MIMBA YA JINI -35

Author

Hadithi ya kusisimuwa: #Mimba ya jini-35-

#LIKE_PAGE USIPITWE NA HADITHI HII SHARE ZIKIWA MINGI NAPOST MWENDELEZO WAKE ONYESHA UPENDO

KWA WALE WANAOLAKAMIKA STORY FUPI NATUMIA FACEBOOK LITE HAIBEBI MANENO MENGI NISAMEEN KWA HILO JAMANI.

ILIPOISHIA :
"Ila mpenzi kwa mwezi mzima hatutaonana, nakwenda nyumbani mara moja kufanya mambo ya kimila baada ya kupata ujauzito."
"Mmh! Mpenzi nitateseka, nilikuzoea sana."
"Usiwe na wasiwasi nitakuwa nawe karibu muda wote."
"Tutakuwa pamoja kivipi wakati hautakuwepo kwa mwezi mzima?"
"Kila siku nitakuwa katika ndoto zako na ukiamka wala hutakuwa na majozi, usiku utakuwa kama mchana tena upo na mimi."
SASA ENDELEA...

"Sawa," Mustafa hakutaka kubishana na Shehna kwa kuamini kabisa alikuwa akipewa moyo kwa kujua siku zote furaha ya ndotoni ni maumivu ya asubuhi.
"Nilitaka kusahau, sasa hivi ruksa kukutana kimwili na mkeo."
"Hata bila ya dawa?"
"Yaleyale mafuta mtajipaka sehemu za siri kabla ya kukutana, ila lazima mkutane mara mbili kwa wiki, Jumatatu na Ijumaa."
"Kwa nini tukutane siku hizo?"
"Ndizo siku zenye nyota ya mtoto zaidi ya hapo mtakuwa mnatenga maji kwenye kinu."
"Basi tunaweza kukutana siku zote ila Jumatatu na Ijumaa ndiyo muhimu."
"Mustafa hiyo unapanga wewe, hii ni dozi ya kutafuta mtoto mkienda kinyume na hapo mtoto mtamsikia kwa kilio, akilia nyumba ya jirani."
"Nimekuelewa mpenzi."
"Najua sasa hivi huna matatizo ya fedha, kama utakuwa na shida amka usiku, washa udi utaweza kuniona ndotoni na kunieleza matatizo yako, kama ni fedha kabla ya kuondoka washa udi acha ufunguo mnapouacha ili niweze kukuletea hela."
"Shehna hivi wewe ni nani hasa?"
"Kivipi?"
"Bado nipo njia panda, wewe ni mganga au ji.., hapana sivyo ila naomba uniweke wazi maana mpaka sasa nipo njia panda," Mustafa alimuuliza huku amemkazia macho.
"Mustafa kipi kimekufanya unitilie shaka hivyo mpenzi wangu?" Shehna alimuuliza Mustafa huku machozi yakimtoka, kitu kilichomfanya Mustafa ajutie swali lake.
"Basi samahani mpenzi kama swali langu nimekukwaza."
"Mustafa mpenzi kipi nimekufanyia kibaya mpaka unifikirie hivyo au umenichoka mpenzi wangu?
Mapenzi yote ninayokupa unayaona bureee?" Shehna aliendelea kulia huku machozi yakimtoka kama maji.
Mustafa alijikuta akijilaumu kwa swali lake ambalo liliharibu furaha yake ya siku ile.
Alijutia nafsi yake kwa swali la kipumbavu lakini aliendelea kumbembeleza Shehna amsamehe kwa swali lake lile.
"Shehna mpenzi nisamehe kwa swali langu la kipuuzi."
"Mustafa mpenzi nikujali vipi? Siku zote nimekuwa nikikujali mbona sijawahi kukuuliza swali kama hilo?
"Au wema wangu wa kujitolea kwako ndiyo umeniponza?" Shehna alilia mpaka akawa mwekundu.
Mustafa alichanganyikiwa na kujikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kupiga magoti mbele ya Shehna na kuanza kulia huku akiomba msamaha kwa kuamini Shehna ni mtu muhimu sana katika maisha yake kutokana na kumsaidia vitu vingi.
Kilio cha Mustafa kuomba msamaha kilimshtua Shehna ambaye siku zote hakupenda kumuona Mustafa akitoa machozi mbele yake.
Alimshika na kumnyanyua na kutazamana kila mmoja, macho yake yakiwa yamejaa machozi.
Machozi ya Shehna yalimfanya aongezeke uzuri maradufu na kuzidi kuutesa moyo wa Mustafa, kumpoteza kiumbe mzuri kama yule.
"Mustafa," Shehna alimwita kwa sauti ya kinanda.
"Naam."
"Nisamehe mpenzi," Shehna alisema huku akimfuta machozi kwa mtandio.
"Shehna huna kosa, mwenye makosa ni mimi niliyetoa machozi yako."
"Hapana Mustafa nakupenda sana, nimeumizwa na machozi yako, narudia tena naomba unisamehe."
"Nimekusamehe japo sioni kosa lako, naomba na mimi unisamehe."
"Nimekusamehe mpenzi wangu nami nashukuru kwa kunisamehe."
Walikumbatiana kila mmoja akirudisha furaha yake. Baada ya utulivu wa muda, Shehna alimuomba Mustafa atoke nje mara moja. Alimruhusu hakuchelewa alirudi baada ya dakika mbili akiwa na vinywaji mkononi. Aliviweka juu ya meza na kwenda kwenye friji ndogo na kutoa glasi mbili. Itaendelea
ONYESHA UPENDO #LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE  HATA MOJA #New_Story_SOON

0 comments:

Post a Comment