Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimevuna wanachama 60 wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kitongoji cha Wangbay, kijiji cha
Logia, Kata ya Sigino Wilaya ya Babati.
Akikabidhi kadi wanachama wapya Mbunge wa Viti Maalum, Paulina
Philipo Gekul, jana, katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya
Logia aliwaasa wananchi kuwa wavumilivu iwapo makada wenzao wanaogombea
udiwani wakishindwa kwenye kura za maoni.
Aidha Bi Gekul amewataka waliochukua fomu za kugombea udiwani
watakaoshindwa kutogawanyika na kukimbilia CCM badala yake wakubalina
ndio watakao kuwa mameneja kampeni katika vijiji wanavyotokea maana wao
wanajulikana kwa wapenzi, washabiki na wanachama wa Chadema.
Wanachama walio hamia Chadema walioongozwa na Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Wangbay Kijiji cha Logia, Fabian Mathe ambaye alikuwa na
haya ya kusema “Mimi nimekwishapigika na mateso nilionayo ni mengi CCM
wamenitesa sana polisi kwenda ni kawaida leo nimeamua ninajua mnanionea
huruma naomba msiendelee kuvumilia huko nimeona chama changu cha CCM
kinamiliki wana watu wawili.”
“Mtendaji wenu ni wakala wa CCM hawa watendaji ndio wasimamizi
wakuu bana mkurugenzi wanasema eti huyu sio mjumbe wa serikali ya
kijiji, hivyo namna moja ya kukombolewa ni kuhama ndio kupatahaki,”
alisema.
“Mbona wengine mlikuwa mnaniombea kura mlikuwa CCM? Karibu kwenye jeshi la ukombozi tupambane,” alisema.
Alikemea wananchi wa Singu wanaowakatalia wenyeviti kusoma mapato
na matumizi eti waliteuliwa CCM akasema sasa hivi nimiliki ya Chadema
hivyo wananchi wasahau ya kale wagange ya sasa na kuwataka wakubali
kusomewa mapato na matumizi kuanzia tarehe 25 Desemba 2014.
Aliongezea kuwa endapo wananchi wakikataa wawafungie simu viongozi wajimbo na wilaya iliwaje wamalize tatizo hilo.
“Wale wanaojipanga kuvuruga ya Singu ya kusoma mapato na matumizi
wanakosea sana maana mikutano hii po kwa mujibu wa sheria, mlishindwa
kuwaondoa viongozi wenu kuanzia mwaka 2013,” alisisitiza.
“Kile kilichowafitinisha CCM ni kutofuata haki siku zote katika
kura za maoni upo uwezekano wa kufunga na kama wamefunga na nivyema
wajipange upya,” alisema.
Miongoni mwa sababu zilizotajwa na wanachama hao kukihama chama cha
mapinduzi ni kunyimwa viwanja, ufisadi uliokithiri huku Emmanuel Demai,
akisema matatizo mengi yanatatuliwa na Chadema.






0 comments:
Post a Comment