LOWASSA KATEKA MEDIA NDANI NA NJE YA TANZANIA

Author
Katika hali isiyo ya Kawaida Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Edward Ngoyai Lowassa ameteka mijadala ya kisiasa nje na ndani ya nchi. Utafiti unaonyesha kwamba Mhe.Lowassa ameteka aina zote za media: Print Media, BroadCast Media na Internet kupitia social medias.

Mashirika yote ya utangazaji ya nje ikiwepo Voice of America, BBC Swahili habari kubwa ni Mhe.Lowassa kubadilisha siasa za Tanzania hasa kwa maamuzi magumu ya kuhamia Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, CHADEMA.Leo jioni kutakuwa na Live Talk kuhusu siasa za Tanzania na Lowassa kupitia kituo cha Voice of America.

Print and Broadcast Medias zikiwepo vinavyomilikwa na Chama Cha Mapinduzi habari ni Lowassa,mitandao ya kijamii nayo habari ni Lowassa.Wachambuzi wa kisiasa wanabainisha kwamba kutekwa kwa medias na Mhe.Lowassa ni tishio kubwa kwa Mhe.Magufuli mgombea wa Chama Cha Mapinduzi, wachambuzi wanasema siasa 'is all about marketing' jinsi inavyoweza kuwafikia wapigakura na wananchi kwaujumla ndivyo ambavyo jina la kisiasa linakuwa. Wachambuzi wanabainisha zipo sababu kuu mbili ambazo zinamfanya Mhe.Lowassa kuteka mijadala ya kisiasa nchini:


1. Uendeshaji wa mchakato wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi na kukatwa kwa jina la Mhe.Edward Lowassa ambaye aliweza kuwaminisha yeye ndio rais kupitia Chama Cha Mapinduzi.
2. Ujasiri wa Mhe.Edward Lowassa kama waziri mkuu mstaafu kujiunga na siasa za upinzani mathalani CHADEMA ambacho kiliweza kuteka siasa za upinzani katika miaka mitano 2010-2015
3. Ujio wa ghafla wa Mhe.Lowassa kwenye siasa za upinzani jambo ambalo halikudhaniwa na wananchi wengi.


Utafiti vilevile unaonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa amekuwa nguzo muhimu ya mshikamano ndani ya CHADEMA.Kauli ya Dr.Slaa mbele ya hadhira kubwa ya Watanzania inasubiriwa kwa hamu katika hatma ya siasa za upinzani Tanzania. Inaminika kwamba uimara wa Mhe.Lowassa ndani ya CHADEMA utategemea na uimara wa Dr.Slaa kutokana na sababu kuu mbili:


1. Dr.Slaa ni mwanasiasa anayekubalika katika harakati za ujenzi wa siasa za upinzani Tanzania hivyo kujijengea heshima kubwa.
2. WanaMageuzi waliamini kwamba Dr.Slaa ndiye angepeperusha bendera ya CHADEMA/UKAWA kwa muda mrefu hivyo mabadiliko ya haraka ya kifikra kwa wanaMageuzi yatategemea kauli yake.


Kwa ujumla muuganiko wa Mhe.Lowassa na Dr.Slaa unaonekana tishio kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa upande mmoja na uimara wa Dr.Slaa kwa upande mwingine unaonekana nguzo imara ya CHADEMA dhidi ya propaganda chafu za CCM.

Mungu ibaiki Afrika,Mungu ibariki Tanzania.

0 comments:

Post a Comment