Marafiki club-32
by Sparner Boy 0765148781
ilipoishia..
Siku moja baada ya chakula cha usiku mchungaji alimkalisha mke wake amueleze tatizo na kinachomsibu mpaka anakuwa katika hali ile.
Endelea
mchungaji alizungumza kwa sauti ya upole akimsihi mke wake amueleze tatizo lakini mama yule hakuzungumza zaidi ya kulia sana mpaka mchungaji akapata kazi ya kum'bembeleza.Alipopunguza kulia mchungaji aliendelea kumuuliza tatizo ni kitu gani ambapo alimwangalia mume wake kisha akamwambia..
"nitakuambia mume wangu,nisamehe pia na mungu anisamehe pia"
"sawa nieleze basi mimi ni mume wako nitakusamehe"
"asante sana kama utanisamehe,lakini nitakuambia siku ya jumapili kanisani"
"mbele ya kanisa ni mbaya,siri zetu za ndani kwa nini upeleke kanisani"
"hili kosa nimekukosea wewe na kanisa pia,nataka nisamehewe na kanisa nzima pia niongozwe sala ya toba upya niwe mtu mpya.sijui kama Mungu atanisamehe mimi"
alizungumza hayo ma mchungaji na kuanza kulia tena kwa kwikwi.Mchungaji alimwelewa mke wake na kumshika mkono kisha wakaelekea kitandani.
........
Siku mbili baadae mchungaji alipata taarifa kuwa Ester amefukuzwa nyumbani baada ya kugundulika kuwa ni mjamzito na akakataa kumtaja aliempa ujauzito ule.Habari zile zilifikuwa pigo kubwa kwani Ester alitegemewa na alikuwa kama nguzo imara kwa vijana wa pale kanisani.Habari zilifikishwa kwa viongozi wa kanisa na kama ilivyo kawaida kwa makanisa ya kilokole wazee walikaa mipango ikapangwa kuwa jumapili itakayofuata Ester atatolewa kundini kwa kosa la uzinzi na kubeba mimba kabla hajaolewa.
Habari hizo pia zilichoma moyo wa mama mchungaji kwani alikuwa ana amini kuwa aliyempa Ester mimba ile ni Roy ingawa hakuwa na uhakika lakini aliamini hivyo.Ilipofika siku ya ijumaa mama mchungaji alimpigia simu Roy na baada ya salamu alimsisitiza kuwa jumapili asiache kwenda kanisani kwani baada ya ibada kuna kitu anataka kuongea nae.Roy alikubali kila alichoambiwa na alikuwa na hamu ya kujua ma mchungaji amefikia muafaka gani mpaka wakati ule.Kwa kifupi Roy alikuwa anajuta sana kwa mambo aliyoyafanya kwa mabinti mbali mbali wakiwemo wa pale kanisani pamoja na mama mchungaji.
Mpaka inafika jumapili Mariam hakuwa ameonekana wala simu yake haikuwa inapatikana,Ester hakuwa na raha ata kidogo lakini kwa upande wa Roy alikuwa kawaida kwani alijua mtu aliyepotea ni Husna ambapo mda wote amekuwa akiishi nae akijua kuwa ni Mariam na ndie aliyemsababishia matatizo yale yote.Kila akiwaza kuhusu Mariam na Husna alihisi kuchanganyikiwa lakini alimficha Ester hakumwambia chochote.
* * *
Siku ya Jumapili Waliamka wakajiandaa tayari kwenda kanisani,Ester hakutaka kwenda siku hiyo kutokana na aibu ya kubeba mimba lakini Roy alimwambia asiogope kwani yupo tayari kila mtu afaham kuwa yeye ndie muhusika wa mimba ile.
"Nakupenda Ester nipo tayari wafahamu kila kitu na ikiwezekana tunahamia kwa shangazi Arusha"
"sawa lakini kuhusu wifi mimi nina wazo"
"wazo gani"
"twende tukaseme kanisani maombi yafanyike atarudi mimi namwamini sana Mungu"
Roy alinyamaza kidogo akatafakari maneno ya Ester kisha akatikisa kichwa kukubali lakini moyoni alitambua kabisa Mariam hataweza kurudi.
Walifika kanisani wakiwa wamechelewa kidogo na ibada ilishaanza mda mfupi uliyopita.Kila mtu aliwaangalia na wengi wao walihisi kuna kitu baina yao kwani habari za Ester kufukuzwa nyumbani zilishaenea kwa chini chini kiasi kwamba nusu ya kanisa walishapata habari zile hivyo walipoingia kwa pamoja walishangaa.
Vipindi mbali vya pale kanisani viliendelea na mda mfupi ma mchungaji aliingia na kukaa kwenye viti vya kawaida tofauti na ilivyozoeleka huwa anakaa kwenye viti vya mbele pembeni na mchungaji sasa mchungaji siku hiyo alikuwa na wazee wa kanisa pekee kitu kilichofanya waumini kutoelewa kinachoendelea.
Baada ya vipindi mbali mbali vya pale kanisani,kiongozi wa ibada wa siku hiyo alisimama na kusema kuwa mama mchungaji anataka kuongea na kanisa hivyo wamkaribishe kwa makofi.
Makofi na vigele gele vilipigwa na mama mchungaji akaelekea mbele ya kanisa.Baada ya kuwasalimu kwa jina la Yesu, kila mtu alikaa kimya wakati huo mchungaji anajifuta jasho huku mapigo ya moyo wake yanaenda mbio kwani hakujua ni kitu gani mke wake alitaka kuliambia kanisa.Wakiwa katika hali ya ukimya sana,mama mchungaji aliomba Roy atoke mbele ya kanisa pia ambapo Roy huku anatetemeka aliinuka na kwenda kusimama mbele ya kanisa pembeni na mama mchungaji huku anajitahidi kuficha uoga wake uliokuwa unaonekana wazi wazi...
Itaendelea..

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment