Marafiki Club-31
By Sparner Boy 0765148781
ilipoishia..
Wakati anawaza hayo simu yake iliita na alipoangalia Mariam ndio alikuwa anapiga
endelea
Roy aliiangalia simu ile bila kupokea huku anatetemeka kwa uoga,simu iliita sana na ilipokata akaizima na kuitupa kitandani.Alijiinamia akawa anawaza alichokisoma alitamani iwe ndoto lakini haikuwa hivyo.Wakati anawaza afanye nini wazo lilimjia atoroke na Ester warudi Arusha kwa shangazi na ikiwezekana arudi kwao kenya kwani matatizo aliyokuwa nayo kwa wakati ule aliona afadhali yale aliyoyakimbia kenya.Wakati anawaza hayo alishangaa simu yake inaita,alishtuka sana kwani ni muda mfupi tu ameizima na alipoangalia aliona jina la Mariam kwenye screen yan Mariam ndio alikuwa anapiga.Haraka alichukua simu ile akaizima kisha akatoa kwenye sim hivyo sim ikabaki bila betri.Alijilaza kwa kwa mgongo pale kitandani akiwa kwenye dimbwi la mawazo na wakati anajishauri afanye nini mara simu yake iliita.aliinuka pale kitandani kama mshale akiwa anapiga kelele kama mtu aliyeona nyoka mkubwa uuwii,,Ester njoo,,maamaa..
Alipatwa na kiwewe baada ya kuona sim yake inaitwa wakati haina betri,alikimbia pembeni ya ukuta na kujibanza huku anatetemeka mda huo simu ikiwa inaendelea kuita.Ester alitoka bafuni akamkuta Roy akiwa anatetemeka huku simu inaita.
"roy nini tatizo unapiga kelele?"
"ni simu..simu..hiyo hapo"
"imefanyaje alafu inaita kwa nini hupokei na Mariam ndio anapiga"
Ester aliongea hayo na kuchukua ile simu tayari kumpelekea Roy Lakini Roy alimwonyesha ishara kuwa asimpelekee yeye hataki kuongea pia asimsogelee abaki nayo ukouko.Ester alipokea simu ile ambapo alisema haloo,,haloo..lakini hakuna aliyemjibu na aliposikiliza simu ile kwa makini alisikia sauti ya mtu akipigwa,alikuwa analia kwa uchungu lakini watu wanaompiga hawakuonekana kujali.Ester aliposikiliza alishtuka sana kwani sauti ile iliyokuwa inalia kwa uchungu ilifanana na ya Mariam na wakati anasikiliza simu ilikatika.
"roy,Roy Mariam amevamiwa na majambazi we unaogopa kupokea simu?"
"ang..alia haina betri"
aliongea Roy uku anatetemeka kwa uoga na Ester alipogeuza simu ile alishangaa kwani haikuwa na betri mda wote hakuwa ameligundua hilo pia ilikuwa imezima na alipojaribu kuiwasha haikuwaka mpaka walipoweka betri.Ester alimwangalia Roy kwa mshangao na kumwambia
"labda ni miujiza ya Mungu amekusaidia ujue Mariam yupo kwenye hatari"
"kwa nini unasema hivyo"
"nimemsikia akilia pia nimesikia sauti za kipigo naomba twende tukamwokoe"
Roy alikataa lakini Ester alisisitiza sana,Roy alitamani kumwambia Ester ukweli lakini alisita na mwisho akakubali waende wakamwangalie Mariam na ikiwezekana wamsaidie.
Ester alivaa kisha wakapanda kwenye gari haraka safari ikaanza usiku ule ule,bara barani Roy aliendesha gari kivivu sana kwani alikuwa anaogopa huenda Mariam akawadhuru,ni yeye tu anayejua kuwa yule sio Mariam bali ni Husna kutokana na barua aliyoisoma.Walifika na kupaki gari nje ya geti,akafungua buti na kutoa lichuma flani linalokuwa humo kisha kwa mwendo wa kunyata na umakini mkubwa wakaanza kuingia ndani.Roy alipoangalia milango na geti aligundua kuwa zipo kama alivyoacha mda mfupi walipotoka na Ester.Alimtanguliza Ester yeye akawa anafuata kwa nyuma akiwa ameshika chuma ile mkononi na alikuwa tayari kwa lolote,uoga aliyokuwa nao ulitoweka gafla.
Walipofika sebuleni walitulia na kusikiliza ambapo kulikuwa na ukimya wa ajabu.Aliwasha taa zote lakini palikuwa shwari na salama kabisa,walipoelekea chumbani walishangaa kwani kitanda kilikuwa kitupu Mariam hakuwepo.
Roy na Ester walitizamana na ukimya wa mda mfupi ukatanda,hakuna aliyejua Mariam alipo na walimtafuta sana nyumba nzima bila mafanikio na kibaya zaidi ata simu yake haikuwa inapatikana.
"atakuwa amekwenda wapi wifi yangu ametekwa jamani,,tumpigie mama mchungaji alafu twende polisi"
"hapana tusubiri kwanza atarudi huwa inatokea analala nje na nyumbani"
"lakini nimesikia akipigwa tena akilia kwa uchungu"
"hilo swala niachie mimi we pumzika subiri niingize gari ndani"
Roy baada ya kuingiza Gari aliingia ndani ambapo hakwenda chumbani bali alilala kwenye Sofa lakini kila akifumba macho taswira ya Husna ilikuwa inamjia,mwisho uoga wa ajabu ulimwingia hivyo akaelekea chumbani ambapo alimkuta Ester amejipumzisha.Alipanda kitandani tayari kuutafuta usingizi.
* * *
Kwa upande wa Mchungaji alishindwa kumuelewa mke wake,alikuwa amebadilika sana tofauti na alivyomzoea yani kila mara alikuwa ni mtu wa kusononeka pia na kulia bila sababu yoyote.Siku moja baada ya chakula cha usiku mchungaji alimkalisha mke wake amueleze tatizo na kinachomsibu mpaka anakuwa katika hali ile...
Itaendelea

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment