MIMBA YA JINI -17

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-17-

Mtunzi: #Mzizi_Mkavu

SASA SKIA ILI USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HIII #LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA #SHARE ZIKIFIKA 250 NAPOST MWENDELEZO WAKE SHARE KWA MRAFIKI NIPO NYINGNE NOW.

ILIPOISHIA:
"Mbona wako niliuweza wa kwenda kubadili matokeo ya usaili ili upite kama ningekamatwa ningekuwa wapi?" Shehna alimuuliza Mustafa akiwa amemkazia macho huku sura ya uzuri iligeuka kama mzee na kumtisha Mustafa.
SASA ENDELEA…

"Mustafa nimejitolea katika mambo yake mengi ambayo wewe huyajui, yaani kwa hili moja umeshindwa. Unakumbuka ulitaka kufukuzwa kazi mimi ndiye niliyerekebisha mahesabu ili ubakie kazini?
Wewe ni mtu gani usiyejiuliza kila kosa lako halionekani?" Shehna alimuuliza huku machozi yakimtoka.
Kauli ile ilimshtua sana Mustafa na kuzidi kumshangaa Shehna na kujiuliza ni kiumbe wa aina gani. Alikumbuka baada ya kupata nyumba ndogo alijikuta akitaka kumfurahisha, alijikuta akifanya ubadhilifu wa fedha kazini kwake.
Taarifa ilifika ofisi kuu na kufanya mahesabu ya ghafla huku akisimamishwa kazi kupisha wafanye mahesabu.
Kitendo kile kilimshtua Mustafa na kujikuta akipandwa na presha na kulazwa hospitali kwa kujua hana kazi na lazima afungwe kwa vile alichota zaidi ya milioni kumi na tano.
Siku ile akiwa hospitali majira ya usiku wa manane aliamshwa na daktari binti mrembo wa Kiarabu aliyekuwa amesimama pembeni ya kitanda chake.
Alikuwa amevalia mavazi ya kidaktari na miwani myeupe nywele zake zilikuwa ndefu na nyeusi. Alikuwa binti mrembo sana, hakuwahi kumuona mwanamke mzuri kama yule katika maisha yake na kumwita jina lake.
"Mustafa."
"Naam."
"Pole sana."
"Asante."
"Tatizo nini?"
"Wanadamu wabaya wamenisingizia nimekula fedha ya kampuni wakati sijala hata senti tano."
"Mustafa kuwa mkweli, fedha umekula. Heri ungeijengea familia yako, wazazi wako wanaishi maisha ya kubahatisha kuliko ulichokifanya kumhonga hawara."
Kauli ile ilimshtua Mustafa na kujiuliza yule daktari amejuaje au kuna mtu alimwambia, ilibidi amuulize amejuaje.
"We umejuaje?"
"Mustafa muhimu si kujua nimejuaje zaidi ya kukusaidia usifukuzwe kazi na kufungwa."
"Utafanyaje?"
"Kazi hiyo niachie mimi," Mustafa alizidi kumshangaa daktari atamsaidia vipi, daktari alitabasamu na kuzitikisa nywele zake ndefu nyeusi zilizoongeza uzuri wake.
"Mustafa bai."
Mustafa siku ya pili aliposhtuka alijua ile ilikuwa ni ndoto kwa vile pale hospitali hakukuwa na daktari wa vile. Lakini ajabu siku iliyofuata alielezwa arudi kazini kila kitu kimekutwa kipo sawa hakukuwa na hasara yoyote kwenye fedha ya kampuni. Japokuwa aliona kama ndoto iliyo na ukweli, hakutaka kushughulika nayo zaidi ya kushukuru kuponea tundu la sindano.
"Mustafa unakumbuka siku hiyo?"
Mustafa baada ya kuvuta kumbukumbu alijikuta akizidi kumshangaa Shehna na kujiuliza ni kiumbe gani aliyekuwa karibu ya matatizo yake muda wote na kujiuliza amekuwa akijuaje na kutokea kumsaidia. Alijiuliza alifanyaje mpaka hesabu zikakutwa zipo sawa wakati alijua tayari hana kazi na jela ilikuwa ikimwita.
Shehna baada ya kumuona Mustafa amehama kimawazo, alimuuliza tena swali lake la awali.
"Mustafa unakumbuka? Au umesahau maana akili yako ina ubongo wa samaki."
"Nakumbuka."
"Uliiba hela hukuiba?"
"Niliiba."
"Unajua kwa nini ulibakia kazini?"
"Sijui."
"Hukujiuliza uliporudishwa kazini wakati ukijua umefanya makosa?"
"Kwa kweli nilipitiwa kwa hilo."
"Mustafa wewe ni mwanadamu gani usiyejiuliza unakwenda kama mnyama?"
"Hata sijui nikuambie nini ili unielewe."
"Inaoneka hata ukipewa kitu hujui kusema asante."
"Shehna ukisema hivyo utanionea, kwa vile mazingira yake yalikuwa kama muujiza au kitu cha ndotoni. Hata wewe baada ya kunifanyia ulitakiwa kujitokeza na kunieleza ili nijue kwa kumshukuru."
"Basi elewa yote hayo niliyafanya kwa ajili yako, kama nilivyokueleza nilipata safari ya ghafla, pia nilitaka kujitokeza muda muafaka kama huu."
"Ulifanyaje?"
"Leo siyo siku yake muhimu ni hili langu, kwa nini hili langu dogo hutaki kunisaidia hujiulizi kuna wanaume wangapi lakini nimekupenda wewe?" Shehna alimuuliza huku machozi yakimtoka na kuyafanya macho yake kuwa mekundu na kuongeza uzuri wake kama njiwa manga.
"Basi nitajitahidi kufanya unavyotaka japokuwa unanipa mtihani mzito."
"Si mtihani kama unavyoona, hebu jaribu leo utaniambia fanya yote niliyokuelekeza kama mkeo atajua basi mimi navunja mapenzi na wewe."
"Shehna sitaki kukupoteza," Mustafa alichangwanywa na uzuri wa Shehna.
"Basi fanya hivyo."
"Nitafanya kwa ajili nakupenda."
Shehna alifurahi na kwenda kumkumbatia Mustafa na kumpiga mabusu.

Itaendelea. SASA SKIA ILI USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HIII #LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA #SHARE ZIKIFIKA 250 NAPOST MWENDELEZO WAKE SHARE KWA MRAFIKI NIPO NYINGNE NOW

0 comments:

Post a Comment