MIMBA YA JINI-41

Author

Hadithi ya kusisimua  #MIMBA_YA_JINI -41-

ONYESHA UPENDO MTU WANGU WA NGUVU SHARE STORY NIPOST KIPANDE KINACHOFUATA LIKE PAGE USIPITWE NA STORY NYINGINE SOON ONYESHA UPENDO GONGA #LIKE #COMMENT #SHARE  TWENDE SAWA

ILIPOISHIA:
“Kweli labda kichaa anaweza kutuuma pia hata watoto wetu.”
Jirani mmoja alishika fimbo na kuingia chumbani kwa Sara na kushtuka kumuona mbwa juu ya kitanda.
SASA ENDELEA..

Alimtishia kumpiga ili atoke nje lakini Sara alitaka kujitetea kwa kuwaeleza kuwa yeye si mbwa ni mtu kama watu wengine lakini aliishia kumfokea kitu kilichoonesha anataka kumuuma.
Ilibidi jirani amtandike fimbo iliyomfanya Sara apige kelele kwa maumivu na kutoka nje ili kujiokoa na kipigo kile na kutokomea mitaani.
Kila mtaa alipopita watoto walimpiga mawe kitu kilichozidi kumweka kwenye wakati mgumu, yeye alijifahamu ni mwanadamu na si mbwa lakini kila kona alipopita aliitwa mbwa.
Alitafuta jumba bovu na kuingia humo kujificha japokuwa kulikuwa na kinyesi ambacho kilikuwa na harufu mbaya, lakini aliamini ile ni sehemu salama kwake kuliko kuzurura mitaani na kupigwa mawe na watoto.
***
Shehna baada kumtia adabu Sara japokuwa moyo wake haukupenda kutoa adhabu yoyote, alirudi nyumbani kwao na kuingia chumbani kwake na kuanza kulia sana, kitu kilichomshtua mama yake Bi Zaldau, mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu aliyempenda sana mwanaye Shehna kama mboni ya jicho lake, hakupenda hata siku moja kumuona akiumizwa na kitu.
Akiwa amejipumzisha chumbani kwake, alishtuka kuona machozi yamemdondokea kifuani, ile ilimjulisha mwanaye ana tatizo na muda ule alikuwa akilia.
Alijiuliza kipenzi chake Shehna kipi kimempata mpaka kulia machozi mengi yaliyomfikia yeye, alikwenda moja kwa moja chumbani kwa mwanaye na kumkuta akiendelea kulia.
“Shehna,” alimwita na kumfanya mwanaye ashtuke na kujifuta machozi haraka kisha alimgeukia mama yake.
“Shehna mwanangu una tatizo gani mama?”
“Hapana mama sina tatizo bali nimemkumbuka mpenzi wangu Mustafa.”
“Shehna nilikueleza mapema kuwa kama unamtaka mwanadamu, mtafute asiye na mke ungeweza kuja naye huku.”
“Mama, Mustafa nilimpenda muda mrefu sana lakini ninyi ndiye mliyenichelewesha kuonana naye mpaka akaoa mwanamke mwingine.”
“Ulikuwa bado hujatimiza umri wa kukutana na mwanaume.”
“Hata kama bado, nilitakiwa nionane naye mapema ili asioe mwanamke mwingine anisubiri mimi.”
“Hilo kweli tulifanya kosa, lakini mbona linawezekana kurekebishika.”
“Utalirekebisha vipi wakati ana mke tayari?”
“Si tunampoteza mkewe.”
“Hapana mama siwezi kufanya hivyo, kosa la mkewe lipi mpaka apotezwe?” Shehna alimkatalia mama yake kumuua mke wa Mustafa.
“Basi tumfanye asiwe na hamu na mumewe.”
“Vilevile sioni kosa lake.”
“Halafu mbona inaonesha kinachokuliza sicho unachonieleza, ulitoka na Kubash, mlikwenda wapi halafu juzi nilimuona Shush akiwa na damu mikononi, kuna nini ambacho sikijui?” mama Shehna mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu Malkia Bi Zaldau alihoji.
“Mama ndicho kinachoniliza, kuna msaidizi wa Mustafa ananifuatilia sana, nimejaribu kumtisha lakini hasikii. Jana usiku alikwenda kwa waganga wawili, mmoja alikataa kumtaka kumfanyia kazi yake lakini wa pili alikubali na kutaka kuniua. Wakati nimejilaza, nilianza kupoteza nguvu na kumwita Shush haraka awahi kumzima yule mganga kwani angechelewa ningekufa mimi.”
“Sasa umempa adhabu gani?”
“Nimemgeuza mbwa.”
“Shehna mtu anataka kukuua, unamgeuza mbwa adhabu gani hiyo isiyolingana na dhamira yake mbaya?” mama yake alikasirika.
“Mama hata kumgeuza mbwa kwangu nimeona ni adhabu kubwa sana, nilitaka kumuacha lakini imebidi nifanye hivyo.”
“Mwanangu huruma gani hiyo ya kujiumiza?”
“Mama, kosa lake kwenda kwa mganga bila hivyo wala asingenisumbua, nimemuua mganga kwa vile alitaka kuniua, zaidi ya hapo nisingesumbuka naye.”
“Mmh! Sasa kinakuliza nini?”
“Sipendi kuingia katika dhambi ya kulazimishwa.”
“Basi kama umempa hiyo adhabu inatosha, usilie mwanangu.”
“Sawa mama nimekuelewa.”
Shehna alijilaza kifuani kwa mama yake kuonesha amekubaliana naye.”
***
Mustafa alishtuka, siku ya pili alishtuka kufika kazini na kukuta ofisi bado imefungwa, alifungua na kuingia ndani. Ofisi ilikuwa chafu, hata hali ya hewa ilikuwa mbaya. Alijiuliza Sara atakuwa wapi mpaka muda ule, kitendo cha kuchelewa kazini kilizidi kumfanya amchukie Sara na kupanga akifika lazima amfukuze kazi.
Alishindwa kukaa ndani kutokana na hali aliyokuwemo na kutoka nje, alikwenda hadi kwa mlinzi ili akamwambie afanye usafi. Kabla hajafika kwa mlinzi, simu yake iliita. Alipoangalia ilikuwa inatoka kwa mpenzi wake Shehna.
Aliipokea na kuzungumza.
“Haloo mpenzi.”
“Haloo laaziz, vipi mpenzi wangu?”
“Safi tu.”
Itaendelea

#SOON NASHUSHA STORY NYINGINE CHAKUFANYA ILI #USIPITWE NA #NEW_STORY #LIKE_PAGE HII UWE WAKWANZA KUIPATA STORY YENYE MVUTO WAKIPEKEEE NAAMINI UTAIPENDAAA #LIKE PAGE #SHARE IWAFIKIE NA MARAFIKI

#SALUTI_NINJA_PICHANI_YULE_MKALI_WA_MASTORY_VITUKO_USHAURI #YUYUTZ SALUTI KWAKO MWANAAA.

0 comments:

Post a Comment