MARAFIKI CLUB -30

Author
Marafiki Club-30
By Sparner Boy 0765148781
ILIPOISHIA
baada ya kupekua alipata bahasha ile na kurudi nayo kitandani akiwa na hamu ya kujua kichokuwa kimeandikwa mle ndani na haraka akaanza kuifungua.
Endelea
Aliifungua huku mikono inamtetemeka ambapo ndani alikuta Barua ikiwa imekunywa vizuri.Ile ameanza kuikunyua simu yake iliita kwa sauti ya juu,Alichukua simu yake na alipoiangalia ilikuwa ni namba mpya,kabla hajapokea aliangalia saa ya ukutani iliyokuwa imetundikwa mle chumbani ambapo ilionesha ni saa 5:45 usiku.
Taratibu alibonyeza kitufe cha kupokea simu na kusema
"hallow"
"Roy ni mimi Ester nipo apa getini nyumbani nimefukuzwa kwa sababu ya huu ujauzito,sina pa kwenda nifungulie"
Roy aliposikia maneno yale taratibu alitoa sim sikioni na kuikata bila kuongea kitu chochote kwan alihisi mwili wote umekufa ganzi na ubongo umeganda hakuamini alichosikia.wakati anawaza afanye nini simu ilipigwa tena ambapo safari hii hakupokea alitoka nje na ile barua akaiacha pale pale kitandani huku nia yake ikiwa ni kumzuia Ester asiingie ndani kwa kuhofia kumchanganya Mariam.Alipofika getini hakuamini macho yake baada ya kumwona Ester akiwa na begi kubwa la nguo kitendo kilicnomaanisha kuwa hakukuwa kabisa na uwezekano wa yeye kurudi kwao.
"Imekuwaje tena"
"nimefukuzwa nyumbani,wamenilazimisha sana nimtaje muhusika wa hii mimba lakini sijakutaja ndio wakakasirika na kuamua kunifukuz..."
Aliongea maneno hayo Ester na kabla hajamalizia sentensi yake alianza kulia.Roy alimkumbatia na kumuambia asijali kila kitu kitakuwa sawa.
Ester alimwelewa Roy na akawa anataka kuingia ndani lakini Roy akamzuia,Ester alimwangalia Roy kwa mshangao na kabla hajauliza swali lolote Roy alimwambia..
"shshsh..sitaki Mariam ajue,ni mkali sana na hatakubali uishi humu ndani"
"Sasa kama unanifukuza mimi nitaenda wapi jamani yaani wewe leo ndio wa kunifanyia.."
"basi Ester naona hujanielewa,mimi sikufukuzi nipo na wewe,sasa naomba nisubiri hapa"
Aliongea hayo Roy kwa sauti ya kunong'ona huku akionekana mwenye wasiwasi sana kisha akaingia ndani.Alielekea chumbani akamwangalia Mariam aliyekuwa usingizini kisha akawaza
"mda huu Naomy ametoka ata ugomvi wetu haujaisha,sitaki amuone Ester,,no siwez kufanya hivi Mariam ataumia sana"
Alichukua funguo za gari akatoka mpaka mlangoni lakini kabla hajatoka nje aliikumbuka ile Barua,alirudi akaichukua na kuweka mfukoni kisha akatoka.Alimfungulia Ester wakaingia kwenye gari na kutoka kwa mwendo wa taratibu wakati huo Mariam hana habari yupo usingizini bado.
* * *
"Roy tunakwenda wapi saa izi"
"nataka tutafute gest yoyote tukae apo siku mbili tatu wakati tunatafuta nyumba"
"kweli tutaishi wote,asante sana lakini lazima dada Mariam tumwambie"
"ukitaka nikuache na usinione kamwe wewethubutu kumwambia,fuata ninachokuambia mimi"
Roy aliongea kwa msisitizo huku akiwa amekunja sura mpaka Ester akaogopa na kukaa kimya.Baada ya mwendo walifika kwenye mtaa wa pili kutoka mtaa walipotokea ambapo kuna umbali kidogo lakini sio sana.Baada ya kuzunguka walipata gest iliyokuwa imejificha kidogo.Waliangalia chumba na baada ya kuridhika nacho Roy alilipia siku saba ambapo waliingia wakakaa kitandani,Ester alimkumbatia Roy na kumuambia
"Nakupenda sana Roy nipo tayari kuishi na wewe maisha yoyote yale"
"Nakupenda pia Ester,wewe ni mke wangu"
"asante Mpenzi twende tukaoge"
"mimi Tayari"
"twende buana"
Ester alim'bembeleza sana Roy Wakaoge wote lakini Roy alikataa na kumwambia Ester akaoge tu kwani yeye tayari ameshaoga.
Ester alifungua begi lake akatoa kanga kisha akavua nguo na kujifunga kanga ile,akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye bafu iliyokuwepo chumbani mle.Roy alimpenda Ester kwa sababu alikuwa mpole pia alikuwa msikivu na anayeheshimu kila anachoambiwa tofauti na Naomy ambae alikuwa m'bishi na mwenye nyodo nyingi.Wakati Ester akiwa Bafuni Roy alikumbuka ile barua aliyoachiwa na Husna ambayo hakuisoma mwanzo,Alipapasa mfukoni kwa bahati nzuri akaipata na haraka akaifungua na kuanza kuisoma ambapo ilikuwa na maneno machache sana tofauti na alivyotegemea,alisoma mara mbili mbili lakini hakuelewa maneno yale yaliyokuwa yameandikwa hivi:
"Roy pole na kazi ngumu niliyokupa,najua umeimaliza yote na ata kama sio yote basi umeifanikisha kwa kiasi fulani ndio maana umeweza kusoma barua hii,najua utashtuka sana lakini mimi sikufa na nipo na wewe kila siku,Alikufa Mariam na mimi nikavaa sura yake kiukweli aliniudhi sana.Nafurahi kuwa na wewe na ikimpendeza baba tutakuwa ivi milele."
wako
Husna.
Roy jasho lilimtoka kwani hakuamini wala kuelewa alichokisoma.Wakati anawaza hayo simu yake iliita na alipoangalia Mariam ndie alikuwa anapiga...
Itaendelea

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment