Marafiki Club-42
By Sparner Boy 0765148781
Ilipoishia..
Alishika shingo ya Roy Tayari kumnyonga lakini kabla hajafanya hivyo akamwambia
"sipendi kufanya hivi lakini nafanya kwa usalama wa Club yangu"
Endelea..
Roy aliposikia maneno yale kutoka kwa Husna alisema
"Husna mpenzi niamini kwanza sintaishi apa tanzania narudi kwetu kenya kwa hiyo mambo ya uku hayatanihusu nitaanza maisha yangu upya naomba usiniue""
Roy alizungumza haraka haraka kama mashine huku anatetemeka na jasho likimtoa cha ajabu pale ni mgahawani lakini hakuna aliekuwa anaangaika nao kila mtu alikuwa bize na mambo yake.Husna alimsikiliza kwa makini kisha akamwachia na kumuuliza
"una uhakika unaondoka apa Tanzania""
""ndio ata kesho ukitaka nitaondoka"
"sio nikitaka wewe nakupa masaa 48 usionekane Tanzania,Roy unajua nimefanya mambo mengi na wewe ndio maana nakuacha sasa ole wako nisikie umefungua mdomo ingawa sintakuwa duniani lakini nitafanya chochote nikukomeshe"
""asante Husna""
Pia gari nakupa lakini iache ka ilivyo wewe chukua kinachobebeka uondoke hilo gari ni la kwako nimekupa"
Husna alizungumza kwa sauti ya upole kisha akaachia msonyo wa nguvu na kuondoka kwa maringo uku makalio yake makubwa ya wastani na malaini yakitingishika.Ni kawaida Husna huwa akikasirika anaongea taratibu alafu kwa upole na anakuuwa bila wewe kutarajia.
Roy aliondoka pale haraka akiwa haamini kuwa amepona,alirudi nyumbani akamwambia Ester kuwa mama anamuita nyumbani hivyo ajiandae kesho yake waondoke.Alimdanganya kwa sababu alimjua vizuri Husna kuwa hana utani na alishamuonya asimwambie mtu yoyote kitu chochote kuhusiana na ile Club hivyo aliogopa akimwambia Ester kuwa amekutana na Husna maswali yangekuwa mengi na asingeweza kuyajibu.Ester alipojaribu kuhoji kuhusu safari ile ya ghafla Roy alikuja juu na kudai hataki maswali kinachotakiwa kesho yake wanaondoka.
Ester alianza kuandaa vitu vya muhimu wakati huo Roy akachukua gari na kupeleka gereji kwa ajili ya kuifanyia Service kwa maandalizi ya safari yao.Mambo yalienda vizuri na kesho yake majira ya saa tano asubuhi walikuwa safarini kuelekea Kenya.Roy aliwaza apitie kwa shangazi yake ni miaka mingi hajamuona lakini akasita akihofia kuwa atamuuliza maswali mengi kuwa alikuwa wapi siku zote,alikuwa anakula nini na maswali ambayo asingeweza kuyajibu hivyo akapitiliza kuelekea nyumbani.Safari ilikuwa nzuri ambapo saa 9alasiri walifika nyumbani.Mama Roy alifurahi sana kumuona mwanae,Alimkumbatia huku machozi ya furaha yakimtoka kwani walijua amekufa kwenye lile basi lililoteketea kwa moto baada ya kupata fununu Roy alikuwa ndani ya basi hilo.Pia alimkaribisha mwali wake yaani Ester kwa mikono miwili pamoja na mjukuu wake yani yule mtoto wa Roy waliempa jina la Nancy na jumapili iliyofuata ikafanyika sherehe kubwa ya kumkaribisha Roy, Ester na Nancy nyumbani ambapo baada ya Hapo Roy na Ester wakaanza kuishi rasmi kama mume na mke huku maisha yakiwa ni mazuri kiasi kwa sababu familia ya akina Roy hawakuwa maskini wala matajiri sana yani ni familia nzuri tu ambayo wanaweza kula kila kitu wanachotaka na kufurahia maisha wanavyotaka pia walimpenda sana mtoto wao Nancy.
* * *
Ilikuwa jumamosi moja ambapo
Club inayokwenda kwa jina la Marafiki Club ilizinduliwa Rasmi na mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ambapo alikuwa ndio mgeni rasmi na aliambatana na viongozi mbali mbali wa mkoa.Siku hiyo sasa ndio kila mtu alimfahamu Husna kuwa ndio mwenye club huku viongozi mbali mbali wa mkoa wakimpongeza kwa kazi aliyoifanya.Watu walikula bure,walikunywa vinywaji mbalimbali lakini pombe haikuwepo. Baada ya hapo Club ilianza kazi rasmi ambapo ilikuwa inaingiza pesa nyingi,watu kutoka sehemu mbali mbali na mikoa ya jirani kama Arusha ,Tanga na Mombasa walikuwa wanaenda kila wikiendi kwani club ni pombe tu ndio haiuzi lakini dhambi zingine zote chafu zilikuwa zinafanyika kama kawaida tena kwa hali ya juu.Wanafunzi wa vyuo mbalimbali hawakuwa nyuma walikuwa wanakwenda kwa ajili ya kuopoa matajiri hivyo kufanya Club kuwa Tishio kwa ukanda mzima wa kaskazini mwa Tanzania.
Husna baada ya kuwaza sana aliona Naomy anafaa kuwa mmiliki wa Club ile,kwanza amesoma sana na ana degree ya biashara lakini yupo nyumbani hana kazi yoyote.Alianza kumuwinda ambapo baada ya wiki mbili alimpata akamwajiri pale club akampa cheo cha manager.Naomy alifanya kazi vizuri sana mpaka Husna akamkubali na akawaza kuwa anafaa kuachiwa Club.Akiwa anawaza hayo kuna wazo lilimjia akakunja sura kwa hasira kisha akasema,
"huyu lazima afe alafu nilitaka nimsahau"
Alijisemea Husna kisha akachukua simu yake akabonyeza namba fulani na kupiga.....
Itaendelea

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment