LOWASSA: KIKWETE AMEARIBU UCHUMI

Author
EDWARD Lowassa, mgombea urais wa
Chadema amesema, Rais Jakaya Kikwete
ameharibu uchumi wa Tanzania.


Akizungumza na wafuasi wa
Chadema pia UKAWA katika
ofisi za Chadema mara baada
ya kuchukua fomu ya kuwania
urais kupitia chama hicho
amesema, “rafiki yangu
Jakaya Kikwete ameuharibu
uchumi wa nchi yetu,”
ameongeza:
“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani
kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300.
Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300.
Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”
Aidha Lowassa amesema, katika kipindi cha
utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila
aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi
chochote katika historia ya Tanzania.
“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo
wameuwawa kuliko kipindi chochote katika
historia duniani kote.
“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko
kipindi chochote katika historia ya nchi yetu.
Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed
(kasi), ambaye hawezi akae pembeni,”
amesema Lowassa.

0 comments:

Post a Comment