Hadithi ya kusisimuwa: #Mimba_ya_Jini-39-
ONYESHA UPENDO MTU WANGU WA NGUVU #SHARE HADITHI HII TWENDE SAWA #LIKE_PAGE USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HIII YA KUSISIMUA
ILIPOISHIA:
Sara na shoga yake waliona msala utawageukia, walitoka taratibu bila kuaga na kurudi nyumbani. Njia nzima Sara alijaa maswali na kukumbuka maneno ya mganga wa Vingunguti aliyemweleza kuwa mganga yeyote atakayetaka kuingilia kesi ile lazima moto umuwakie. Alipofika kwake aliteremka na kumuacha shoga yake arudi nyumbani kwake Kigogo.
SASA ENDELEA...
Alipofika alijikuta akizidi kukosa amani moyoni mwake na kujiuliza nini hatima yake baada ya kukaidi amri ya sauti ya kuacha kufuatilia mambo yasiyo muhusu Kilishomshtua zaidi kujua Shehna ni jini na ndiye aliyekuwa akimfanyia mauzauza yale.
Alijiuliza atamtazamaje hasa baada ya kumuasa aache kufuatilia mambo yasiyo muhusu. Alipofika nyumbani hakuwa hata na hamu ya kula, alinunua soda na keti, alikula kisha alioga na kupanda kitandani.
Usiku wa manane akiwa amelala alishtushwa na sauti kali ya vicheko mfululizo, alifumbua macho kutazama na kukutana na kiza kizito. Vicheko viliendelea mpaka kikawa kero masikioni mwake, mapigo ya moyo yalimwenda mbio kwa hofu.
Alipapasa pembeni ya kitanda na kushika swichi ya kitandani na kuwasha taa.
Ilipowaka alishtuka kuona viumbe wa ajabu mbele yake wakiwa wamesimama sambamba na ukuta. Walikuwa watu weusi sana wanne wenye mikia mifupi kama ya mbuzi na pembe ndogo kichwani. Sara alishtuka na kutetemeka kwa hofu huku haja ndogo ikimtoka bila kujijua.
Alijiuliza wale ni kina nani na wamefuata nini, wazo lake lilielekea moja kwa moja kwa wachawi. Akiwa bado hajajua nini kinaendelea aliiona ardhi ikipasuka na kuingia mwanamke aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha dhahabu cha kifalme kilichokuwa kimebebwa mabegani na wanaume wengine wanne weusi wenye miili mikubwa na mikia kama wenzao lakini hao walikuwa na pembe moja katikati ya kichwa tofauti na wale wengine waliokuwa na pembe mbili.
Wale viumbe wa ajabu waliendelea kukibeba juu kiti kilichokaliwa na mwanamke mrembo mpaka ardhi iliyopasuka kujifunga ndipo walipomtua chini. Sara aliendelea kutetemeka huku akiwa amejikunyata upenuni mwa kitanda akiwa umesogea ukutani kabisa.
Yule mwanamke alikuwa amempa mgongo, alipopiga kofi aligeuzwa kumtazama, Sara hakuamini macho yake kumuona aliyekuwa mbele yake ni Shehna rafiki wa bosi wake. Baada ya kutulia alipiga makofi, viumbe vile vya ajabu vilitoweka na kubakia peke yake akiwa bado amekaa kwenye kiti chake cha dhahabu.
Baada ya kubaki wawili, Shehna aliteremsha pumzi nzito na kunyanyuka kwenye kiti na kusimama. Alimtazama Sara aliyekuwa bado amejikunja pembeni ya ukuta kwa woga. Alitembea taratibu kukizunguka chumba, alipompa mgongo alishtuka kumuona Shehna ana mkia mkubwa kama wa kangaroo lakini ule ulikuwa umenenepa sana.
Alipofika mwisho wa ukuta aligeuka akiwa amegeuka sura yake na kuwa ya kutisha meno yake yaligeuka kama ya ngiri juu ya paji la uso kulikuwa na pembe mbili kama za faru. Macho yake yalikuwa yakiwaka moyo, alicheka kicheko kizito kilichofanya Sara atokwe damu masikioni.
Shehna alikuwa kiumbe cha kutisha ambacho Sara hakuwahi kukiona maishani mwake, kwa sauti kali Shehna alisema huku moto ukitoka mdomoni.
“Sara umenichimba sana, sasa umenijua haya niambie shida yako?”
“Ni..ni ..samehe She..she...”
“Sara sitakusameha lazima utajua faida ya kiburi chako, nilikuonya kwa sauti hukusikia nikaja mwenyewe hukunielewa, nina imani ulitaka uone nini kitatokea baada ya wewe kufuatilia mambo yasiyokuhusu. Nimekutisha ninavyojua lakini kichwa chako kimejaa kiburi nami nataka nikuonesha jeuri yangu.
“Sitakuua bali nitakupa adhabu ya kipindi chote nitakapokuwa sipo chagua adhabu moja, nikugeuze Nguruwe, Chura, Funza maisha yako yote yawe kwenye kinyesi, bundi au mbwa?”
Sara hakujibu, alijitahidi kumsogelea Shehna ili amuombe msamaha.
“Shehna nisamehe shoga yangu.”
“Wewe si shoga yangu, mlitaka kuniua na mganga wako bila kosa, nimekukosea nini Sara?” Shehna alirudi katika umbile la kibinaadamu na kuanza kulia machozi ya damu.
“Ni sa..samehe sirudii tena.”
“Sitaki kusikia sauti yako, umetaka kunijua leo umenijua mimi ni jini, ujini wangu umekuathiri nini katika maisha yako?”
“Najua nimekukosea naomba unisamehe sirudii tena.”
“Sara sitakusamehe ukichelewa kuchagua adhabu yako nitakugeuza kiumbe cha ajabu kisicho na mfano.”
Itaendelea
SHARE #LIKE_PAGE TWENDE SAWA USIKUBALI KUPITWA NA KIPANDE KINACHOFUATA KAMA BADO UJALIKE PAGE LIKE SASA UWE WA KWANZA KUPATA KIPANDE KINACHOFUATA
0 comments:
Post a Comment