MIMBA YA JINI 31

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-31-

KAMA BADO UJALIKE PAGE HII LIKE SASA USIPITWE NA HADITHI HII INAYOENDELEA #LIKE PAGE TWENGE SAWA HADI MWISHO WA STORY HIII

ILIPOISHIA
Hakukuwa naiko zaidi ya kuona nguruwe amesimama kwenye kiti cha bosi wake akichezesha pua. Alikaza macho kuangalia kama anachokiona ni kweli au maruweruwe. Bado hali ilibakia ileile ya kumuona nguruwe mbele yake. Alipekecha macho ili kuikataa hali ile kwa kuamini yale yalikuwa maruweruwe kama yaliyomtokea jana yake.
SASA ENDELEA...

Aliamini yule ni nguruwe kweli wala si bosi wake baada ya kutoka mlio wa nguruwe ambao ulimfanya apige kelele za woga.
“Mamaa nakufa!”
Alishangaa nguruwe yule kuzungumza kwa sauti ya kibinadamu:
“Sasa unaogopa nini wakati ulifunga safari kunitafuta mpaka Dodoma, nimekuja unapiga kelele.”
“Ha..hapana..hapana,” Sara alikataa huku akitikisa kichwa.
“Mimi muongo hujatoka nyumbani kwako kunifuata unilete ofisini?”
“Ha..ha..hapana,” Sara kwa woga haja ndogo ilimtoka bila kujijua.
“Saraaaa!” Sauti kali ya Mustafa ilimshtua.
Hakuitika alishika mikono masikioni kuzuia sauti ya nguruwe, alishangaa kumuona bosi wake akiwa amesimama mbele yake huku akimshangaa.
“Sara nini?” alimuuliza kwa sauti kubwa baada ya kushindwa kumuelewa.
“Nakufa bosi,” alisema huku pumzi zikimtoka kama alikuwa akikimbizwa na simba.
“Sara kipi kinakuua?”
“Mungu wangu nakufa..nakufa mimi,” Sara alisema huku akikaa chini baada ya nguvu kumuishia na kuhema kwa nguvu.
Mustafa alizunguka meza na kumsogelea Sara aliyekuwa amekaa chini, alimshika kichwani na kumuuliza kwa sauti ya upole.
“Sara una nini?”
Sara pumzi zilikuwa zimemjaa na kushindwa kuzungumza, alijiuliza amekumbwa na nini kwa vile kitu kama kile kilikuwa hakijawahi kumtokea. Sara alikuwa akitetemeka na jasho kumtoka kitu kilichozidi kumtia kwenye wakati mgumu Mustafa kwa kuamini angesema angejua tatizo lake.
Akiwa katika kizungumkuti asijue nini kimemtokea Sara ambaye aliendelea kuhema huku macho kayatoa pima. Mlango uligongwa na kumfanya ahamishe macho yake kuelekea mlangoni bila kuitikia. Mlango uligongwa tena hakutaka kumkaribisha mtu ndani kutokana na hali ya Sara ilivyokuwa aliamua kusogea mlangoni.
Alikwenda hadi mlangoni na kufungua, alijikuta akikutana uso kwa uso na Shehna.
“Ha! Karibu!”
“Mbona umeshtuka?”
“Sikutegemea kukuona.”
“Kwa nini unasema hivyo au kuna muda uliopanga mimi kuja hapa.”
“Walaa, karibu.”
“Asante.”
Sauti ya Shehna ilimshtua Sara ambaye mapigo ya moyo yaliyoanza kupoa, yalianza upya tena kwa kasi kubwa. Alijiuliza nini hatima yake kama kweli ni jini na kama ndiye aliyekuwa akimfanyia mchezo ule nini atamfanya. Alitamani kumuomba msamaha lakini alijiuliza ataanzia wapi ikiwa hana uhakika yale yalikuwa mawazo yake tu.
Shehna aliingia ndani ya ofisi na kushtuka kumuona Sara amekaa chini.
“Mustafa! Shoga yangu kafanya nini tena?”
“Yaani nashangaa ameingia ofisini tu na kuanza kupiga kelele.”
”Kelele! Kipi kimemtisha?”
Sara alijikuta njia panda kutokana na maneno ya Shehna yalimshangaza na kuona kama mawazo yake ni tofauti na alivyokuwa akifikiria.
“Ha...halafu si ulisema alisafiri amerudi lini?”
“Ulinisikia vibaya nilisema haonekani ofisini sikujua amekwenda wapi.”
“Sasa nini kimemsibu?”
“Hata najua? Namuuliza amegeuka bubu, yaani nachanganyikiwa.”
“Sasa kipi kimemsibu jamani shoga yangu?” Shehna alisema huku akimsogelea na kumuinamia Sara.
“Eti Sara umepatwa na nini?”
Sara bado mdomo ulikuwa mzito kwa vile mapigo ya moyo bado yalikuwa juu.
“Mustafa niletee maji ya baridi niwekee kwenye glasi.”

Je, nini kitaendelea.

KAMA BADO UJALIKE PAGE HII LIKE SASA USIPITWE NA HADITHI HII INAYOENDELEA #LIKE PAGE TWENGE SAWA HADI MWISHO WA STORY HIII

0 comments:

Post a Comment