MIMBA YA JINI -33

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-33-

ILI USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HII #LIKE_PAGE SHARE STORY NIPOST KIPANDE KINACHOFUATAAA

ILIPOISHIA:
“Sara umefika salama?” sauti haikuwa ngeni lakini hakuwa na uhakika nayo ilibidi aulize.
“Nani?”
“Mi shogayo Shehna.”
“Aah! Dada nimefika salama.”
“Ile hali haijatokea?”
“Ndi..ndiyo.”
“Mbona kama una wasiwasi?”
“Ni kweli kuna sauti naisika kwa mara ya pili lakini siielewi.”
“Inasemaje?”
SASA ENDELEA...

“Inasema niache kufuatilia mambo yasiyonihusu la sivyo nitageuzwa nguruwe kabisa.”
“Kwani unafuatilia nini?” Shehna alijifanya kuuliza.
Swali lile lilikuwa gumu kwa vile asingeweza kumueleza anamfuatilia yeye, alibidi adanganye kwa kusema:
“Dada wee nimfuatilie nani?”
“Haiwezekani sauti hiyo kutokea mara ya pili, kama kuna kitu unakifuatilia achana nacho kwa vile kila kitu cha ajabu kikikutokea kina sababu.”
“Nimekusikia dada yangu.”
“Hebu acha kufuatilia hicho ulichotaka kukifuatilia tuone nini kitatokea.”
“Sawa dada.”
“Basi mdogo wangu oga kisha kunywa maji ya baridi ulale.”
“Nitafanya hivyo dada.”
Sara alikwenda kuoga kisha alikunywa maji ya baridi na kujikuta akipitiwa na usingizi mzito.
***
Sara aliamka siku ya pili bila kutokewa na mauzauza yoyote, alikwenda hadi kazini kama kawaida na kukuta ofisi haijafanyiwa usafi. Aliingia katika kazi ya kufanya usafi kama kawaida yake na kusubiri muda wa bosi wake kufika. Baada ya muda Mustafa aliwasilili na kupokewa na Sara.
Kama kawaida alichukua vitu vya bosi na kwenda kuviweka ofisini, Mustafa alipoingia ofisini alishangaa kukuta ofisi chafu. Hata hali ya hewa haikuwa kama ile aliyoizoea wakati wa Shehna akifanya usafi. Alitoka hadi kwa Sara na kumuita.
“Sara njoo mara moja.”
Sara alinyanyuka na kwenda kwa bosi wake kumsikiliza alijua anaitiwa kazi ya siku ile. Alipofika alikutana na swali lililomshtua.
“Sara kazi imekushinda?”
“Kwa nini bosi?”
“Mbona ofisi inanuka kama zizi la ng’ombe.”
“Bosi mbona mi sisikii harufu yoyote mbaya?”
“Ina maana husikii harufu mbaya ya ofisi?”
“Bosi kipi kimeongozeka, nimefagia na kufuta kama siku zote sasa hiyo harufu kama zizi imetoka wapi?”
“Sara kazi imekushinda heri usingerudi ofisi yangu ikaendelea kusafishwa na Shehna, unakuwa kama upo bustanini lakini kurudi kwako hakuna ulichokifanya zaidi ya kuongeza uchafu.”
“Bosi mbona sikuelewi hiyo harufu kama beberu ipo wapi?”
Ghafla ndani ya ofisi ilisikia harufu nzuri ya manukato aliyoizoea, alimwambia Sara aondoke.
“Sara kaendelee na kazi.”
“Asante bosi.”
Sara alitoka na kwenda kuendelea na kazi, wakati akifanya kazi alijikuta mtu mwenye mawazo mengi juu ya tukio la muda mfupi uliopita la bosi wake kumgeuka kuwa hajafanya usafi na kusema ofisi inanuka kama zizi. Kilichomshangaza kingine kilikuwa harufu nzuri ya manukato iliyoingia ghafla ofisini ambayo hakujua yametoka wapi.
Hakutaka kusema kitu aliendelea na kazi na kupanga akitoka kazini jioni lazima aende kwa mganga wake ili amuangalizie kinachomtokea ni nini kwa vile haikuwa hali ya kawaida kwa mtukio yote.
Wakati akiwaza vile alishtuliwa na sauti ya Shehna.
“Shoga za kazi?”
“Ooh! Dada karibu,” alisema huku akionesha kushtuka.
Shehna alikuwa amevaa dela zuri lililonakshiwa na nyuzi za hariri, alikuwa amenawiri na kupendeza alionekana mwanamke mrembo zaidi ya siku zote.
“Asante.”
“Da Shehna hongera umependeza sana.”
“Nashukuru.”
“Karibu dada a’ngu.”

Itaendelea

ONYESHA UPENDO #LIKE_PAGE SHARE STORY NIPOST MWENDELEZO

0 comments:

Post a Comment