Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-30-
KAMA BADO UJALIKE PAGE LIKE SASA USIPITWE NA HADITHI HII INAYOENDELEA
ILIPOISHIA:
"Wazo zuri lakini lazima nifike kwanza ofisini nijue hatima yangu ndipo twende huko kanisani."
"Basi ukirudi jioni tutapanga."
"Sawa."
Sara aliagana na shoga yake na kuwahi kazini kama kawaida ili afanye usafi kabla bosi wake hajafika.
SASA ENDELEA...
Mlinzi alimpa ufunguo kama kawaida, alifungua ofisi na kushtuka kuikuta safi imeisha safishwa. Hali ile ilimshtua na kumfanya atoke nje mpaka kwa mlinzi na kumuuliza;
"Eti nani kafanya usafi?"
"Wapi?"
"Ndani ya ofisi?"
"Wewe ndo wa kwanza kuja sijamuona mtu yeyote."
"Kwa...kwa niiii toka nilipoondoka nani alikuwa akifanya usafi?"
"Kwani da Sara ulienda wapi?"
"John si muhimu kujua, nijibu swali langu."
"Toka uondoke sijawahi kumuona mtu akifanya usafi, nakumbuka siku ambayo wewe hukuja bila taarifa nilitaka kwenda kufanya usafi lakini bosi alinikataza, tokea siku hiyo sijamuona mtu akifanya usafi."
"Ina maana toka niondoke hakuna mtu uliyemuona anafanya usafi?"
"Sijawahi kumuona."
"Mbona ofisi inaonesha imefanyiwa usafi muda si mrefu tena wa hali ya juu?"
"Basi majini ndiyo yamefanya usafi," mlinzi alisema kwa utani.
"John na wewe umeligundua hilo?"
"Lipi?"
"La kuwepo na jini ofisini?"
"Mi nimesema tu, hilo jini lifanye usafi kwa ajili gani?"
"Kama mimi nilikuwa sifanyi usafi, basi nani amefanya?"
"Mmh! Labda bosi."
"Nataka kukuambia hapa kuna mchezo, unamjua yule mwanamke?"
"Mwanamke gani?"
"Yule mrembo anayekujaga ofisini."
"Ndiyo."
"Yule nina wasiwasi siyo mtu wa kawaida."
"Una maanisha nini?"
"Mimi simwelewi huenda ni jini!"
"Jini? We acha mambo ya ajabu angekuwa jini tungemuona?"
"Nakwambia ipo siku utakubaliana na mimi."
"Kwa hiyo bosi wateja wake wengine ni majini?"
"Hebu kwanza nikuulize?"
"Uliza."
"Tangu niondoke yule mwanamke kaja mara ngapi?"
"Kwa kweli sijamuona."
"Muongo!"
"Kweli."
"Basi we subiri kama ni yeye nitakomeshana...na...na,"Sara alinyamaza baada ya kuliona gari la bosi wake likisimama getini.
Hakutaka kuongeza neno alichepua mwendo kuwahi ofisini, alijisikia vibaya bosi wake kumkuta eneo lile badala ya ofisini. Lakini alipanga kujitetea alikuwa akimuuliza kitu mlinzi.
Mustafa toka akiwa ndani ya gari alishtuka kumuona Sara, baada ya kupaki gari alielekea ofisini na kupokewa na Sara kama ilivyokuwa kawaida na kupeleka vitu ndani.
Wakati wa kupokelewa alitaka kukataa lakini hakuona sababu ya kukataa, alimuacha apokee lakini alitaka maelezo ya kina atakapomuuliza ili aendelee na kazi lakini kinyume na hapo alipanga kumfukuza kazi kwani tangu aondoke hakukuwa na pengo lolote.
Baada ya kutulia kwa muda Sara aliingia ofisini kwa bosi wake akiwa hajiamini na kufika kusimama mbele ya bosi wake. Mustafa aliacha kusoma gazeti la siku ile na kunyanyua uso wake kumtazama.
"Shikamoo," Sara alimuamkia kwa kupiga magoti.
Ilikuwa mara ya kwanza Sara kumuamkia kwa heshima vile jambo ambalo hakuwahi kulifanya siku za nyuma. Mustafa alijikuta akimshangaa Sara kwa kitendo kile, wakati huo Sara alishtuka kuona aliyekaa mbele yake si bosi bali nguruwe. Alituliza macho ili kupata uhakika.
Hakukuwa na mabadiliko zaidi ya kuona nguruwe amesimama kwenye kiti cha bosi wake akichezesha pua. Alikaza macho kuangalia kama alichokiona ni kweli au maruweruwe. Bado hali ilibakia ileile ya kumuona nguruwe mbele yake, alipekecha macho ili kuikataa hali ile kwa kuamini yale yalikuwa maruweruwe kama yaliyomtokea jana yake.
Itaendelea LIKE PAGE USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HIIII
0 comments:
Post a Comment