MARAFIKI CLUB-40

Author
Marafiki Ckub-40

By Sparner Boy 0765148781

Ilipoishia..

Naomy alicheka sana mpaka Manesi waliokuwa wanamhudumia wakashangaa..

Endelea..
Baada ya kila kitu kukamilika Naomy alirudi nyumbani lakini kwanza alipitia kwa Sheila.Alimuadithia Sheila kitu pia kwa furaha akiyokuwa nayo alimuadithia mambo yule mganga aliyomfanyia ingawa aliapa kutomwambia mtu yoyote.Sheila alimsikiliza kwa makini akamwambia..
"unataka kuniambia huyo Roy ni mchawi"
"mwenywewe nimeshangaa au ni janja ya yule mzee ya kutaka kunifaidi"
"hapana yule mzee mimi namjua huwa hakosei kwenye mambo yake"
Naomy alinyamaza kidogo kisha akachukua sim yake na kumpigia Roy..
"haloo baba watoto mambo"
"safi vipi Naomy unaendeleaje"
"nimejifungua mtoto wa kiume mpenzi njoo muone"
"kweli Naomy...nimefurahi sana garama zote nitamhudumia mimi wala usihofu"

"nyoo...pumbavu unapenda eeh..kitoto kimekufa mchawi mkubwa wewe,Roy wewe ni kijana mdogo sana kwa nini unakuwa mchawi?"
"Sikuelewi Naom.."
"Nyamazaa..sasa nitadili na wewe yani lazima ufahamu mimi ni nani,katoto kako kamekufa nimekaacha wakafukie hosptali bye"

Alikata simu wakacheka sana kwani mda wote wanaongea Naomy alikuwa ameweka loud spika.

Walipiga stori mbili tatu Naomy akaaga na kuondoka kuelekea nyumbani.

***
Mama mchungaji aliendelea kuishi maisha ya peke baada ya watu wote kumtenga.Hakuna ata muumini aliyetaka kufahamu habari zake wala kwenda kumsalimia.Mwezi mmoja tangu ajifungue afya yake ilikuwa imezorota sana na mda wote alikuwa mtu wa mawazo.Kadri siku zilivyokuwa zinaenda mama mchungaji akili yake ilizidi kuaribika na kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa,alikuwa anateseka sana mama yule.

Kwa upande wa Ester afya yake ilikuwa nzuri na ndoa yao sasa ikawa imeota mizizi yani walikuwa wanapendana sana.Hawakujua kinachoendelea kanisani pia waliamini Husna ameondoka kuelekea kuzimu na hatarudi tena hivyo maisha yao sasa yapo huru kabisa.Pamoja na furaha yote hiyo Roy kila akimkumbuka mama mchungaji Roho ilikuwa inamuuma sana.Alijua lazima atakuwa amejifungua na hakujua yupo kwenye hali gani kwa wakati ule au mtoto pia amefariki kama wa Naomy hakujua lakini aliomba isiwe hivyo.

Siku moja aliamua kufunga safari kwenda kwa mama mchungaji.Alifika akakuta mlango umerudishiwa ambapo alianza kugonga,aligonga sana lakini hakuna aliyekuja kufungua.Akiwa amekata tamaa akijiandaa kuondoka alisikia kwa mbali mtoto akilia,mtoto alikuwa analia lakini hakukuwa na sauti ya mtu anayem'bembeleza.Roy alishindwa kuvumilia akaingia ndani ambapo alimkuta mama mchungaji amempakata mtoto lakini hakuwa anaongea chochote na mtoto alikuwa anajaribu kunyonya maziwa ya mama yake lakini maziwa hayakuwa yanatoka pia mtoto alikuwa amelia mpaka sauti ikawa imeanza kukauka yani inatoka kwa shida.

Mama mchungaji hakuwa amefumba macho wala hakuwa usingizini alikuwa anaona vizuri,Cha kushangaza Roy alipomuita mama yule hakuzungumza zaidi ya kumwangalia tu.Roy machozi yalimtoka kwa jinsi mama mchungaji alivyokuwa amekonda yani huwezi kujua kama ndio yule mama mchungaji wa enzi zile.Aliangaza macho akaona kadi ya kuzaliwa ya mtoto yule na alipoisoma akatambua kuwa mtoto anaitwa Rehema.Aliita gari tayari kumpeleka mama mchungaji hospitali lakini kwanza akampeleka mtoto kwa Ester na kumwambia amnyonyeshe na kumwogesha kuhusu maelezo mengine atamwadithia akirudi. Kwa kuwa watoto wote ni wa kike haikuwa na madhara Ester alifanya kama Roy alivyomwambia.

Alimpeleka katika hosptali ya Mawenzi ambapo baada ya Vipimo mama mchungaji alionekana kuwa mawazo yamemuathiri kisaikolojia pia na kukaa mwenyewe kwa muda mrefu hivyo kwa sasa akili yake haipo sawa hivyo ataendelea kuhudumiwa pale pale na atalelewa katika wodi ya watu wenye matatizo ya akili.
Roy alitoa maelezo kuwa mama yule pia ana mtoto mdogo wa mwezi mmoja ambapo maelezo yote aliacha pale kisha madaktari wakamuhaidi kushughulikia hilo swala kwa kuwa hosptali ile ina wafadhili hakuna shida na ndani wiki moja au mbili watampa majibu mazuri.

Roy aliondoka pale akilia kwani mateso yote anayoyapata mama mchungaji ni yeye ndio chanzo mpaka amekuwa kichaa alijilaumu sana.
Alirudi nyumbani akamweleza Ester kila kitu kilichoendelea.Ester alishangaa sana baada ya kujua kuwa mtoto ni yule wa Roy aliyezaa na mama mchungaji,alimuonea sana mama mchungaji huruma kwa yaliyomtokea pia hakumlaumu Roy kwani alijua fika Husna ndio chanzo na alihaidi kumlea yule mtoto siku zote za maisha yake kama mtoto wake wa kumzaa.

Wiki mbili baadae Roy na Ester wakiwa nyumbani wamejipumzisha baada ya chakula cha mchana walisikia honi getini.
"Ester kafungue geti sijui nani anagonga"
"Nenda wewe buana mimi nmefunga kanga tu hapa ndani sijavaa chochote ebu angalia nilivyo"

Ester alijitetea

Roy baada ya kufungua geti alikutana na watu asiowafahamu,Baada ya Salam watu wale walijitambulisha kuwa ni wafanyakazi katika hosptali ya mawenzi na wamekuja kumchukua yule mtoto wa mama mchungaji na Roy anatakiwa kuongozana nao mpaka kituoni kwa ajili ya maelezo akiwa kama msamaria mwema.

Roy alishtuka sana kusikia mtoto anachukuliwa.Aliingia ndani akabadilisha nguo na kuondoka bila kumwambia Ester chochote ingawa Ester alimuuliza anapokwenda na mtoto lakini Roy hakuweza kuzumza chochote kwa wakati ule.

Wakiwa njiani Roy alikuwa amempakata mtoto wake huku machozi takimtoka,wazo lilimjia awapige wale maafisa kisha atoroke na mtoto.Akiwa na mawazo hayo akipoangalia nje alimuona Husna akiwa na mtu mmoja mnebe mwenye kitambi wanatembea pembeni ya bara bara.Roy alishtuka sana kidogo amdondoshe mtoto.Aliwaomba wale maafisa wasimamishe gari lakini walikataa kitendo kile kilimkera sana Roy akachungulia nje na kuita Huuuuusnaaaa.....

Itaendelea

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment