MAKUNDI ya vijana yameonekana kumiminika
mithili ya kumbikumbi warukapo wakati wa
masika wakimsindikiza mgombea urais
Edward Lowassa anayewakilisha Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Lowassa ambaye alifika makao
makuu ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kuchukua
fomu za kugombea, amefanya
hivyo chini ya mwamvuli wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA), ulioanzishwa wakati
wa Bunge Maalum la Katiba.
Makundi ya vijana yalionekana katika nyuso
zilizojaa furaha na bashasha wakithibitisha
imani yao kwa Lowassa ambaye alihamia
Chadema baada ya kukatwa jina lake katika
kile alichokieleza mwenyewe “mpango wa
kunihujumu.”
Vijana walijitokeza na masanduku ya mfano
wa jeneza, wakiimba nyimbo za kumtaka Dk.
John Magufuli anayegombea urais kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ahame chama
hicho na kuingia kambi ya Ukawa.
Vijana wanaonekana kuguswa na nguvu
iliyoimarika katika kundi la UKAWA wakiamini
nguvu hiyo itakidhi kiu yao ya mabadiliko ya
uongozi nchini.
Lowassa alihama CCM mapema mwezi huu na
kujiunga Chadema, chama alichosema
kimepata mafanikio makubwa katika kujenga
mtandao nchi nzima.
Tangu alipohama CCM, Lowassa amekuwa
akirudia maneno yaliyosemwa na Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwamba
“Watanzania wanataka mabadiliko na
wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya
CCM,” akimaanisha kuwa ameingia Chadema
na kubeba dhamana ya UKAWA ili kusaidiana
na viongozi wao kutafuta mabadiliko
waliyoshindwa kuyaleta CCM.
Hali imekuwa tofauti na ilivyotarajiwa kuwa
kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim
Lipumba, kuwa kungesababisha mpasuko CUF
na UKAWA, badala yake maelfu ya
wanachama wanaendelea kumuunga mkono
Lowassa kuwa Rais.
“Nimepata faraja sana kujiunga na Ukawa
japo kumekuwa na misukosuko. Ni lazima
tuwe wamoja, mtunze kadi zenu za kupigia
kura. Mwaka huu lazima tushinde, tena kwa
kura asilimia 90 ili wakiiba asilimia 10
tusisikitike,” amesema Lowassa alipozuru Ofisi
Kuu za CUF jana ambako pia alihutubia
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililofanya
kikao cha dharura kutafuta kuziba nafasi ya
mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa chama
hicho.
Lowassa aliondoa uvumi kwamba
akichaguliwa kutakuwa na vurugu nchini.
Alisema kutakuwa na utulivu mkubwa na
wafanyabiashara hawana sababu ya kuhofu.

0 comments:
Post a Comment