Hadithi ya kusisimua #Mimba ya jini-32-
LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA ONYESHA UPENDO SHARE HADITHI NIPOST KIPANDE KINACHOFUATA
ILIPOISHIA:
Sara alishindwa kuzungumza mbele ya Shehna jambo ambalo aliliona na kuomba kutoka nje.
"Mustafa nipo nje zungumza na mfanyakazi wako."
"We baki, kumbuka kabla ya wewe kuja alikuwa haongei."
"Hapana hili ni la kikazi, zungumzeni tu," Shehna alisema huku akitoka nje ya ofisi na kwenda kukaa mapokezi.
SASA ENDELEA...
Ofisini walibakia Mustafa na Sara aliyekuwa amesimama.
"Kaa," Mustafa alimwambia Sara.
Sara alikaa kwenye kiti, Mustafa aliendelea kusimama.
"Sara," alimwita."
"Abee."
"Una tatizo gani?"
Sara ilibidi amueleze mkasa mzima kuanzia siku aliyotoka kwenda kununua nyama ya nguruwe. Lakini alificha kufuata nyama ya nguruwe na kusema alifuata chakula cha usiku na yaliyomtokea na vituko vilivyokuwa vikimtokea toka siku aliyofika nyumbani na ofisini.
"Sara mbona unafanya utani."
"Kweli bosi, siwezi kusema uongo."
"Kwa hiyo hata hapa ilitokea?"
"Kule ilikuwa tisa kumi hapa mpaka sauti katoa."
"Mmh! Itakuwa nini? Hebu ngoja," Mustafa alisema huku akielekea mlangoni na kuufungua kisha aliita.
"Shehna njoo."
"Vipi mmemalizana?"
"Hebu njoo mara moja."
Shehna aliingia ofisini na kusimama pembeni ya Mustafa ili kusikiliza alichoitiwa.
"Unasemaje?"
Alimweleza yote yaliyomtokea Sara, baada ya kumsikiliza alisema.
"Mmh! Pole, lakini maji aliyokunywa yatamsaidia haitamtokea hali ile tena."
"Kwa hiyo aendelee na kazi au akapumzike?"
"Mwache akapumzike ili kesho aanze kazi vizuri."
Mustafa alimpa ruhusa Sara akapumzike ili kesho aende kazini, Sara alishukuru na kuondoka na kutaka kutoka lakini alikumbuka alichafua chini kwa haja ndogo baada kumtoka bila kujijua kutokana na hofu ya maruweruwe.
Alikwenda msalani kuchukua Mop kwa ajili ya kufanya usafi, alipoingia Shehna alimuwahi na kumwambia.
"Shoga kapumzike nitakusaidia mimi."
"Acha tu dada."
"Hapana kapumzike."
Sara alikubaliana kumpa Mop Shehna na kuondoka kuelekea nyumbani, lakini Shehna alimwambia Mustafa.
"Mustafa mpeleke Sara, ukirudi utakuta nimemaliza kufanya usafi."
"Sawa."
Mustafa alitoka kumpeleka Sara nyumbani na kumpa nafasi Shehna kufanya usafi. Baada ya kuondoka tu Shehna aliwaita vijakazi wake ambao walianza mara moja kazi ya usafi.
Mustafa alimpeleka Sara mpaka nyumbani na kumuacha kisha alirudi nyumbani na kumkuta Shehna kaisha maliza kazi ya usafi. Baada ya kuachwa Sara aliingia chumbani kwake na kujikuta akianguka kilio kutokana na matukio yaliyokuwa yakimuandama kila kukicha.
Katikati ya kilio aliisikia tena sauti aliyoisikia wakati alipomuona nguruwe ofisini kwa bosi wake.
"Kulia siyo dawa zaidi kuacha kuyafuata mambo yasiyo kuhusu la sivyo utageuka nguruwe kabisa."
Sauti ile ilimfanya anyamaze na kujiuliza kitu gani ambacho amekuwa akikifuatilia zaidi ya kutaka kumjua Shehna ambaye kwa jinsi alivyomuona na upole wake aliamini si jini bali kiumbe cha kawaida tena mwenye upendo tofauti na alivyomfikiria. Hakuamini mwanamke mrembo kukubali kusafisha haja yake ndogo.
Lakini alimuhakikishia hali ya kumtisha haitamrudia tena, haikuwa kama alivyomwambia na kusikia sauti ile. Akiwa hajapata jibu simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni. Alipokea na kuzungumza.
"Haloo."
"Sara umefika salama?" sauti haikuwa ngeni lakini hakuwa na uhakika nayo ilibidi aulize.
"Nani?"
"Mi shogayo Shehna."
"Aah! Dada nimefika salama."
"Ile hali haijatokea?"
"Ndi..ndiyo."
"Mbona kama una wasiwasi?"
"Ni kweli kuna sauti naisika kwa mara ya pili lakini siielewi."
"Inasemaje?"
Itaendelea LIKE PAGE USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HII YAKUSISIMUA SHARE HADITHI NIPOST KIPANDE KINACHO ENDELEA
JAMANI NATUMIA #FACEBOOK_LIKE KUPOST HADITHI HAIBEBI MANENO MENGI #MSILALAMIKE STORY NI FUPI FACEBOOK LITE NAZAN UNAIELEWA ASANTEN KWA KUWA NAMI NA KUSHARE STORY HIIIIII
0 comments:
Post a Comment