HADITHI YA KUZUGIA-02

Author
HADITHI,SAFARI YA MAREKANI,
SEHEMU YA PILI (2),
MTUNZI Deo Young Massawe,
MAWASILIANO 0769297430.
sehemu ya pili (2)
Baad ya masaa kumi na sita tayari ndege iloyowabeba akina Anekke na kundi lake lilikua anga ya Marekani na wahudumu walitangaza, ni mda karibu ndege inatua.
Katika uwanja wa ndege wa Los Angeles watu wengi walikusanyika kusubiria wageni wao waliotoka sehemu mbali mbali na ilikua mwendo wa saa tatu usiku. Wakati huo Michael Reuben alikua katika ukumbi mmoja wa starehe uliokua kama kilomita 100 kutoka uwanja wa ndege na kwakua alikua na ahadi ya kuwapokea wageni wake basi alikua anatoka kuelekea kwenye gari yake aina ya Bugatti New model ambayo iliweza kutembea kilomita 250 kwa lisaa limoja hivyo yeye alikua atembee kilomita 100 kwa dakika 25 tu.

"Waooh this is America it's beautiful one" (waooh hi ndo Marekani, ni nzuri sana),
Sikujua alianza kwa kuongea kiingereza kwani aliona kila mwenyeji wa pale aliongea kiingereza ila Anekke aliwaasa kutoongea kingereza ,
"Jaman sisi hapa tukiwa watano tusiongee kiingereza na hata huyu tunaemsubiri akija anajua kiswahili hivyo lugha tutakayotumia ni kiswahili tu",
Waliyaongea hayo wakiwa wamekaa kumsubiri Michael Reuben ambae kwa maelezo ya Anekke ndo alitakiwa kuja kutoa ajira.

Baada ya nusu saa Michael Reuben alifika pale na Sikujua alikua wakwanza kuongea kana kwamba ndo alikua kiongozi nyuma ya Anekke,
"Shkmoo baba"
"Marahaba mwanangu"
Michale Reuben alikatiza mazungumzo ya Sikujua kwa kumvuta Anekke pembeni,kumsifu kwa kazi nzuri aliyofanya, ila akamwambia "nilikua nataka kuelekea California kuna mzigo wangu umekamatwa huko na askari polisi wametaka kuonana na mimi hivo nasafiri saivi kwa hiyo endelea kukaa na hawa watu hadi nitakaporudi sasa chukua hiki kiasi cha hela uwazungushe kila mahali wanapotaka kuenda ndani ya nchi hii maana nikirudi naanza nao kazi mara moja hivyo kabla hawajaanza kuteseka wewe watembeze kwanza",
Michael Reuben alisema hayo na kumkabidhi fedha ambayo ingewatembeza nchi yote ya Marekani.
" Sasa jaman ndugu zangu huyu anaetaka kuwaajiri amepata safari kidogo hivyo nitaedelea kuwa mwenyeji wenu hapa hadi atakaporud"
"Sasa kazi hatutapata tena ?" Sikujua aliongea kwa kufoka wakati huo akina Hilary, Gema,na Jumanne ambae kwa wakati huo anaitwa jina kwa lugha ya kiingereza basi J'four walikua kimya kumsikiliza kiongozi wao. Anekke aliwatoa wasiwasi kwa kuwaambia kuhusu kuwatembeza kila mahali watakapotaka kuenda kwani Anekke alikua kasoma somo la Geography hiyvo kila aliposhika ramani ya eneo husika basi alilielewa mapema ukizingatia ujanja pia ilikua asili ya raia wengi wa Nigeria.
"Jaman tunamkumbuka mwalimu Sabas alitufundisha kuna kimondo kilidondoka katika jimbo la Arizona huku twendeni huko basi" hapo Gema alitoa pendekezo,
"Wewe kwa hiyo umekuja kuangalia kimondo huku Marekani mbona hujawahi kuenda Mbozi kule Mbeya ukaangalie" Sikujua aliongea kwa shauku ya kusema mahali anapotaka aende yeye na kwa kua basi hela ilikuepo ya kutosha basi walianzia safari yao jimbo la Arizona.
Wote walifurahia kwa jinsi walivyotembezwa na kuamini mungu wao anatenda kazi kwani hawajawahi kukaa mahali wafikirie kama kuna siku wangekuja kuabudiwa hadi kutembezwa kama watalii kwa gharama za watu.Walijikuta wakifananisha jimbo la Arizona na wilaya ya kiteto ambako shughuli ya kule ilikua kilimo cha mahindi na wote walifuarahi sana kuona kimondo pamoja na kukipiga picha.
Siku nyingine walitembelea jiji la New York nako pia walifurahia sana wakajikuta wakifananisha na jiji la Dar es salam,Tanzania kwani kule walifurahia kuona kila kona kunafanyika biashara za kila namna maduka makubwa yalionekana watu wakifanya manunuzi katika super market.
Kisha walitembelea hadi Washington DC nako walifananisha na Dodoma nchini Tanzania kwani waliona kila mtu kavaa suti na tai hivyo basi kwa haraka wakajua ni mji wa viongozi wa nchi. Walipofurahi zaid ni pale walipoenda jiji Miami kwani walikuta ndiko kwenye kila aina ya starehe kwani wasanii wengi walikuja kutumbuiza katika kumbi mbalimbali za huko na walifurahi zaid kupelekwa ufukwe wa bahari,hivyo wakawa wameupenda zaid mji wa Miami kwani starehe walizokuta huko hazikutofautiana sana na za Los Angeles.

Baada ya mwezi mmoja Sikujua na kundi lake walishazoea mazingira ya nchini marekani japokua waliteseka kuzoea hali ya ubarid wa kule basi walijikaza na wakafanikiwa kuzoea na kwa hapo walikua wamepiga kambi jijini Texas kwa mapunziko ili wamsubirie sasa Michael Reuben kwani washaridhika na matembezi hivo wanataka sasa kuanza kazi kwani wamezunguka sana hadi wanashangaa kwa nini sisi tunazunguka tu akati mwenyewe mtoto wa rais wa nchi hii tulimkuta kule Boston,Washington DC akihudumia mgahawani nasi tutafanya kazi kama yeye. Wakati wanaongea hayo Anekke huwa anawasikitikia tu kwani anajua sio kazi wameitiwa bali ni kama kifo wamefuata.
*
Katika mawasiliano ya barua pepe Anekke alipata ujumbe wa Michael Reuben kua anakuja na anapitia kwanza jimbo Colorado kwani kuna vidonge alikua anafuata huko vyakuja kutumika kwenye kazi ambayo akina Sikujua wangeifanya.
Michael Reuben aliamini kanini moja ya kua pale unapokua na vyanzo vingi vya pesa basi ndio unatengeneza pesa nyingi zaidi hivyo yeye alikua na biashara nyingi na kubwa na haramu ambazo alizifanya kupitia watu wengine yeye akiwa kama mkubwa wao ilikua vigumu mtu kumjua kwani alikua mnyeyekevu mbele za watu pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa watu.Mojawapo ya biashara zake ilikua kusambaza madawa ya kulevya kutoka nchini Pakistani na kusafirisha kwenda nchi mbali mbali hasa barani Africa kama vile Zambia, Libya, Misri na Africa kusini ambako katika nchi ya Africa kisini basi majiji maarufu kama Durban,Johannesburg,KwaZulu Natal na mengineyo yalishamiri kwa matumizi ya madawa hayo yaliyokua yanasambazwa na Michael Reuben. Pia alifanya biashara ya bangi kutoka Jamaica na kusambaza katika nchi mbali mbali za ulaya na maeneo mengine yenye baridi.Pia alikua kiongozi wa vikundi mbali mbali vya ujambazi kwa kuwapa silaha.
"Hii biashara nitakayoenda kufanya na hawa vichaa kutokea huko Tanzania nahisi itanilipa sana" Michael Reuben alijisemea moyoni akiwa njiani kuelekea mjini Texas sasa tayari kuenda kuwachukua watu wake na kumkabidhi Anekke mshahara wake. Na tayar alikua na vidonge vya kutosha vya kutumia kwenye biashara mpya aliyoibuni ambayo angeifanya na akina Sikujua.
"Tena walivyo na mvuto lazima hii biashara itakua nzuri na nitakua tajir zaidi ya hapa" alijisemea Michael Reuben huku akipandisha ngazi kuelekea chumba cha hoteli walimokua wamepanga akina Anekke.


Itaendelea.
Usikose maana nahisi tutajua ni biashara gani itaenda kufanyika basi kama inalipa na sisi tuliobaki Tanzania tuifanye.

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment