HONGERA MANCHESTER UNITED

Author
NILIYOYAONA Community Shield.

Manchester United 2-1 Leicester City

1. Rashford na Lingard labda tu uchawi wa majeruhi uwakute lakini kinyume na hapo hawa makinda wana maisha marefu sana chini ya Jose Mourinho na wana maisha marefu sana ndani ya Manchester United.

2. Eric Bertrand Bailly, kwangu huyu leo alikuwa "MOTM" mshikaji ameonyesha utulivu sana eneo la nyuma, zile pauni milioni 30 zilizolipwa kwa kiasi kikubwa leo zimeonekana, ingawa bado anahitaji uzoefu lakini kwa leo nimemwelewa.

3. Zlatan Ibrahimovic, katika umri wa miaka 34 hutamwona akikimbia mara nyingi sana ila utamwona kwenye eneo la 18 mara nyingi, na kile kichwa kimethibitisha uhusiano wake na nyavu umekomaa sana. Ingawa bado anahitaji kuelewana na Wazza.

4. Rooney and Carrick leo hapana, ni kama wachezaji wageni waliosajiliwa na hii ilikuwa mechi yao ya kwanza kubwa, bado Wazza hajakaa sawasawa kama "rafiki" wa Zlatan na Carrick kasi ya LCity ilimpa shida eneo la katikati.

5. United wanapata goli la ushindi dk ya 83 halafu dk ya 88 anatoka Rooney anaingia Schneiderlin hapo ndipo unapojua kwamba kwasasa kocha ni JOSE MOURINHO na habari ya filosofia na zama za LVG zishawekwa kando. Ingawa bado United hawajakaa sawa vile ambavyo ungeweza kutembea kifua mbele kama shabiki wa mashetani wekundu.

6. Leicester City ni walewale ukijumlisha na Ahmed Musa, washikaji bado wameonyesha kasi na mfumo wao wa kushambulia kwa kushtukiza (counter attack), na pia wameonyesha kwamba wao ni mabingwa watetezi.

7. Vardy na Musa wakicheza pamoja hilo balaa halitakuwa la kawaida, na kwa mfumo wa Lcity wa kushambulia kwa kushtukiza hawa ni wachezaji stahiki kuboresha mfumo huo chini ya Ranieri, iliwachukua dk sita toka kuingia kwa Musa, Lcity kusawazisha.

8. Mahrez sijui anasumbuliwa na ofa za Arsenal ama simu za Wenger, leo sikumwona kabisa ni kama vile bado yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa msimu, sikumbuki sana wapi alimpita Luke Shaw kirahisi.

9. Kwa Claudio Ranieri kufungwa leo nafikiri ndiyo anatakiwa kufahamu kwamba ligi ishaanza kwa upande wao na kila timu atakayocheza nayo watataka kuwamaliza, hakuna raha kama kumfunga bingwa mtetezi, awaulize Chelsea watamjuza.

10. KARIBUNI TENA KWENYE MAANDISHI HAYA KWA MECHI NYINGI ZIJAZO.

@Chikoti Cico

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment