamuona yupo kama wanawake wengine?"
"Ndiyo, kwani vipi?"
"Ushawahi kuona mwanamke mzuri kama yule?"
"Mmh! Sijawahi, wewe umemtoa wapi? Kwa kweli ni mzuri sana tena sana, ajabu kila nikimuona mwili unanisisimka na mapigo ya moyo hunienda mbio."
"Unajua kwa nini?"
"Hata sijui."
"Mimi nina wasiwasi na yule mwanamke ni ji...."
Mustafa alinyamaza ghafla baada ya kumuona aliyekaa mbele yake hakuwa mlinzi John bali Shehna akiwa anamtazama uso wake umejaa machozi ya damu. Alishtuka sana mpaka akaanguka chini ya kiti, John aliyekuwa amekaa kwenye kiti alishtuka kumuona Mustafa akishtuka na kuanguka vile.
Alimuokota na kumkalisha chini kisha alimnyanyua kumrudisha kwenye kiti, lakini ajabu kila alivyoongea sauti haikutoka. John alishtuka na kujitahidi kumwita Mustafa ambaye alinyanyua mdomo kuzungumza kakini sauti haikutoka.
Alimpigia simu mkewe ambaye naye alifika mara moja. Alishtuka kumkuta mumewe kwenye hali ile.
Itaendelea
ONYESHA UPENDO #SHARE #LIKE_PAGE #COMMENT KUWA WA KWANZA KUIPATA #NEW_STORY FANYA HIVI LIKE PAGE USIPITWE NA STORY YENYE MVUTO ZAIDI NATUMAI UTAIPENDA. #Nakuelewa_sana_mtu wangu wa nguvu kipande hiki jana nilikisahau nikakiruka ili story ikamilike ukikisoma kipande hiki kama ulikuwa unafatilia story hiii nazani utakielewa na utaelewa story yenyew #NISAMEHE kwa hilo #Asanteeee
0 comments:
Post a Comment