WAKATI wabunge 51 wakiangushwa katika
mchakato wa kura ya maoni, ambao
unatumika kumpata mgombea atakaye
kiwakilisha chama katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu, David
Kafulila – Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR –
Mageuzi) amepita bila kupigwa ndani ya
chama chake.

Sababu kubwa inayotajwa na
wananchi kusababisha
wabunge hao kuangushwa ni;
kushidwa kuwawakisha
wananchi Bungeni na
kushidwa kushirikiana na
wananchi wanaowaongoza
katika kutatua kero
zinazowakabili.
Kwa upande wa Kafulila, hali ni tofauti.
Anajivunia kuwajibika ipasavyo. Japo
hakufikia malengo kwa asilimia 100, lakini
kwa hatua iliyofikia katika kutatua
changamoto za wananchi wake katika jimbo
analoliongoza na ngazi ya taifa
anajihakikishia kurudi bungeni iwapo tu
“matokeo ya uchaguzi hayatachakachuliwa.”
Katika mahojiano
Kafulila anasema, “sikuahidi kutatua kila kero
na matatizo ya jimbo. Lakini niliahidi
kuonesha tofauti ya jimbo kabla na baada ya
miaka mitano ya uongozi wangu.”
“Niliahidi kujenga heshima ya jimbo letu
bungeni na taifa kwa ujumala kupitia hoja
niliyoitoa ya ESCROW. Serikali ilivunjika.
Kuivunja serikali ndio kilele cha uwajibika
katika vita dhidi ya mafisadi,” anasema
Kafulila.
Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya jimbo
hilo Kafulila anasema alipewa jimbo ikiwa
ukanda mzima wa ziwa hauna huduma ya
simu, leo kata zote za ukanda huo zina
huduma hiyo.
“Nimepewa jimbo ukanda wa ziwa haupitiki
kwa barabara; Leo barabra zimebaki kilomita
chache ifike Kalya na madaraja zaidi ya 19
madogo yamejegwa. Kata ya mtego
imeunganishwa kwa barabara,” anasema
Kafulila.
Amehakikisha serikali inatekeleza ahadi ya
ujenzi wa barabara mbili za lami zenye urefu
wa Kilomita 126 na kufanya jimbo hilo kuwa
na mtandao mrefu wa lami kuliko jimbo lolote
mkoa wa Kigoma na ndio jimbo pekee
lililopata lami 2010- 2015 katika mkoa huo.
Mbali na kero ya barabara, jimbo hilo
halikuwa na vivuko bora hasa ubovu wa
kivuko cha Ilagala. Kwa sasa kuna kivuko
bora kutoka Uholanzi chenye thamani ya Sh. 3
bilioni ingawa kwenye ilani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ujenzi wa kivuko hicho
haukuwemo.
“Nimehakikisha serikali inatekeleza ahadi ya
ujenzi wa daraja malagarasi iloshidwa tangu
mwaka 1979 kwenye mpango wa kwanza wa
maendeleo na hata miaka mitano ya kwanza
ya utawala wa Rais Kikwete,” amesema
Kafulila.
Pia, jimbo hilo halikuwa na utaratibu wa
kusomesha watoto yatima au wale wanaotoka
katika familia zisizojiweza. Kafulila
amefanikiwa kusomesha watoto 200 huku
wengine wakifanikiwa kumaliza na kuendelea
na elimu ya juu.
Katika kuhakikisha maendeleo katika sekta ya
elimu yanapanuka katika jimbo analoliongoza
Kafulila anasema, “Nimepeleka vifaa maabara
(mobile laboratory) katika shule za sekondari
17, rekodi ambayo hakuna jimbo katika mkoa
wa Kigoma limefikia hatua hiyo.”
“Nimepeleka vifaa vya computers, printers, fax
na mashine za photocopy katika shule za
sekondari tano za; Ruchungi, Nguruka,
Kalenge, Sunuka na Ilagala na kutumia mfuko
wa jimbo kuanzisha ujenzi wa shule ya
sekondari Basanza,” ameeleza Kafulila.
Aidha, katika kukabiliana na changamoto ya
afya hasa afya ya mama na mtoto,
amefanikisha ujenzi wa kituo cha afya katika
kata ya Kalya kwa hoja na mchango wa moja
kwa moja;
Amefuta tatizo la vitanda na magodoro katika
kituo kikubwa cha afya Nguruka kwa kupeleka
magodoro 20, vitanda 20, shuka 30 na
kuchangia juhudi za ujenzi wa kituo cha afya
Kazuramimba.
Kuhusu kupunguza kero ya upatikanaji wa
maji safi na salama, Kafulila amehakikisha
jimbo hilo linapata miradi mitano mikubwa ya
maji Rukoma, Nguruka, Uvinza, Kandaga na
Ilagala. Amesaidia upatikanaji wa visima
vifupi kata ya Mtego, Chagu na anaendelea na
juhudi hizo katika kata ya Mgaza.
“Nimehakikisha serikali imekubali kulipa
mafao ya waliokuwa wafanyakazi wa mgodi
wa chumvi Uvinza tangu mwaka 1999.
Niliahidi kuhakikisha kiwanda cha chumvi
kinaacha kutumia kuni kutokana na uharibifu
wa mazingira. Serikali ipo tayari kukifunga
mpaka hapo mwekezaji atakapobadilisha
teknolojia,”amesema Kafulila.
Mafanikio mengine ambayo Kafulila
anajivunia kupatikana wakati wa uongozi
wake katika jimbo hilo ni ujenzi wa mtandao
wa umeme ambapo kwa kuanzia unajegwa
Ilagala, Mwakizega, Simbo, Kandaga,
Kazuramimba, Uvinza na Basanza. Pia
anaendelea kupigania tarafa ya Nguruka ipate
kituo cha umeme. Ukanda wa ziwa utapata
umeme baada ya mpango wa REA unaofuata.
Kuhusu kuwainua wajasirimali wadogo
anasema aliishawishi benki ya Twiga na
kupeleka jimboni kwake mafunzo ya banki
vijijini (Vikoba) na kufanikisha Halmashauri
ya jimbo hilo kupata trekta 10 za mkopo
kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Ametoa vifaa vya michezo kama jezi na mipira
kwa timu za vijiji vyote jimbo zima. Na baadhi
ya kata zimeshiriki katika michezo kiwango
cha ligi.
Katika kuimarisha utwala bora jimboni kwake
Kafulila anasema, “Nimeendera kupinga
utawala mbovu wa mkuu wa wilaya bungeni
mpaka nishtakiwa polisi kwa kuwatetea
wananchi wangu kutokana na vitendo vya
mkuu wa wilaya kuchoma nyumba za
wakulima.”
“Nimewapigania wananchi wangu hasa
ukanda wa ziwa kwa kuitwa wakimbizi na
serikali hii. Nilipambana mbele ya waziri mkuu
na kuwatoa katika vizuizi wakazi wengi
waliokamatawa. Nilirudishaia hadhi na
heshima yao,” ameeleza Kafulila.

0 comments:
Post a Comment