Marafiki Club-25 Sparner Boy 07148781
ilipoishia
aliongea hayo Ester na kuondoka kwa hasira akielekea kanisani ambapo mama mchungaji alikuwepo pamoja na baadhi ya wazee wa kanisa..
Endelea..
Roy alijishika kichwa kama mtu aliyesikia taarifa za msiba wakati Ester alipokuwa anaelekea kanisani,alitamani amkimbilie kumzuia lakini alishindwa alipokumbuka kuwa alishatembea na wasichana wengi sana pale kanisani hivyo aliogopa kuamsha mambo mengine watakapomuona.Ester alifika mlangoni akasimama baada ya kumuona ma mchungaji akiwa na wazee wa kanisa,alisimama kwa dakika kadhaa kisha akaondoka na kuzunguka nyuma ya kanisa akisubiri ma mchungaji amalizane na wazee wale kwanza.Roy akiwa amesimama huku anatetemeka,Naomy alimfuata akamshika bega na kumuuliza
"baby nini kinaendelea kati yako na Ester"
"hakuna pia naomba niache"
"sawa nakuacha lakini namsubiri mchungaji"
"hapana nakutania mpenzi wangu we ni mke wangu au unapenda mmeo nihaibike?"
aliongea Roy kwa unyenyekevu Naomy akatikisa kichwa kukubali kuwa amemsamehe na baada ya kuongea kidogo Naomy aliaga na kuelekea nyumbani.Baada ya Naomy kuondoka Roy alimfuata Ester kule nyuma ya kanisa ambapo alimkuta amejiinamia huku analia,alimwinua akamkumbatia na kumwambia kuwa watoke eneo lile watafute mahali palipotulia waongee vizuri pia akimpa moyo kuwa mambo yale yatakwisha,alim'bembeleza sana mpaka Ester akakubali.Walienda kwenye mgahawa mmoja maarufu mkoani kilimanjaro ambapo walikaa kwenye bustani nzuri iliyopandwa majani na maua kwa umahiri wa hali ya juu.Roy alianza kumpanga sana Ester watoe ile mimba lakini Ester hakuonekana kuelewa. Kwa upande wa Roy alijua ile mimba ata Ester asipoitoa Husna ataichukua lakini atakuwa amepata aibu pale kanisani hivyo aliona bora atoe mapema Husna afurahi pia heshima yake ibaki pale pale.Alipoona Ester ameshikilia msimamo wake,Roy alipiga magoti huku analia kama mtoto akimsihi akubali watoe ile mimba.Roho ya huruma ilimwingia Ester,alimwinua Roy pale chini akamkumbatia na kumwambia
"Roy unanipenda?"
"ndio nakupenda"
"najua nikitoa hii mimba utaniacha tu"
"hapana sintakuacha mpenzi nakuhaidi"
"sawa nimekubali kuitoa"
aliongea Ester huku machozi yakimtoka na kulowanisha mabega ya Roy walipokuwa wamekumbatiana.Roy alifurahi sana aliposikia maneno yale kutoka kwa Ester na walipanga jumanne inayofuata watakwenda hosptali kwa ajili ya kutoa mimba ile na Ester akakubali kwa kutikisa kichwa.Walikula wakanywa mpaka majira ya saa 12 jioni kisha wakapanda kwenye gari Roy akampeleka Ester mpaka kwao na yeye akageuza gari tayari kuelekea nyumbani.Akiwa njiani aliwaza sana kuhusu wasichana wote wa pale kanisani aliowapitia kuwa wote wapo kwenye janga lile mpaka mama mchungaji,alichanganyikiwa zaidi alipokumbuka kuwa Mariam pia na yeye tayari yupo kwenye idadi ile ya wasichana 50.Alisimamisha gari pembeni akapiga piga usukani kwa hasira na kwa mara ya kwanza alijilaumu sana ni kwa nini alikutana na Husna aliyempa kazi ile ngumu na ya kikatili.Pale pale wazo la kwenda bar kunywa pombe walau apunguze mawazo lilimjia.
Alitafuta Bar iliyotulia akaingia na kuanza kuagiza pombe kwa fujo.Alikunywa akalewa chakari kisha akaegemea juu ya meza,pale alipitiwa na usingizi mpaka saa saba kasoro usiku wahudumu wa bar ile wakiwa wanajiandaa kufunga bar walipomuona.Wal
imwita meneja na kumuambia kuna mtu amelala.Meneja alikuja akamwangalia Roy na kuwauliza wahudumu
"amekunywa pombe ya shilingi ngapi"
"elfu 60 boss"
"ooh,mteja mzuri sana nyie endeleeni kukusanya viti mi nitampeleka nyumbani niitie mtu wa boda boda anifuate kwa nyuma"
Meneja alimwinua Roy alimkokota mpaka kwenye gari na kumuuliza anapoishi lakini Roy ulimi ukawa mzito kujibu,Baada ya kumuuliza mara kadhaa alitaja mtaa na nyumba anayoishi hivyo meneja akampeleka mpaka nyumbani kisha yeye akarudi na boda boda iliyokuwa inamfuata.
Mariam siku hiyo alishangaa sana kwani hakuwahi kumuona Roy katika hali ile,alimkokota mpaka kitandani akamlaza mpaka asubuhi.
* * *
Siku waliyokuwa wamepanga Roy na Ester kwenda kutoa mimba ilifika.Roy alimpigia Ester majira ya saa nne asubuhi wakakutana na safari ya kwenda hospitali ikaanza.
Walikwenda hosptal moja maarufu ya kulipia kisha wakaonana na daktari.Roy alieleza shida yake akidanganya kuwa yule ni mwanafunzi na imetokea bahati mbaya.Daktari alimsikiliza Roy kwa makini na kumwambia
"hili swala haliruhusiwi kisheria lakini nitakusaidia una laki moja na elfu ishirini?"
"ndio"
aliitikia Roy haraka na kutoa pesa zile kisha akamkabidhi daktari ambapo alizipokea akamchukua Ester na kuingia nae kwenye chumba kimoja wakamuambia Roy kuwa awasubiri kwa nje.
Ilipita muda mrefu bila docta kutoka,Roy alianza kuogopa kila mara alikuwa anaangalia saa yake.Baada ya masaa kadhaa daktari alitoka akamwita Roy pembeni na kumwambia
"ndugu yangu pole sana"
"pole ya nini docta Ester yupo wapi"
aliuliza Roy huku anatetemeka kwani kwa hali aliyokuja nayo daktari iliyonesha kuwa hali haikuwa nzuri humo ndani..
Itaendelea

posted from Bloggeroid
0 comments:
Post a Comment