Hadithi ya kusisimua #Mimba_ya_Jini-16-
Mtunzi: #Mzizi_Mkavu
SASA SKIA ILI USIPITWE NA MWENDELEZO WA HADITHI HIII #LIKE PAGE USIPITWE NA KIPANDE HATA KIMOJA #SHARE ZIKIFIKA 250 NAPOST MWENDELEZO WAKE SHARE KWA MRAFIKI NIPO NYINGNE NOW
ILIPOISHIA JANA:"Namba yako nitawapa."
"Namba yangu umeipata wapi?"
"Mustafa hujawahi kuigawa namba yako?"
"Nimegawa basi nitashukuru japokuwa najua hakuna kitu."
"Siku tukikutana ataniambia."
SASA ENDELEA…
Mustafa aliagana na yule msichana mwenye lafudhi ya mwambao bila kumuuliza jina. Siku moja akiwa hana hili wala lile alipigiwa simu kujulishwa amefanikiwa kupita katika mchujo wa usaili na yeye ndiye aliyefanya vizuri kuliko wote anatakiwa kubakia Dar es Salaam.
Alishtuka sana lakini hakuamini aliona kama watu wanamchezea akili, siku ya pili alikwenda ofisini kujaribu lakini alipotaja jina lake alikabirishwa na kujaza fomu ya kuajiliwa na wiki iliyofuata alianza kazi kwa kupewa ofisi na sekretari pamoja na mshahara mzuri.
Lakini Mustafa alisahau kama kuna mtu alimweleza taarifa kuwa atapita kwenye usaili na atabakia jijini Dar japokuwa alikuwa amefanya vibaya sana.
Furaha ya kupata kazi ilimfanya asitumie muda kuwaza ilikuwaje mpaka kupita na msichana yule alijuaje. Mustafa alitulia na kuvuta kumbukumbu kisha aliteremsha macho kumuangalia Shehna na kuamini kabisa ndiye yeye. Kwa lafudhi aliyoitumia japokuwa alimuona macho tu aliamini kabisa ndiye msichana aliyemtabilia mambo ya ajabu.
"Dah! Kweli."
"Kweli nini?" Shehna alimuuliza akiwa anamtazama usoni.
"Nimekumbuka, hivi ulijuaje mi nitapita wakati nilikuwa najua nimefanya vibaya?"
"Leo siyo siku yakeikifika nitakueleza, mpaka hapo nina imani baadhi ya vitu umevielewa kama una swali niulize."
"Swali lingine nilitaka kujua wewe unakaa wapi katika familia yenu mpo wangapi, kwa sasa unajishughulisha na nini. Wewe ni mganga au nani?"
"Ninapokaa si rahisi kukuelekeza mpaka twende pamoja, katika familia yetu tupo watatu wote wanawake mimi ni mtoto wa mwisho na swali la mwisho mimi si mganga wala mnajimu ila Mungu kanipa uwezo wa kuyajua matatizo ya mwenzangu."
"Kwa nini huwezi kupata ujauzito kwa mara moja kama mke wangu?"
"Dawa ya haraka nilikuwa nayo moja ambayo nilimpa mkeo hii inachelewa, kwa vile nami nina hamu ya mtoto sina jinsi lazima nitumie njia ya muda mrefu."
"Kingine unajua sijawahi kulala nje ya nyumbani kwangu nitafanyaje?"
"Mustafa nyumba ndogo huwa unalala nayo nyumbani kwako?"
"Mmh!" Mustafa aliguna baada ya kujua ameumbuka.
"Najua wasiwasi wako kulala nje ya nyumba yako mwezi mzima, nitalala na wewe mwezi huo mzima nyumbani kwako na kitandani kwako."
"He! Na mke wangu atakuwa wapi?" Mustafa alioshtuka.
"Atakuwepo ndani."
"Siwezi kufanya mapenzi ndani na mke wangu akiwemo itakuwa kumdhalilisha."
"Mustafa naomba unisikilize, wewe kila siku naomba ukilala usiku wakati mnataka kulala hakikisha wewe unakuchelewa kulala usikubali hata siku moja mkeo akukute kitandani.
"Mkeo akiisha lala utaingia bafuni kuoga na kujipaka mafuta nitakayokupa.
Isipande kitandani hakikisha mlango wako umeurudisha bila kuufunga au dirisha ili nikija nisipate tabu ya kuingia.
"Ukiishapanda kitandani usilale na nguo ya ndani kisha hakikisha mkeo analala ukutani wewe lala katikati ya kitanda mimi nikija nitalala mwanzoni mwa kitanda. Mpake mkeo mafuta kichwani kisha lala."
"Mmh! Nitaweza kweli, mbona unanipa mtihani, kwa nini tusiwe tunakutana hotel na tukimaliza haja zetu, narudi nyumbani kulala?"
"Mustafa kutafuta kwangu mtoto natakiwa kupata dozi ya mara tatu kwa usiku mmoja hivyo lazima nilale na wewe."
"Una maanisha dozi ya kivipi."
"Ya saa sita, saa tisa na kumi na moja alfajiri, unaweza kulala nje?"
"Shehna mbona unanipa mtihani mgumu."
"Mbona wako niliuweza wa kwenda kubadili matokeo ya usaili ili upite kama ningekamatwa ningekuwa wapi?" Shehna alimuuliza Mustafa akiwa amemkazia macho huku sura ya uzuri iligeuka kama mzee na kumtisha Mustafa.
Itaendelea #SHARE KWA MARAFIKI NIPOST MWENDELEZO WAKE NOW NASUBIRIA SHARE 250 NIPOST KIPANDE KINACHOENDELEA
JAMAN WENGI SANA WANALALAMIKA ILA TATIZO HAMUONYESHI SAPORT NDIO MAANA NAPOST KIPANDE KIMOJA KIMOJA NAONA VIEWZ 50000 LAKIN #LIKE NA #SHARE HAZIFIKI HATA 500 SAPORT YENU HAPO IPO WAPI WATU WANASOMA TU WANAONA HATA UVIVU KULIKE ALAFU MNA LALAMIKA JAMAN MSIWE HIVYOOO NYIE MNAONILALAMIKIA #INBOX
0 comments:
Post a Comment