Kasi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kukihama chama hicho inazidi
kupanda chati.
Madiwani 18 wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro, jana walitangaza kuhama rasmi.
Madiwani hao waliwakilishwa ofisi za
Chadema Mkoa wa Arusha jana na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elias
Ngorisa aliyeambatana na Diwani wa Kata ya
Engusero Sambu, Kagil Mashati Ngukwo,
ambaye pia alikuwa Katibu wa Fedha na
Uchumi wa CCM Wilaya ya Ngorongoro.
Pamoja nao walikuwepo wazee wa mila wa
Kabila la Wamasai (malaigwanani) Laurence
Ngorisa na Lekakui Oleiti, wote kutoka
Engusero Sambu.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua
Nassari, ndiye aliyewapokea makada hao na
kuwapatia kadi za Chadema.
Akizungumza baada ya kupokea kadi, Elias
Ngorisa, alisema wapo madiwani 18 kati ya
28 ambao tayari wamechukua kadi za
Chadema.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wanawake (UWT), Wilaya ya Siha, mkoani
Kilimanjaro, Susan Natai na madiwani
wengine wawili, wamejitoa CCM na kujiunga
Chadema.
Mbali na Natai, wengine waliojiunga na
Chadema ni Denengwa Leole ambaye ni
Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kashashi,
Diwani wa Viti Maalum, Tarafa ya Siha
Magharibi, Eliaika Kileo na aliyekuwa
mgombea wa kiti cha udiwani, Kata ya
Gararagua, John Sambua maarufu kama
Mwarabu.
(CCM) kukihama chama hicho inazidi
kupanda chati.
Madiwani 18 wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro, jana walitangaza kuhama rasmi.
Madiwani hao waliwakilishwa ofisi za
Chadema Mkoa wa Arusha jana na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elias
Ngorisa aliyeambatana na Diwani wa Kata ya
Engusero Sambu, Kagil Mashati Ngukwo,
ambaye pia alikuwa Katibu wa Fedha na
Uchumi wa CCM Wilaya ya Ngorongoro.
Pamoja nao walikuwepo wazee wa mila wa
Kabila la Wamasai (malaigwanani) Laurence
Ngorisa na Lekakui Oleiti, wote kutoka
Engusero Sambu.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua
Nassari, ndiye aliyewapokea makada hao na
kuwapatia kadi za Chadema.
Akizungumza baada ya kupokea kadi, Elias
Ngorisa, alisema wapo madiwani 18 kati ya
28 ambao tayari wamechukua kadi za
Chadema.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wanawake (UWT), Wilaya ya Siha, mkoani
Kilimanjaro, Susan Natai na madiwani
wengine wawili, wamejitoa CCM na kujiunga
Chadema.
Mbali na Natai, wengine waliojiunga na
Chadema ni Denengwa Leole ambaye ni
Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kashashi,
Diwani wa Viti Maalum, Tarafa ya Siha
Magharibi, Eliaika Kileo na aliyekuwa
mgombea wa kiti cha udiwani, Kata ya
Gararagua, John Sambua maarufu kama
Mwarabu.






0 comments:
Post a Comment