HALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa
wa Mwanza si shwali baada ya aliyekuwa
Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo
(Fashion), na wanachama zaidi ya 100
kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF)
Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwendelezo wa
wimbi la wanachama wa CCM kuhamia
upinzani hususani Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA.
Diwani na wanachama hao
kutoka matawi mbalimbali ya
CCM, walieleza chanzo na
sababu za kutimkia CUF, kuwa
chama hicho kimetawaliwa na
vitendo vya rushwa, chuki na
undugu kitendo
kinachosababisha kukosekana
kwa demokrasia ya kweli.
Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi
ya chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia
rushwa kushika madaraka na kusababisha
watu ambao ni wazalendo wenye nia dhabiti
ya kuwatumikia wananchi kukosa haki hiyo.
Wanachama hao wakiongozwa na diwani
huyo, walipokelewa leo na Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa CUF, Karume Jeremiah,
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika
eneo la Chakechake, Nyamagana.
Akizungumzia tamko la wao kujiengua CCM
na kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia
hatua hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo
alivyodai vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu
na hila na kukosekana kwa demokrasia.
“Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa
waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magori
ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa
tumekuja huku upinzani. Lazima
tuwashughulikea mpaka waachane na wizi
wao.
“Niliwania udiwani kwa mara nyingine tena,
hila na tamaa ya CCM walinikata jina kwa
sababu nilikuwa napingana nao,
walipolazimisha fedha za miradi ya wananchi
tuzitumie kwa mambo ya chama,” amesema
Fashion.
Kwa upande wake, Jeremiah amesema
kutokana na CCM kushindwa kuwatumikia
wananchi ipasavyo, sasa umefika wakati
wakaipisha UKAWA kuingia `magogoni` ili
kutatua kero za watanzania.
wa Mwanza si shwali baada ya aliyekuwa
Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo
(Fashion), na wanachama zaidi ya 100
kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF)
Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwendelezo wa
wimbi la wanachama wa CCM kuhamia
upinzani hususani Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA.
Diwani na wanachama hao
kutoka matawi mbalimbali ya
CCM, walieleza chanzo na
sababu za kutimkia CUF, kuwa
chama hicho kimetawaliwa na
vitendo vya rushwa, chuki na
undugu kitendo
kinachosababisha kukosekana
kwa demokrasia ya kweli.
Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi
ya chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia
rushwa kushika madaraka na kusababisha
watu ambao ni wazalendo wenye nia dhabiti
ya kuwatumikia wananchi kukosa haki hiyo.
Wanachama hao wakiongozwa na diwani
huyo, walipokelewa leo na Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa CUF, Karume Jeremiah,
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika
eneo la Chakechake, Nyamagana.
Akizungumzia tamko la wao kujiengua CCM
na kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia
hatua hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo
alivyodai vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu
na hila na kukosekana kwa demokrasia.
“Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa
waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magori
ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa
tumekuja huku upinzani. Lazima
tuwashughulikea mpaka waachane na wizi
wao.
“Niliwania udiwani kwa mara nyingine tena,
hila na tamaa ya CCM walinikata jina kwa
sababu nilikuwa napingana nao,
walipolazimisha fedha za miradi ya wananchi
tuzitumie kwa mambo ya chama,” amesema
Fashion.
Kwa upande wake, Jeremiah amesema
kutokana na CCM kushindwa kuwatumikia
wananchi ipasavyo, sasa umefika wakati
wakaipisha UKAWA kuingia `magogoni` ili
kutatua kero za watanzania.






0 comments:
Post a Comment