MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa
CCM, (UWT), Sophia Simba, amekiri wazi
kwamba wabunge vijana kutoka vyama vya
upinzani wanaweza kujenga hoja wawapo
bungeni tofauti na walce wa Chama tawala
(CCM).

Mbali na hilo aliwataja
wajumbe wa Baraza Kuu
Maalum la umoja huo
kuwachagua wabunge
watakaozunguza bungeni kwa
kujenga hoja badala ya
kuwepo bungeni kama watalii.
Alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa
baraza hilo mjini hapa , Simba amesema kuna
maneno asiyoweza kuyaongea yeye bungeni
lakini vijana wanaweza kuyazungumza
kutokana na malezi.
Alisema kuna kila sababu ya kuwachagua
viongozi ambao wataweza wana uwezo
mkubwa wa kutetea hoja pindi wawapo
bungeni badala ya kwenda huko kwa lengo la
kutambishiana kwa mavazi.
“Chagueni watu watakaoengea bungeni. Nyie
mmefundishwa kujiamini, kuna maneno
ambayo mnaweza kuyasema lakini mimi
siwezi kuyasema,”amesema.
Mbali na hilo Simba amesema uchaguzi wa
mwaka huu ni tofauti na chaguzi zilizopita,
wanawake watakaochaguliwa wahakikishe
wanafanya kampeni kwa lengo la kukipatia
ushindi chama chao.
“Kuna jambo baya ambalo linafanywa na
baadhi ya wabunge wa Viti Maalum
wakichaguliwa wanaenda zao Ulaya kununua
nguo na mabegi jambo kubwa ni kutambiana
na kuoneshana mavazi wawapo bungeni.
“Hawaonekani kwenye kampeni, safari hii
tunawaangalia. Sio kupaka lipstic tu bali mje
kufanya kampeni,”amesema.
Amesema katika uchaguzi mkuu uliopita
walipata tabu kwasababu walipokuwa wakifika
kwenye kampeni wilayani wabunge hao wa
kuteuliwa walikuwa hawaonekani.
Simba amesema pia UWT iliwataka makada
watakaoshinda ubunge wa Viti Maalum kutoa
Sh100,000 kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa
magari ya umoja huo lakini waligoma kutoa.
Kabla ya kuanza kwa kwa kikao hicho baadhi
ya wajumbe wa baraza hilo walihoji juu ya
kutoonekana kwa majina yote ya wagombea
Viti Malum kupitia Jumuiya ya wazazi.
Hata hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi, Zakhia
Meghji, aliwaondoa hofu kuwa majina yote ya
walioshinda mkoani kupitia jumuiya hiyo
yatapigiwa kura katika baraza hilo.
Kauli iliyoungwa mkono na Katibu Mkuu wa
UWT, Amina Makilagi, aliyewaomba radhi
wajumbe kuwa hawakuweza kuingiza maelezo
binafsi ya wagombea viti maalum kupitia
jumuiya ya wazazi na vijana kutokana na
kuchelewa kuyapata majina hayo.
Akanusha kumfuta Lowassa
Simba amesema hana mpango wa kuhama
CCM kama baadhi ya watu wanavyoandika
katika mitandao ya jamii.
Simba ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati
Kuu (CC) waliojitokeza hadharani na kumtaka
kuwa kanuni zilikiukwa katika zoezi la uchujaji
wagombea.
Wengine waliojitokeza kupinga maamuzi ya
CC hadharani ni Dk. Emanuel Nchimbi na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam
Kimbisa.
Simba amesema hajawahi kufikiria wala
kupanga kuhama chama hicho.
“Nafahamu kwamba CCM ndiyo iliyowezesha
watu kunifahamu, naringa, natamba kwa
sababu ya CCM. Nimejipanga kuongoza timu
ya wanawake kunamepeleka Dk. John
Magufuli Ikulu, tumevunja kambi zetu zote
tumebaki na kambi moja ya
tingatinga,”alisema.
Kuhusu Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa, Simba amesema kila mtu anahama
chama kwa sababu zake na kwamba yeye
hana sababu ya msingi ya kufanya hivyo.
“Yeyote atakayeondoka CCM, hatupi mtikisiko
ni uhuru wake kufanya hivyo, CCM haiwezi
kutetereka kwa wachache wanaohama sisi
mamilioni hatuhami na tupo strong (imara),”
amesema Simba.
Mbwembwe za wapambe
Kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza hilo,
wapambe wa wagombea walionekana wakiwa
wameshika mabango yanayowanadi
wagombea wao wamnaowaunga mkono.
Wapambe hao wakiwa wameshikilia mabango
walikuwa wamesambaa hadi nje ya lango kuu
la kuingilia katika jengo la makao makuu ya
chama hicho maarufu kama White House.
Miongoni mwa mabango yaliyoonekana katika
eneo hilo ni la Rita Mlaki, Halima Bulembo na
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Angella Kairuki.
Uchaguzi wa wawakilishi wa wabunge wa viti
maalum kutoka makundi mbalimbali ya
Jumuiya za wazazi, vijana, wafanyakazi, watu
wenye ulemavu na vyuo vikuu.

0 comments:
Post a Comment