MARAFIKI CLUB -26

Author
Marafiki Club~26
by Sparner Boy 0765148781
Ilipoishia
aliuliza Roy huku anatetemeka kwani kwa hali aliyokuja nayo daktari iliyonyesha kuwa hali haikuwa nzuri humo ndani
endelea,,
docta alimwangalia Roy kwa sekunde kadhaa kisha akamuambia kuwa imeshindikana mimba imekataa kutoka na endapo wataendelea kujaribu kutoa mimba ile basi Ester atapoteza maisha.
Roy alishangaa sana kwa nini imekuwa hivi.Alimpeleka Ester mpaka kwao kisha na yeye akaanza safari ya kwenda nyumbani kwake.
Alifika nyumbani akajitupa sofani akiwa na mawazo sana.Akiwa kwenye dimbwi la mawazo Mariam alitoka chumbani alipokuwa amepumzika mchana ule na kumfuata.Alim busu na kumuuliza
"unawaza nini mpenzi"
"naomba niache sipo vizuri"
"nikuache kwa nini kwanza bora umekuja"
"naomba niache Mariam sipo vizuri kwa sasa tafadhali"
aliongea hayo kwa upole mda huo mariam mkono wake ulishafika kwenye zipu ya Roy inaonekana alikuwa anataka mchezo wa kikubwa.Mariam alimsikiliza Roy kwa makini kisha akamuacha na kurudi chumbani huku anatingisha makalio yake yaliyokuwa ndani ya kanga moja.
Jumapili iliyofuata baada ya ibada Ester alimfuata Roy na kumuuliza
"sasa tunafanyaje Roy unajua nyumbani wakijua nitafukuzwa pia apa kanisani sijui nitakuwa mgeni wa nani"
"usihofu mpenzi nitajua cha kufanya we tulia wakianza kukushtukia niambie"
aliongea hayo Roy akiamini kuwa mda wowote mimba ile ingearibika Husna angeichukua.
Ester alitikisa kichwa kuwa amekubaliana na maneno ya Roy.Wakati wanaongea hayo Roy alimuona Naomy anakuja pale alipokuwa amesimama na Ester,alipowafikia aliwasalimia kisha Naomy akamwambia Roy kuwa watoke pembeni kidogo ana maongezi na yeye.
Roy alimuaga Ester na kumfuata Naomy
"Bwana asifiwe Naomy"
"apa hakuna cha bwana asifiwe Roy sijui nitakuwa mgeni wa nani mimi"
"tatizo nini unaumwa?"
"nina Mimba Roy nina mimba sijui itakuwaje"
Roy alihisi kama moyo umepasuka baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa Naomy,kigugumizi cha ghafla kilimpata asijue la kufanya.Baada ya ukimya wa muda mfupi Roy alimuuliza Naomy
"sasa tunafanyaje mpenzi"
"tuoane haraka kabla mambo hayajaaribika"
"whaat?"
"ndio hivyo kama nilivyokuambia na wiki hii naenda kwa dada yako Mariam kumueleza ukweli"
Roy alihisi mwili wote umekufa ganzi kwani pale kanisani wanajua yeye na Mariam ni mtu na dada lakini wale ni wapenzi na Roy hakujua ni kwa nini Mariam alikuwa anawaambia watu kuwa yeye ni kaka yake.Aliondoka bila kuongea chochote kwani alihisi kuchanganyikiwa.
Ilipita wiki 3 bila mimba yoyote kuaribika kama alivyotarajia,alishangaa kwa nini Husna ameamua kumfanyia vile kwani alikuwa anaelekea kuumbuka vibaya sana.
"mbona mimba haziharibiki,au nimemkosea nini Husna na kazi hii sifanyi tena kama ni kuniua aniue tu"
aliwaza hayo Roy kwani alihisi kazi ile imekuwa mzigo mzito kwake.
* * *
Ester mimba yake ilishaanza kuonekana,siku moja wakiwa wametoka kwaya mama mchungaji alimuita na kumwambia
"Ester wewe ni msichana mwenye tabia nzuri pengine kuliko wasichana wote hapa kanisani"
"asante mama mchungaji"
"lakini sijui shetani amewezaje kukuteka mwanangu,hiyo mimba ni ya nani?"
"mama..mimi ss..sina mimba,mimba ip,,pii"
alijibu Ester kwa kigugumizi na mshtuko wa hali ya juu.Mama mchungaji alim'bembeleza sana amuambie ukweli wa ile mimba lakini Ester akakataa kuwa hana mimba.
Mama yule alihis kitu fulani, alimpigia Roy simu na kumuambia kuwa kesho yake aende kwake kuna maongezi wanataka wazungumze.
Roy aliitikia kwa wasiwasi kwani hakujua kwa nini mama mchungaji ameamua kumuita kwake.
Kesho yake aliitikia wito wa mama yule wa kanisa,alifika akakaribishwa vizuri mama mchungaji alikuwa peke yake kwa wakati ule.Roy alikaa huku anashangaa nyumba ile utadhani ndio mara yake ya kwanza kuingia.
"Roy nimekuita hapa kuna kitu nahisi sasa sijui kama kina ukweli ndani yake"
"kitu gani hicho mama mchungaji?"
"unajua sielewi nini kilitokea mpaka nikamsaliti mume wangu na kijana mdogo kama wewe,tangu nioane na mchungaji miaka 17 iliyopita sijawah kumsaliti,sasa mimi nahis wewe siyo mtu wa kawaida"
"mama mchungaji ina maana mimi ni.."
"shshs,,,mbaya zaidi huwa natumia uzazi wa mpango na ndio natumiaga miaka yote hiyo lakini nashangaa umenipa ujauzito sijui imeingiaje,pia Ester ana mimba nahis ni yako lakini sina uhakika sana"
Jasho jembaba lilimtoka Roy baada ya kusikia maneno yale..Alishindwa ajibu kitu gani pia alichanganyikiwa aliposikia ma mchungaji ana mimba yake pia.
Akiwa amejiinamia asijue la kujibu mama mchungaji alimuuliza
"niambie tu ukweli wewe ni ajent wa shetani au wewe ni nani"
Roy aliinua kichwa chake akamuangalia mama mchungaji na kabla hajamjibu simu yake iliita na alipoangalia Naomy ndio alikuwa anapiga.
Alipokea na baada ya kusalimiana Naomy akamwambia
"Nipo njiani nakuja kumueleza Mariam ukweli kuwa mimi ndio wifi yake"
"usije sipo nyumbani nimetoka"
"hapana mimi namtaka dada yako Roy siwezi hii aibu mimi"
aliongea hayo Naomy na kukata simu,Roy alikuwa kama aliechanganyikiwa.
"Huuuuuusnaaaaa!!"
Roy alipaza sauti iliyomshtua mama mchungaji.

Itaendelea

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment