MIMBA YA JINI -29

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-29-

#LIKE PAGE MWENDELEZO WA HADITHI HII USIKUPITE ONYESHA UPENDO KWA #KUSHARE HADITHI HII KWA #MAFRIEND #GROUP UNIPE MOTISHA YA KUPOST KIPANDE KINACHOENDELEA

ILIPOISHIA:
"Zile sauti za kutisha zilizidi kunisogelea nikaona kama nitazubaa basi nitakufa. Nilijilazimisha kukimbia huku nimeshika mkono kwenye mbavu. Nilikwenda hivyo kwa kuchechemea mpaka nilipotokea kwenye mti mkubwa.
SASA ENDELEA...

"Kwa vile nilikuwa nimechoka sana, nilijiegemeza kwenye mti mkubwa pembeni ya barabara, pamoja na alfajiri ile kuwa na baridi kali lakini usingizi ulinichukua.
"Mpaka nilipoamshwa na wanakijiji, sikuamini waliponiambia pale ni Kongwa Dodoma na muda ule ni saa nane mchana, kingine kilichonishangaza kuelezwa siku ile ni Jumapili wakati niliondoka nyumbani Jumatatu.
"Yani bado siamini kutembea kwa mguu kwa wiki nzima, kibaya zaidi nakumbuka nilitembea usiku mmoja lakini imeonekana nilitembea wiki nzima. Kama nilitembea wiki nzima, mbona sikuuona mchana zaidi ya usiku tu?" Sara alihoji huku machozi ya uchungu yakimtoka.
"Dada hiki ni kituko yani lazima uende kanisani ukaombewe, lazima watakuwa ni wachawi tu walikuchukua."
"Na..na..kwe...," Sara alisita kuzungumza baada ya kumuona nguruwe amekaa kwenye kiti alichokaa Happy, alipiga kelele za uoga.
"Mamaa nakufa nguruwe."
"Sara nguruwe yupo wapi?" Happy alimshangaa rafiki yake.
"Si..si...," alituliza macho na kushangaa kumuona aliyekaa mbele yake ni Happy na si nguruwe kama alivyoona..
"Sara upo sawa?" Happy aliamini rafiki yake hayupo sawa.
"Ni..ni..hapana..hapana," Sara alituliza macho yake baada ya kumuona tena nguruwe kwenye kochi hakupiga kelele, alitulia na kufikicha macho ili kupata uhakika kama kweli kilichopo mbele yake ni nguruwe au anaona maruweruwe. Baada ya macho kutulia alimuona tena shoga yake Happy wala si nguruwe.
"Happy naomba nipumzike, siko vizuri sijielewi kabisa."
"Sawa dada lakini kwanza nenda ukaoge ili kuufanya mwili upumue."
"Sawa," Sara alisema huku akivua nguo alizokuja nazo na kuchukua taulo ili aende bafuni.
Alichukua sabuni na mswaki kisha alitoka nje na kumuacha shoga yake akimfanya usafi wa chumba. Sara alielekea nje alipofika mlangoni alisita kutoka baada ya kuona nguruwe wamejaa uani. Alizidi kushangaa na kumwita Happy kwa sauti.
"Happy njoo."
Happy aliacha kufanya usafi na kusogea mlangoni.
‘Vipi?"
"Eti nje unaona nini?"
"Kawaida, kwani umeona nini?"
"Nguruwe."
"Nguruwe?" Happy alishtuka.
"Hebu ngoja," Sara alisema huku akipekecha macho na kuona wapo wapangaji wenzake na si nguruwe.
"Mmh! Mbona mwaka huu wangu."
"Shoga kuna umuhimu twende kanisani ukaombewe."
"Ngoja nikaoge."
Sara alikwenda hadi bafuni na kuoga kisha alirudi ndani bila hali ile kumtokea tena. Kwa vile alikuwa amechoka sana, alipanda kitandani na usingizi mzito ulimchukua.
****
Siku ya pili Sara alidamka mapema na kuoga kisha alitoka kwenda kazini kwa kumuaga shoga yake Happy. Happy alimuuliza alivyolala.
"Vipi umelala salama?"
"Namshukuru Mungu nimelala salama, wacha niwahi kazini japo sijui bosi wangu kama atanielewa."
"Atakuelewa tu kwani kilichotokea si cha kawaida."
"Mmh! Ngoja niwahi."
"Mi nilikuwa na wazo."
"Wazo gani?"
"Nilikuwa na wazo la kwenda kwanza kanisani ukaombewe pepo mchafu."
"Wazo zuri lakini lazima nifike kwanza ofisini nijue hatima yangu ndipo twende huko kanisani."
"Basi ukirudi jioni tutapanga."
"Sawa."
Sara aliagana na shoga yake na kuwahi kazini kama kawaida kwa kuwahi ili afanye usafi kabla bosi wake hajafika.

Je, nini kitatokea? #SHARE STORY NIPOST NYINGNE TUJUE NINI   kitaendelea.... #SHARE ZIWE MINGI.

0 comments:

Post a Comment