Marafiki Club-41
By Sparner Boy 0765148781
Ilipoishia...
Kitendo kile kilimkera Roy akachungulia nje na kuita Huuusnaa..
Endelea..
Husna na yule baba waliangalia lile gari na kumuona Roy,Husna alimpungia akamwonyesha ishara kuwa atampigia simu.Roy alishangaa sana kumuona Husna Duniani.walifika kwenye kile kituo ambapo alitakiwa asaini kuwa yeye ndio alimkabidhisha yule mtoto pale kituoni akiwa kama msamaria mwema.Roy alikataa lakini aliogopa kusema yule mtoto ni wa kwake kwani angeshtakiwa kwa kumtelekeza mama mchungaji pia kutokana na maelezo yake ya mwanzo alisema hamjui mama yule alimkuta njiani.Aliwaangalia wale maafisa akawaambia
"naombeni huyu mtoto nimlee mimi nitaweza jamani"
"hapana,tutakuwa tumemnyima huyu mama haki yake pia mtoto anatakiwa kunyonya,huyu mama tutamtunza na mtoto atakuwa ananyonya maziwa ya mama yake""
Roy alikosa la kusema akasaini kwa hasira lakini kabla hajaondoka aliomba akamuone mama mchungaji.Alipelekwa ambapo alikuwa amechanganywa na matahaira.Wengine walikuwa wanamchezea lakini mama yule alikuwa kimya tu ameangalia upande mmoja na ukimuita au kumgusa hakuwa anashtuka kuwa ameguswa wala kugeuza macho.
Roy huku machozi yanamtoka alisema..
""nisamehe mama mchungaji sio mimi,nisamehe mama yangu na Mungu atanisamehe pia""
Aliongea Roy na kuondoka.
Ile ametoka nje simu yake iliita namba mpya na alipopokea Husna akijitambulisha kuwa ni yeye ndio anapiga na anataka waonane.Alimsikiliza kwa makini akamjibu kwa hasira..
"sitaki kuonana na wewe Husna naomba niache na maisha yangu"
"acha hasira Roy usione nimekuacha umeoa mke mwingine ukadhani mimi ni mjinga na mbaya zaidi unatumia pesa zangu na gari langu..ata nyumba unayokaa ulinunua kwa pesa zangu""
"Nitaacha mali zako lakini bora niwe huru naomba niache"
"njoo nikupe maisha kijana umefanya kazi kubwa sana,nipo apa uliponikuta saa ile nakupa dakika 20"
Maneno ya Husna yalimchoma Roy,aliwaza akaona ni kweli Husna ndio anamuweka mjini hivyo hakuwa na ujanja alienda kuonana nae lakini akapanga atachukua kias kikubwa cha pesa kwenye acount ile kisha arudi kwao Kenya ila kwa wakati akaona aitikie wito wa Husna.
Husna alimpekeka mpaka kwenye ile Club iliyokuwa imeshawekwa kibao kikubwa kinachosomeka
MARAFIKI CLUB OPEN SOON
Roy alishtuka kanisa limekwenda wapi pia alishangaa sana kwa sababu ramani na mandhari walitengeneza kama ile Marafiki Club nyingine iliyopo chini ya bahari ambayo Husna akishawapeleka yeye na Mariam.
""Mungu wangu wewe Husna kanisa lipo wapi""
"apa nimepanunua mimi,na kujenga.pia yule mtu mnene mwenye kitambi ulieniona nae saa ile ndio engineer wangu"
"yeye amepataje hii raman au alishaenda uko""
"hapana mimi ndio nimempa ramani"
Roy alistahajabu wakaingia mpaka ndani,palikuwa pazuri sana na ilishakamilika kila kitu pale ilikuwa inafanyiwa usafi tu.
* * *
Walitoka pale wakaenda mahali palipotulia wakaagiza juice wakawa wanakunywa.Husna alimwangalia Roy akamwambia.
"kwa kazi uliyofanya ya kuteketeza lile kanisa umenifurahisha sana Roy sasa nataka nikupe zawadi""
"zawadi gani""
"mimi hivi karibuni naenda kwetu na sintarudi tena apa duniani kutokana na makosa yaliyotokea baba alisema ataninyang'anya nguvu za kurudi duniani"
""sasa zawadi gani unataka unipe""
"ile marafiki club nakuachia wewe kwa kazi nzuri uliyoifanya""
"hapana sitaki tena mambo ya majini mimi nataka kuwa huru"
"hapana mimi sintakuwepo na hatutaonana kwamwe mi naondoka sasa unategemea nitamuachia nani"
"hapana yani hotel ya gharama kama ile unipe ivi ivi mi sitaki"
Ilitokea mabishano sana mwisho Husna akakasirika na kumwambia Roy..
"Bora ungekubali tu,sasa kuanzia leo navunja mkataba na wewe na acount yangu ile unayochukuaga pesa haitakuhusu tena naifunga sasa ivi"
"hapana Husna naomba japo nikatoe pesa kidogo"
"We binadamu mjinga sijawahi kuona,mda wote nimekuachia acount yenye mamilioni ya pesa umeshindwa kuanzisha ata kamradi hahaha""
""nisamehe nimekubali kumiliki ile Club""
"Nani akupe si umeringa kaa mbali na mimi"
Husna aliongea kisha akaondoka akiwa anacheka,alipofika kwenye mlango wa kutoka nje alimwangalia Roy kisha akafungua pochi yake akatoa mabunda matatu ta milioni milioni akamrushia na kumwambia
""Hiyo itakusaidia siku mbili tatu na kwanzia leo hutaniona tena kwa heri" na hapo nimekufanyia msaada tu kwa sababu tumetoka mbali"
Aliongea Husna na kutoka nje.
Roy aliangalia zile pesa alizopewa akatikisa kichwa kwa huzuni kwani aliona umaskini sasa unabisha hodi kwenye maisha yake.Alikumbuka maneno ya Husna akimcheka kuwa mda wote amekabidhiwa acount yenye mamilion ya pesa hajafungua mradi wake.Aliwaza sana akajiona mjinga kuliko watu wote duniani.
Husna baada ya kutoka pale alikuwa anaumiza kichwa amwachie nani ile club,wakati anawaza afanye nini kuna wazo likamjia haraka akamrudia Roy.Roy akiwa anawaza pale kwenye ule mgahawa baada ya Husna kuondoka alishangaa kumwona Husna amerudi akiwa amekunja sura sana akionekana na Hasira. Alimfuata mpaka pale alipokuwa amekaa na kabla hajaongea jambo lolote Husna aliangalia uku na uku,baada ya kuhakikisha hakuna mtu akamshika Roy shati na kumwambia..
"kuna kitu nimewaza Roy,nisamehe lakini inabidi iwe hivyo kuwa wewe lazima ufe""
"Husna mimi nife yani leo unaniua"
"ndio,najua nikikuacha utatoa siri za ile club kwa sababu wewe tu ndio unajua kila kitu"
"hapana sintasema Husna usiniue""
""noo,wewe unajua kila kitu sasa nikimwachia mtu wewe utakuwa unatoa siri zangu am sory Roy Nakuuwa hapa hapa,nakuuwa Roy""
Aliongea hayo Husna kisha taratibu akapandisha mkono wake mpaka kwenye shingo ya Roy uku Machozi yakimtoka.Roy hakuwahi kuona machozi ya Husna lakini siku hiyo aliyaona.Alishika shingo ya Roy tayari kumnyonga lakini kabla hajafanya hivyo akamwambia
"am sory Roy sipendi lakini inanibidi kwa usalama wa Club yangu""
Itaendelea

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment