CCM yapata wasiwasi

Author
BAADA ya wanachama wa CCM kukihama
chama hicho na kuhamia vyama vya upinzani,
uongozi wa CCM umeanza kuweweseka na
kudai kuwa UKAWA wanatengeneza kadi feki
na kuzisambaza kwa wananchi.
Hali hiyo ilijitokeza jana,
kufuatia kauli Katibu wa Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye kudai
kuwa uongozi wa CCM
umepata taarifa kuwa UKAWA
wanatengeneza kadi feki na
kuzisambaza kwa wananchi
huku wakifanya maigizo ya
kuzirejesha na kudai
wamehama CCM.
Nape amesema kuna mchezo mchafu ambao
unafanywa na Ukawa wa kutengeneza kadi feki
na kuzigawa kwa makundi ya watu ili
inapofikia kipindi cha kampeini watu hao
wajitokeze kwa UKAWA na kujidai wamehama
CCM.
Katika hali hiyo ya kujihami, Nape aliwatishia
wananchi kwa madai kwamba yoyote ambaye
atabainika kuhama CCM kwa kutumia kadi
hizo feki hatachukuliwa hatua kali pamoja na
wahusika kutoka UKAWA.
Akizungumzia malalamiko yaliyojitokeza
kwenye chaguzi mbalimbali za kura za maoni
kuwa yanahusiana na vitendo vya rushwa,
amesema malalamiko hayo hayahusiani na
rushwa bali ni kutokana na kukiukwa kwa
taratibu na kanuni za uchaguzi.
Nape ambaye naye ni kati ya wagombea
ambao walituhumiwa kwa rushwa, amesema
chama hicho kina wala rushwa ambao
wanasababisha kuwepo kwa malalamiko.
Mbali na hilo aliwataka wagombea wote
ambao hawakuridhika na matokeo wafuate
taratibu za kupeleka malalamiko yao katika
ngazi ya juu ya uongozi ambayo ilikuwa
hukihusika katika usimamizi pamoja na
nakala kwa katibu mkuu.
“Hatuwezi kushughulikia matatizo ambayo
yanatolewa katika vyombo vya habari wala
malalamiko ya barabarani, tutatenda haki
hata kwa kutengua matokeo pale tu ambapo
tutahakikisha kuwa mlalamikaji kaonewa
kweli.
“Utaratibu wa Chama chetu unafahamika siku
zote mtu ambaye anaona hajatendewa haki
anatakiwa kipeleka malalamiko yake katika
ngazi ambazo zinastahili hivyo kila mmoja
aelezwe hivyo,” amesema Nape.
Sambamba na hilo alisema vikao ndani ya
CCM kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali
vimeanza leo, Agosti 8 hadi 9 ni Sekretalieti,
10 hado 11 vikao vya Kamati Kuu na 12 hadi
13 ni vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM.
Hata hivyo kwa sasa kuna malalamiko mengi
kwa wagombea walioshindwa katika kura za
maoni kutokana na kuwepo kwa malalamiko
ya rushwa.
Mbali na hilo waliowengi wametangaza
kuondoka CCM na kujiunga katika vyama vya
upinzani ili kuunganisha nguvu kwa ajili ya
kuiondoa CCM madarakani.

0 comments:

Post a Comment