Hadithi ya kusisimua #Mimba_Ya_Jini -43-
#Soon NAACHIA STORY NYINGNE NATUMAI MTAIPENDA CHAKUFANYA #LIKE_PAGE ILI USIPITWE NA STORY INAYOFUATA SHARE HADITHII HIII UNIPE MOTISHA YA KUPOST STORY NYINGINE ONYESHA UPENDO #MTU_WANGU_WA_NGUVU
ILIPOISHIA:
"Jamani lazima kutakuwa na tatizo, Sara jana si alilala chumbani kwake, ajabu asubuhi hatukumuona na kukuta mlango upo wazi na mbwa huyu alitoka ndani. Ajabu tulimfukuza asubuhi, usiku akarudi," shoga yake Happy alisema.
"Sasa Sara atakuwa wapi?"
SASA ENDELEA...
"Hapa ndipo tunachanganyikiwa maana hajaaga kama amepata dharura usiku."
Sara yote aliyasikia akiwa bado amesimama kwenye mlango wake, lakini alishindwa kuzungumza kwa kuhofia kubweka na kuwatisha, jambo ambalo lingewafanya wamfukuze kwa kumpiga. Akiwa bado amesimama mlangoni alisikia akiitwa jirani yake kwa sauti aje amfukuze.
"Baba John, yule mbwa wa asubuhi amerudi tena," mama John alimwita mumewe.
Sara alijua majanga bado yanamuandama, alilia kilio cha kimyakimya kwa kuogopa kutoa sauti kuwatisha. Alijiuliza atajitetea vipi ikiwa hawezi kuzungumza sauti ya kibinadamu. Alimuona jirani yake baba John akitoka ndani na kuuliza:
"Yupo wapi?"
"Yule pale kwenye mlango wa Sara."
"Huyu mbwa anatafuta kufa hapa subiri," alisema kwa sauti ya hasira aliyoisikia Sara.
Baba John alisogea pembeni na kuchukua gongo ili ampige, Sara alishangaa kusikia sauti iliyokuwa ikimtokea bila kumuona anayezungumza ikisema:
"Sara ondoka haraka watakuumiza."
Sara hakuchelewa alitimua mbio, alipoondoa mguu tu gongo lilitua kwenye mlango na kutoa sauti, alisikia sauti ya baba John akisema:
"Bahati yake lingempata angekufa, ------- kafie mbele kama umetumwa."
"Jamani huyu ni mchawi, huyu mbwa si bure, iweje ang'ang'anie hapa tena kwenye chumba kimoja cha Sara?" alisema Happy kwa uchungu.
Sara alitimua mbio mpaka nyumba ya jirani na kutweta huku akijiuliza nini hatima ya maisha yale?Alijiuliza atalala wapi usiku ule wenye baridi, kama angekuwa na uwezo wa kibinadamu basi angechukua kamba na kujinyonga. Njaa na kiu vilimshika, asingeweza kula jalalani au maji machafu. Kwake kilichobadilika kilikuwa umbile tu lakini akili ilikuwa ileile ya kibinadamu.
Wingu la mvua lilitanda na baridi ilizidi kuwa kali na kumfanya atetemeke, ilionesha mvua kubwa inaweza kuteremka wakati wowote. Aliona sehemu anayoweza kujistiri usiku ule ni mule kwenye jumba bovu lenye harufu kali ya kinyesi.
Alijiuliza nini hatima yake hata kama usiku ule utapita na atawezaje kulala na njaa na kesho yake aamke?
Hakuwa na jinsi kwani wingu lilikuwa zito, alikimbilia kwenye jumba lile na kuingia ndani ili mvua isimkute. Alisogea kwa ndani na kutafuta sehemu kavu kisha alijilaza chini, moyoni alijuta kutosikiliza maneno ya Shehna. Kiherehere chake kilimponza na kujiuliza hata kama Shehna ni jini, bado hakumuhusu kwa vile Mustafa hakuwa mumewe, wala ndugu yake na ujio wake pale hakumuathiri chochote.
Sara alilia sana lakini hakuna aliyesikiliza kilio chake kwa vile kilikuwa cha kujitakia, hakikuwa na pole. Njaa nayo ilizidi kumchonyota kwa vile toka asubuhi hakuwa ameweka kitu chochote tumboni wala kunywa maji. Hakuwa na jinsi, alikubaliana na yaliyokuwa mbele yake na kumuachia Mungu aamue maisha yake.
Majira ya saa saba usiku, mwanga mkali ulimpiga machoni, alipoangalia vizuri aliwaona wanawake wawili wazuri waliokuwa wamesimama mbele yake na kumwita jina lake.
"Sara."
Alishindwa kuitikia kwa kuhofia kubweka, aliwaangalia tu huku akijiuliza wale ni akina nani na wamejuaje yupo pale. Wale wasichana warembo walimwambia atoke ndani, alinyanyuka na kuwafuata. Alishangaa kuwasogelea bila kushtuka, alipowasogelea walimshika kichwani, ghafla Sara alirudi katika umbile la kibinadamu.
"Sara tumetumwa na Shehna tukuletee chakula."
"A..asa..sante," Sara alishukuru huku akipiga magoti.
Alijua baada ya chakula atabakia katika umbile lake la kibinadamu, alitoka nje ya jumba lile na kurudishwa kwenye chumba chake kisha akala chakula kile kitamu na kunywa maji.
Baada ya kula na kushiba alielezwa maneno yaliyomnyong'onyesha na kutamani ardhi ipasuke na kummeza.
"Sara, samahani tutakurudisha katika umbile la adhabu kisha tutakurudisha tulipokutoa."
"Jamani nisameheni, sirudii tena, nikirudia nifanyeni vyovyote," Sara alipiga magoti kuwaomba msamaha.
"Sara sisi hatujui sababu ya wewe kugeuzwa mbwa, tumetumwa tukuletee chakula tu, zaidi ya hapo hatuna mamlaka yoyote."
"Na..naomba unikutanishe na Shehna nimweleze haya."
"Sara unatuchelewesha," walimshika kichwani mara moja Sara akarudi katika umbile la mbwa. Wale wasichana warembo walitoweka ghafla na kumuacha Sara nje ya jumba bovu walipomtoa na kumrudisha.
****
Mustafa kila alipokuwa kazini, alikuwa na maswali mengi juu ya tumbo la Shehna kuwa kubwa kama puto lililojazwa hewa lakini lilikuwa laini na kupenda kulishika muda wote hata kumfanya kila siku alale kwa muda mchache.
Itaendelea
#SHARE HADITHI HII NIPOST KIPANDE KINACHOFUATA #LIKE PAGE HII #SHARE STORY #COMMENT NA USIKUBALI KUPITWA NA NEW STORY LIKE PAGE SOON NAACHIA HAPA HAPA
0 comments:
Post a Comment