MIMBA YA JINI -18

Author

Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-18-

Mtunzi: #Mzizi_Mkavu

SASA SKIA ILI USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HIII #LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA #SHARE ZIKIFIKA 250 NAPOST MWENDELEZO WAKE SHARE KWA MRAFIKI NIPO NYINGNE NOW

ILIPOISHIA:

Niliyokuelekeza kama mkeo atajua basi mimi navunja mapenzi na wewe."

"Shehna sitaki kukupoteza," Mustafa alichanganywa na uzuri wa Shehna.

"Basi fanya hivyo."

"Nitafanya kwa ajili nakupenda."

Shehna alifurahi na kwenda kumkumbatia Mustafa na kumpiga mabusu.

SASA ENDELEA…

"Katika siku uliyonifurahisha leo imezidi siku zote, Mustafa ukizaa na mimi nitakupa zawadi kubwa ambayo hukuwahi kuiota maishani mwako."
"Nitashukuru."
"Kingine ulichonifurahisha kutengeneza uongo kwa mkeo juu yangu, imenifanya nizidi kukupenda."
"Lazima nifanye hivyo wewe ni mtu muhimu sana kwangu."
"Basi acha nikuache uendelee na kazi tutaonana usiku."
"Hakuna tatizo."
Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akiendelea na kazi, baada ya muda Mustafa alitoka kufuata kitu kwenye gari. Alipofika mapokezi alishangaa kukuta rafiki yake kipenzi James akimsubiri.
"Ooh! James umefika zamani?"
"Kama nusu saa nimeambiwa una mgeni."
"Mbona ametoka muda mrefu."
"Bosi ametoka kapitia wapi?" Sara aliuliza.
"Jamani si hapa au ulipitiwa na usingizi?"
"Hatujamuona mtu, mgeni mwenyewe labda jini?"
Sara alisema jina ambalo siku zote lilikaa mdomoni kwake na kumchefua sana Shehna na kupanga kumkomesha na tabia yake ya kumwita jini. Alipanga usiku kabla ya kwenda kwa Mustafa aanzie kwa Sara ili kumkomesha aachane na kufuatilia mambo yake.
"Sara sitaki tena kusikia ukitamka jina hilo, siku hizi umenizoea sana eti eeh? Unasema lolote mdomoni mwako," Mustafa alimfokea Sara ilikuwa ni mara ya kwanza kukasirika toka aanze naye kazi miaka saba iliyopita.
"Samahani sana bosi," Sara alishtuka huku woga ukimtawala.
"Katika siku uliyoniudhi leo umeniudhi sana, una bahati nina mgeni ningekufukuza kazi sasa hivi," Mustafa alisema kwa hasira mpaka povu likamtoka mdomoni.
"Bosi nisamehe, nilisema kwa utani sikujua kama nitakuudhi kiasi hiki," Sara alijitetea.
"Nitamalizana na wewe baadaye ngoja nizungumze kwanza na mgeni wangu."
"Kwani tatizo nini mpaka ukwazike hivyo?" James aliuliza.
"James, tuzungumze yetu huyu nitamalizana naye."
James ilibidi anyamaze kwa vile hakujua chanzo cha Mustafa kukasirika vile kilitokana na nini, siku zote alimjua ni mkimya na mpole. Waliingia ofisini huku Mustafa akiwa bado ana hasira, kabla ya kuzungumza aliinama kwa muda kuonesha Sara amemuudhi sana.
"Kwani best kipi kimekukwaza hivyo?"
"U...u...u na..," Musfata alinyamaza baada ya simu yake kuita, alipoangalia aliiona inatoka kwa Shehna aliipokea.
"Haloo."
"Mustafa."
"Naam."
"Mbona kama haupo sawa?"
"Kwa nini?"
"Sauti yako inajieleza."
"Si huyu mshenzi leo atanitambua namfukuza kazi."
"Kwa nini?"
"Sikufurahia alivyokuita."
"Ananiitaje?" Shehna alijifanya hajui kitu.
"Eti anakufananisha na jini."
"Hapana mpenzi usimfukuze kazi."
"Kwa nini?"
"Ameropoka kwa bahati mbaya, sitaki mimi kuwa na wewe tuongeze maadui."
"Kwa hiyo?"
"Mpe onyo tu, hawezi kurudia."
"Ana bahati bila wewe ningemfukuza kazi sasa hivi."
"Msamehe kuanzia sasa fungua moyo wako zungumza na mgeni kwa uchangamfu."
"Sawa nitafanya hivyo."
"Naomba ucheke kidogo basi," Shehna alisema kwa sauti tamu iliyofanya Mustafa acheke.
"Haya mpenzi wangu kazi njema."
"Asante nawe siku njema."
Wakati huo Sara alikuwa kwenye hali mbaya kwa kujua siku ile ndiyo ya kufukuzwa, kazi ilimshinda, mapigo ya moyo yalimwenda mbio. Alijiinamia kwenye meza huku mkono mmoja ukiwa kifuani kuzuia mapigo ya moyo yaliyokuwa yakienda kwa kasi. Mustafa baada ya kuzungumza na mgeni wake alitoka kumsindikiza, alishangaa kumkuta Sara akiwa amejiinamia huku akilia kilio cha kwikwi.
"Sara una nini?"
"Sina kitu, nitafanya nini nawe hutaki kunisamehe?"
"Yale yameisha ila siku nyingine kuwa makini na kauli zako kwa wageni wangu hasa Shehna."
"A...a...sante bosi sirudii tena," Sara alitaka kumshika miguu, lakini Mustafa alimuwahi kumshika na kumnyanyua juu.

Itaendelea SASA SKIA ILI USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HIII #LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA #SHARE ZIKIFIKA 250 NAPOST MWENDELEZO WAKE SHARE KWA MRAFIKI NIPO NYINGNE NOW

0 comments:

Post a Comment