Author
Marafiki Club-43
By Sparner Boy 0765148781

Ilipoishia...



"huyu lazima afe"
Alijisemea Husna akachukua simu yake na kubonyeza namba fulani kisha akapiga..

Endelea..

Upande wa pili simu iliita mara kadhaa kisha ikapokelewa.

"Hallo engineer upo wapi?"
"Nipo mjini kuna baadhi ya vitu nimekuja kuchukua lakini sio muhimu sana Boss vipi kuna tatizo?"
"nilitaka unipeleke Arusha mara moja nitakulipa muda wako tafadhali pia njoo na copy zote ulizonazo za ramani ya jengo lile nna kazi nazo"

"aah ok boss ngoja nizifuate nyumbani mara moja"
"ok nashukuru njoo utanikuta apa njia panda kama unaenda Club"

Husna alikata simu kisha akacheka kidogo na baada ya nusu saa yule engineer aliyepewa kazi ya kujenga Marafiki Club alifika.Husna kabla hajapanda kwenye gari aliangalia pande zote baada ya kuhakikisha hakuna mtu aliyemwona akapanda na kumwambia engineer waondoke.
Safari ya kwenda Arusha ilianza lakini Husna siku hiyo alikuwa kimya akikagua tu zile ramani.Walipofika mahali ambapo hakuna nyumba wala maduka,Husna alimwangalia yule Engineer na kumuuliza

"engineer wewe unaonekana una akili sana mi nimekukubali na kazi zangu nitakuwa nakupa"
"asante sana Boss ndio kazi zetu hizi"
"pia unaonekana una kichwa kizuri inayoshika vitu haraka sana,nikuulize kitu?"

"haha..bosi bana,asante.we niulize tu chochote usijali"
"mfano sasa hivi nikakuambia unijengee Club kama ile ile alafu nisikupe ramani utaweza?"
"ndio naweza,mimi hiyo ramani ipo kichwani naweza kuichora kama ilivyo bila kuiangalia"

"haha..safi sana naomba simamisha gari nimebanwa na mkojo au gari lako lina choo?"

"hahahaha.. Boss Hamna gari yenye choo labda meli na maboti makubwa"
aliongea hayo Yule engineer ambapo wote walicheka kisha akapaki gari pembeni.Baada ya kupaki Husna hakushuka alimwangalia kwa hasira kisha akamwambia
"lazima ufe engineer"
"kwa kosa lipi kama ni gari unataka chukua"
""Hapana,ile ramani kama unaijua kichwani ina maana akitokea tajiri mkubwa akuambie umjengee club kama ile unaweza si ndio?"
"bos unaongea ushenzi gani mimi siwezi kufanya hivyo pia ile haiwezekani kuijenga bila ramani"

"kwa hiyo mimi naongea ushenzi,si umesema unaweza kuchora ramani bila kuangalia"
""bos bana acha kunitisha,kwa hiyo unatakaje we ni mchumba tu ata kama una pesa na mimi ninazo pia"

Alijibu yule engineer kwa jeuri,
Husna alicheka kisha akamkaba shingo kwa nguvu yule engineer,jamaa alijitahidi sana kujinasua kwenye mikono ya Husna lakini alishindwa na alishangaa mtoto yule wa kike ametoa wapi nguvu kama zile.Alirusha miguu, mikono na baada ya sekunde kadhaa alitoa ulimi nje na kuaga dunia.

Husna alipomaliza kazi alimrudisha upande aliokuwa amekaa kisha akashika usukani na kurudi wakipotoka ambapo hatua chache alifika kwenye daraja ambapo walilipita mda mfupi uliopita.Alishuka kwenye gari akasubiri magari yapite na alipohakikisha hakuna gari linalokuja alisukumia kile gari mtoni ambapo lilisagika sagika na kuaribika vibaya hivyo taarifa zikatangazwa kuwa engineer amekufa kwa ajali baada ya gari kukataa njia na kutumbukia mtoni.

Siku zilienda na Club ilizidi kupata umaarufu siku mpaka siku,kwa siku naomy alikuwa anakwenda benk mara tatu kupeleka pesa yani biashara ilikuwa ni nzuri haswa.

Siku moja Husna alimwita akampa maelezo kuwa anasafiri anakwenda urusi na atakaa sana uko hivyo majukumu yote anamwachia yeye.Alimwambia pesa awe anaweka kwenye acount ya kawaida na ikifika mwisho wa mwezi pesa ya mauzo awalipe wafanyakazi pia akampa ovyo kuwa asijaribu kuuza pombe kwenye ile Club.

Alimpa maelezo mengi kuagiza vingwaji vya jumla na email za wafanyabiashara wakubwa wa vinywaji ambapo atakuwa anafanya nao biashara.

Naomy baada ya kuelewa kila kitu na Husna kuhakikisha kila kitu kitaenda sawa,Wiki mbili baadae Husna aliondoka na kurudi kwao.

* * *
Alipofika getini alisita kidogo kwani alikaa sana duniani zaidi ya mda aliotakiwa kurudi nyumbani alipitiliza akaongeza miezi sita na hii ni kutokana na kwamba hakuwa amempata mtu wa kumwachia ile Club pia haikuwa imekamilika hivyo ikamlazimu akae mpaka ahakikishe imesimama na kila kitu kinaendelea vizuri kwani baba yake alishamwambia kuwa akija hatarudi tena duniani ata iweje na nguvu atamnyang'anya.

Alisukuma lango kuu akaingia.Alipoingia alishangaa watu wote wanampigia magoti ata wale waliokuwa na cheo kikubwa kuliko yeye.Akishangaa kwa sababu siku zote akija huwa wanam'beza pamoja na kumtemea mate kuwa anatembea na binadamu na mara ya mwisho walimpiga sana.Aliangalia wale watu vizuri ambapo aliwaona mpaka ndugu zake wamepiga magoti.Alifika mahali ambapo baba yake huwa anaketi akamkuta lakini baba alipomwona akainuka na kumpisha yeye akae.Husna alikataa akisema kuwa kile ni kiti cha baba wala yeye hastahili kukaa pale ni kukosa adabu.
Basi haraka kiti kililetwa kingine Husna akakaa.
Baba yake alimpa mkono na kumwambia..

""mwanangu sikukutuma ufanye ile kazi lakini nimeipenda nakupa hongera sana""
"asante baba pia nisamehe kwa kuchelewa kuj..""
"hapana najua ulikuwa kazini,kuteketeza lile kanisa na kufungua club hapo ni dharau moja ambayo haijawahi kutokea duniani"

"baba asante""

"kwanzia leo wewe utakuwa kiongozi wa watu wote humu ndani,nitakupa nguvu nyingi lakini nguvu moja tu sintakupa ya kurudi duniani."

Husna aliumia sana aliposikia kuwa hatarudi duniani,pale pale aliongezwa nguvu nyingi hivyo akawa malkia wa majini wote.Baba Husna aligundua kuwa Husna hakuwa na furaha kama alivyotegemea.Baada ya kumjaza nguvu za kichawi alimuuliza tatizo ni nini mbona hana raha.Husna akisema kwa kuwa amekuwa malkia wa watu majini wote anataka baada ya miaka kumi arudi duniani au kama haiwezekani atume mtu.Baba alimwangalia akamwambia..

""utamtuma mtu wewe ni malkia na nguvu za kurudi duniani wewe sintakupa"
"sawa baba lakini kuna watoto wawili duniani mmoja anaitwa Rehema na mwingine anaitwa Nancy"

"wamefanyaje hao watoto"
"baada ya miaka kumi kuna kazi nataka watufanyie,wale watoto mimi nimechangia kwa kiasi kikubwa mpaka wakapatikana na wote baba yao ni mmoja anaitwa Roy hivyo wale ni kama watoto wangu mimi""

"sasa chagua mtu yoyote humu ndani utakaemtuma wewe hutakwenda duniani kamwe""

Husna baada ya kuangaza macho uku na uku aliita jina la Aisha ambapo aliinuka binti mmoja mzuri balaa yani anavutia kuliko ata Husna.Aisha pia alikuwa anasifika kuwa ana akili sana kwenye kufanya mambo yake, alikuwa aende yeye duniani badala ya Husna lakini kura nyingi zikamwangukia Husna lakini Aisha pia yupo vizuri na huwa hakosei ata siku moja.

Husna alimwambia ajiandae baada ya miaka kumi atatumwa duniani na maelezo yote atapewa mda ukifika.Aisha aliitikia na kuketi kisha ikafanyika sherehe kubwa ya kumpongeza Husna kwa kuwa malkia wakati huo wanasubiri miaka kumi ambapo Aisha atakuja duniani kuwatafuta Nancy yani mtoto wa Roy na Ester pamoja na Rehema yani yule mtoto wa Roy na mama mchungaji na mpaka wakati ule hakuna aliyejua kuwa ni kazi gani watoto wale wanatakiwa kuifanya.Sherehe ilinoga watu walicheza,kula na kunywa huku wanaimba nyimbo za kumsifia Husna.

MWISHO
Part 2 ikiwa tayar nita kujuzaaa.

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment