HADITHI FUPI YA KUZUGIA

Author
HADITHI,SAFARI YA MAREKANI,
SEHEMU YA KWANZA (1)
MTUNZI Deo Young Massawe,
MAWASILIANO 0769297430.

sehemu ya kwanza (1).

"Mambo mrembo"
"Poa kaka za sahizi"
"Nzur tu dada nimekuona tokea nkiwa mbali umesimama hapa juani vipi dada kunani ?"
"Acha tu kaka nina mawazo yangu binafsi kuna ofisi nilipeleka vyeti vyangu vya kuombea kazi wala sijafanikiwa me nimechoka kabisa saiv heri tu nirudi nyumbani nikakae na mama yangu nimsaidie angalau kazi,"
"Kwa nini dada unasema hivo ?/kwani huna ajira?"
"Kaka angu huu ni mwaka wa sita natafuta ajira sijapata na ndo hivo sina mtaji wa kufanya hata biashara yoyote sijui hata nifanye nini",
"ooh sawa dada mimi naitwa Anekke naishi Tanga ila hapa Dar es salam nipo kwa ajili ya kutafuta watu wanne yaani wavulana wawili na wasichana wawili,wote wawe na mvuto maana wanahitajika kufanya kazi katika mgahawa mmoja huko Marekani,sijui kama nawe utakuabali hiyo tenda dada uangu",?
" ooh my God (ooh mungu wangu) umejibu maombi yangu, naomba kaka yangu nisaidie tu maana nimeteseka sana kupata ajira sasa kama ipo ya kutoka tena nje ya nchi ndo nzur nkakae na wazungu",
"Sawa dada nitakusaidia, tena wewe itabidi ukakae reception (mapokezi) maana una mvuto wa kutosha,sasa chukua namba zangu za simu ili tuwasiliane ila cha kufanya we tafuta msichana mmoja mwenye mvuto kama wewe na wanaume wawili wenye mvuto maana mgahawa wenyewe lazima wakae watu wakuvutia wateja".
Hayo yalikua maongezi kati ya Anekke na mwanadada alieitwa Sikujua, waliokutana katika kituo cha daladala huko Posta,Dar es salaam, Sikujua alikua kashika bahasha yenye vyeti na bahasha ilionekana kuchakaa kana kwamba hubebwa Mara kwa Mara akizunguka katika maofisi mbalimbali kuomba kazi bila mafanikio kwani alikua mtu wa kujiheshimu hivyo alijikuta kila ofisi anayoingia anakutana na viongozi wa kiume hivyo kwa uzuri aliokua nao basi aliombwa rushwa ya ngono kwenye kila ofisi aliyopeleka vyeti,na yeye alishaapa hatokaa atoe mwili wake kupata kazi na ndo kitu kilimfanya kutopata kazi kwani kila alipoombwa mapenzi alijibu kwa zarau na kuondoka.
*
Anekke ambae aliejitambulisha kwa Sikujua kwa uhalisia wake alikua mzaliwa wa Lagos Nigeria, ila alikaa sana nchini Tanzania ambapo pia alijitahidi kujifunza lugha ya kiswahili na kwa hiyo kwa alivyokua kila mtu aliamini ni mtanzani.
Anekke alijihusisha na biashara ya kuuza binadamu kutoka nchi mbali mbali za Africa na kuwasafirisha nchi za ulaya na uarabuni ambapo alijipatia utajiri mkubwa sana,kwani biashara hiyo alifanya kwa siri sana na alitumia pesa nyingi kuhonga ili kupata visa na kuhonga balozi husika kutia sahihi ya safari za halali. Kazi hiyo aliifanya kwa kuagizwa na matajiri wakubwa zaidi yake na kwa wakati huo ilikua ni kazi ya kumtafutia tajiri mmoja alieitwa Michael Reuben, aliishi jimbo la Los Angeles,Marekan ila alikua mtu wa kuzunguka sana katika majiji makubwa duniani ili kujiingizia kipato kwa kazi aliyokua anafanya.

"Shoga hebu njoo hapa home chapu nikupe mchapo na wewe acha kujifungia tu ndani wanakwambia mtembea bure sio sawa na mkaa bure"
"Hee! nawe Sikujua ukishapata mwanaume akikununulia kichupi tu lazima uniite ili nikuone ukikijaribisha, kwa nini huyo mwanaume asikuvalishe huko huko ?"
"Shoga njoo mwenzio tunakwea pipa huyoo Marekani,"
"Mm Kweli leo umelewa marekani tena? ila ngoja nifike hapo kwako maana nilitoka kwa Jumannne saiv kuzungumza nae kuhusu lile suala la kikundi chetu kuanza kilimo cha matikiti huko Hedaru",
" weeeee! shogaa mambo ya matikiti tuwaachie waliokataa shule sie tunaenda Marekani ".
Yalikua maongezi kati ya Sikujua na rafiki yake aitwae Gema, kwa pamoja walihangaika kwa siku nyingi kutafuta ajira baada ya kumalizia masomo ya chuo kikuu,na hadi wakati huo walishakata tamaa ya kutafuta ajira kwani walishaunda kikundi chao cha watu sita kwa ajili ya kuenda kulima matikiti maji Baada ya dakika 20 Gema alikua kashafika kwa Sikujua,
" sasa shoga angu leo nikiwa nasubiria daladala pale posta akatokea kaka mmoja sio mkaka sana yaani ni mwenye umri kama miaka 40 hivi tena handsome sana, tukaongea then (alafu) akanipa namba ya simu ili nimpigie kwani kanambia tunaenda kupewa kazi huko marekani ya kuendesha mgahawa wa kitalii sasa kanambia mimi nitafute msichana mmoja tuwe wawili na wanaume wawili,maana mgahawa unahitaji wahudumu wanne ndo maana nkakuita wewe hapa",
"Heeee! nikweli au unatania ?",
" nikweli kabisa we lazima tufanye haraka maana tiketi zishaandaliwa kila kitu yani sisi hatutoi hata mia yeye anatugaramia kila kitu",
"Sasa wewe Sikujua kama umeambiwa wanne na sisi unajua tuko kikundi cha watu watano marafiki tusiotengana itakuaje na ndo hivi tunataka tukalime kwa pamoja ??
" haaa ! Gema nishakuambia jembe tuachie waliokimbia umande na pia nimesisitizwa kua nitafute wenye mvuto hivyo basi sisi wawili tushakamilika wasichana wanaume wenye mvuto wenye mvuto katika kikundi chetu ni Hilary na Jumanne, ila huyu furaha na Benjamini mungu kawanyima mvuto hivyo watabaki huku wakalime pamoja,tena ikiwezekana waoane ili wazidi kuendeleza kizazi cha watu wenye sura mbaya",
Sikujua na Gema waliongea mengi na hapo wakaamua kuwaita akina Hilary na Jumanne ili kuwajulisha huo mpango wakupata kazi nchini Marekani.

"Ongea dada nakusikia"
"Nilikua nakwambia tayar nishapata wenzangu"
"Wana mvuto lakini ?"
"Kama ulivonambia yaani kama huyu mwenzangu ana viziwa viko kama vya mtoto wa miaka sita kwa kweli tuko vizuri kaka na pia tushajipanga tayar kwa safari.
" sasa Fanya hivi wapige picha pamoja na wewe unitumie kwenye WhatsApp ".
Yalikua mazungumzo kati ya Anekke na Sikujua.
Hapo hapo Anekke aliwasiliana na Michael Reuben kwenye barua pepe (E-mail) ambapo kwa wakati huo alikua Ontario nchini Canada kwa shughuli zake, alimfahamisha kurudi Los Angeles Marekani,kwani atamletea watu wake alioagizwa ili aweze kulipwa pesa yake,kwani Anekke ndo ilikua kazi yake akishakukabidhi watu wako basi yeye huchukua hela yake na kuondoka.

Jumanne na Hilary waliandamana pamoja na marafiki zao yaani Furaha na Benjamini,
"sasa jamani Sikujua shoga angu unaniacha huku mwenyewe ?" Furaha alimuuliza Sikujua,
" utabaki na Benjamin usiogope sisi tutawatumia pesa kidogo kwa Western Union,nyie mtakua mnalima matikiti kwa wingi huku" Sikujua aliongea kwa kejeli na hapo Benjamin na Furaha wakaondoka kwa hasira kwani waliona wivu wenzao kuondoka na kuwaacha,ila Benjamin alikua na upeo wa akili sana na ghafla alimuamuru Furaha warudi kuna kitu alisahau kuwaeleza hao wanaosafiri na bila ubishi Furaha akakubali warudi.
"Ila Sikujua angalieni huko mnakoeda maana kuna mtoto wa shangazi yangu alichukuliwa hivyo hivyo kupelekwa kwa wazungu ila mateso aliyoenda kupata mungu ndo anayajua maana alie___"
Kabla hajamalizia Sikujua alimtemea mate ya usoni na Benjamin aliondoka kwa aibu pamoja na Furaha.
"Nendeni huko na lifuraha lako tena mkalime pamoja yaani mungu angewapa mvuto nanyi tungeenda na nyie ila rafiki yenu jembe wivu tu mnao hapa nyooooo!" Sikujua aliwasindikiza kwa maneno ya kejeli.
Tayari kikosi cha watu wanne kilikua tayari kwa safari na hapo wote walipanga waage nyumbani kua wamepata kazi huko Bujumbura,Burundi, kwani Sikujua alipewa mashariti ya kutosema ukweli kwa wazazi wao na wote wakawa wasiri kwa wazazi wao.
Baada ya kujipanga kwa kila kitu basi safari ilipangwa ifanyike jumamosi. Na hapo waliwasiliana na Anekke kwamba wapo tayari ndipo wakapanga wakutane uwanja wa Julius Nyerere.
**
Mida ya saa tatu kasoro robo usiku siku ya jumamosi tayari Sikujua,Gema, Jumanne na Hilary walikua uwanja wa Julius Nyerere wakimsubiri Anekke huku wakipiga story mbali mbali
"Yaani mwaka huu ni wangu nikifika kitu cha kwanza namtafuta Rihhana nipige nae selfie nipost kwenye Facebook" Sikujua alisema,
"Mimi nataka Beyonce awe mwenyeji wangu" Gema alisema,
"Mimi namuonaga tu Anord Schezniger kwenye runinga sasa nitamuona uso kwa uso" Hilary alisema
"Mimi kuanzia saiv nataka mniite J'Four" nae Jumanne alisema wote wakacheka na hapo Anekke akatokea akiwa na visa zenye hadi passport size.Hapo hakuna alieuliza wa kujiuliza visa imeandaliwaje maana walikua na hamu tu ya kusafiri.
Walipanda ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ambapo safari ilitakiwa waende watue Addis Abab nchini Ethiopia kisha waruke tena hadi Qatar na hapo wapande ingne kutoka Qatar hadi Los Angeles Marekani hivyo basi kutoka Qatar hadi Los Angeles walitakiwa wakapande ndege yenye kutembea masafa marefu angani nayo ilikua ndege kutoka kampuni ya Emirates.
Anekke alikaa siti ya nyuma huku Sikujua na wenzake wakikaa siti za mbele.wote wakiwa na hamu ya kufika mapema.
Huko Los Angeles nako Michael Reuben alikua akisubiria Anekke alete watu wake.

Itaendelea....

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment