Hadithi ya kusisimuwa: #Mimba ya jini-34-
UNYESHA UPENDO #SHARE STORY NIPOST KIPANDE KINACHOFUATA #LIKE_PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA SHARE ZIKIWA MINGI NAPOST VIPANDE VIWILI
ILIPOISHIA:
Shehna alikuwa amevaa dela zuri lililonakshiwa na nyuzi za hariri, alikuwa amenawiri na kupendeza, alionekana mwanamke mrembo zaidi ya siku zote.
"Asante."
"Da Shehna hongera umependeza sana."
"Nashukuru."
"Karibu dada a'ngu."
SASA ENDELEA...
"Nimekaribia, vipi umeamkaje?"
"Namshukuru Mungu leo nimeamka salama."
"Vipi ile hali ilitokea tena?"
"Kwa kweli mpaka nakuja kazini nashukuru hali ile wala sauti haijanitokea tena."
"Kama nilivyokueleza, zingatia uliyoambiwa na ile sauti yana sababu, utashangaa mambo yako yatakwenda vizuri."
"Asante dada kwa msaada wako pia nitazingatia ushauri wako."
"Vipi bosi yupo?"
"Yupo pita."
"Hapana muulize kwanza."
Sara alinyanyua simu na kumpigia Mustafa aliyemwambia amruhusu aingie.
"Dada pita."
"Asante."
Shehna aliingia ndani ya ofisi alikutanisha macho na Mustafa aliyekuwa akiangalia mlangoni.
"Wawooo mpenzi."
Mustafa alijikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea kwa kumkumbatia kisha alimchumu.
"Asante mpenzi," Shehna alishukuru baada ya kubusiwa kwenye shavu.
Waliachana kwa kila mmoja kukaa sehemu yake, Shehna alionekana mwenye furaha usoni mwake tofauti na siku zote. Alimuangalia Mustafa usoni alitaka kusema neno lakini aliishia kutabasamu na kufanya uzuri wake uongezeke.
"Vipi mpenzi?" Mustafa alimuuliza huku naye akijenga tabasamu mwanana lililokuwa likimpa uhuru Shehna kuzungumza.
"Mmh! Mustafa nashukuru sana."
"Kwa kipi?"
‘Kwa vyote, lakini kimoja ndicho nimefurahi sana tena sana sipati kusema."
"Vipi hivyo na kipi kimekufurahisha sana?"
"Nikwambie?" Shehna alimuuliza Mustafa huku akimtazama kwa jicho la aibu.
"Niambie mpenzi," alitoa tabasamu la kumruhusu aseme kilichokuwa moyoni mwake.
"Kwanza nashukuru kwa kunipa nafasi moyoni mwako, pili kunivumilia kwa usumbufu wangu, tatu kunipa penzi ambalo sijawahi kupata katika maisha yangu yote na kubwa zaidi nimekuja kukueleza sasa hivi mimi ni mjamzito."
"Wewe!" Mustafa alishtuka.
"Kweli kabisa, unakumbuka jana ilikuwa siku ya ngapi mimi kulala kwako?"
"Mmh! Hata sikumbuki."
"Muone!" Shehna alisema huku akimshika kidevu Mustafa.
"Jana mpenzi ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kukutana kimwili, mpaka juzi bado sikuona mabadiliko. Nilichanganyikiwa mtoto wa kike, lakini penzi ulilonipa jana lilikuwa tamu ajabu kidogo nife kwa raha kumbe watoto walikuwa wanaingia."
"Kweli?"
"Kweli kabisa nami si muda mrefu nitaitwa mama."
"Hongera!" Mustafa alisema huku akizunguka meza na kumkumbatia.
"Hongera wewe kunipatia nilichokitafuta kwa muda mrefu."
"Basi tuongere wote."
"Mustafa mpenzi, kuanzia leo hatutaonana mchana kwa vile sipendi kutembea na tumbo."
"Mbona bado sana?"
"Siwezi kutembea, familia yetu ikibeba ujauzito husumbuka sana."
"Sawa mpenzi, lakini nyumbani si utakuja?"
"Hapana ila nitawatuma watu wakufuate usiku siku mojamoja na alfajiri watakurudisha."
"Hakuna tatizo."
"Ila mpenzi kwa mwezi mzima hatutaonana nakwenda nyumbani mara moja kufanya mambo ya kimila baada ya kupata ujauzito."
"Mmh! Mpenzi nitateseka, nimekuzoea sana."
"Usiwe na wasiwasi nitakuwa nawe karibu muda wote."
"Tutakuwa pamoja kivipi wakati hautakuwepo kwa mwezi mzima?"
"Kila siku nitakuwa katika ndoto zako na ukiamka wala hutakuwa na majonzi, usiku utakuwa kama mchana tena upo na mimi."
Itaendelea
SHARE STORY NIPOST KIPANDE KINGINEEE #LIKE PAGE TWENDE SAWAAAA
0 comments:
Post a Comment