PROF. LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI CUF

Author
Prof. Lipumba akiongea na waandishi wa Habari kwenye Hoteli ya Peacock

Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti kwenye chama chake cha Wananchi CUF.

Ametangaza kuachia ngazi uenyekiti wa chama hicho mapema leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacok.

Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.


Prof Lipumba akitaja sababu za kujiuzulu nafasi ya uenyekiti CUF

Sentensi za Prof. Lipumba akiwa na waandishi wa habari
Habari wakuu,
Baada ya sintofahamu ya jana, leo mwenyekiti wa CUF ameamua kujiuzulu nafasi yake kama mwenyekiti wa chama cha CUF, Prof Lipumba atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa CUF. Ameita waandishi wa habari na kuongea baada ya jana kuzuiwa na wazee.

Sababu ni kutokwenda sawa na wenyekiti wenza wa UKAWA kuhusu kumuunga mkono mtu na kuwapokea watu ambao wamehusika na kutengeneza rasimu ya katiba mpya ambayo yeye hakubuliani nayo na yeye anaunga mkono rasimu ya katiba ya jaji Warioba.

Atashiriki kupigia kampeni wagombea ukiacha Urais na alipoulizwa kuhusu kuhusu kuchukua uamuzi huu sasa kasema dhamira yake inamsuta na walipomuuliza kuhusu pesa kasema hata kumuita mgombea ambae atagombea kupitia UKAWA wanashutumiwa wamepokea pesa hivyo hilo halimsumbui bali dhamira yake na nia ya kuungana kuitetea rasimu iliyopigwa teke na CCM.

0 comments:

Post a Comment