NJIA TANO ZAKUELEKEA KWENYE MAFANIKIO

Author
Mara nyingi katika maisha yetu ya kila siku tumesikia maneno kama “nipe tano” “chukua tano” maneno haya yamekuwa maarufu katika mazingira tofauti maneno yakiashiria ushindi, au hali ya mafanikio au furaha baada ya hali fulani.

Vivyo hivyo katika maisha yetu ya kutafuta kufanikiwa katika yaleyote tunayoyafanya kilasiku viko vitu au ziko hatua ambazo huwa zinatulazimu kuzijua au kuzipitia kama kweli tunamaanisha na tunayadhamiria hayo mafanikio tunayoyatafuta.

Ni ukweli kwamba watu wengi hutamani mafanikio na kuyazungumzia katika maneno yao ya kila siku lakini kwa bahati mbaya hawajawahi kuyaishi mafanikio hayo kwa sababu ya kutokuwa na dhamira madhubuti katika kuyaelekea mafanikio hayo.

Kama ambavyo tunaposema “high five” tunagonga mikono yetu na vidole vyetu vitano vikiwa vimefunguka kuashiria ushindi basi vivyohivyo nitajaribu kugusia hatua tano au vitu vitano vitakavyokusaidia kugonga mkono wa “ high five” baada ya kuyafikia mafanikio yako.

Kwa kifupi vitu hivyo ni, uwezo binafsi wa kuvikagua vile ulivyo navyo ndani yako, uwezo wa kusimama au kuwa na msimamo, uwezo wa kupiga hatua, uwezo wa kujitengenezea sura ya maisha yako, na uwezo wa kuyaongoza maisha yako. Fuatana na mimi katika kuzichambua hatua hizi hapa chini.

1. Kuwa na uwezo binafsi wa kuvikagua vile ulivyonavyo ndani yako

Katika maisha yetu ya kilasiku hatuna budi kujifunza namna ya kujikagua sisi wenyewe, kuvikagua vile tulivyonavyo ndani yetu kwa sababu ni ukweli kwamba pasipo kujikagua sisi wenyewe basi hatutaweza kutambua upungufu tulionao na kama hatutotambua upungufu huo basi hautoweza kushughulikiwa na kuondolewa, maana yake ni kwamba tutazidi kuishi na upungufu wetu na hivyo kuathiri ufanisi wetu na mwisho wake mafanikio yetu kwa ujumla yataathirika.

Nikupe mfano wa mtu mwenye duka, mara kwa mara mmiliki wa duka huwa na muda wa kuvikagua vitu au mali aliyonayo dukani (stock taking) na hapa huweza kutambua nini kimepungua, nini hakipo kabisa na nini kipo kwa wingi.

Katika kujikagua sisi wenyewe sio tu tunapata uhakika wa vile tusivyonavyo bali pia tunapata kufahamu vile tulivyonavyo kwa wingi (strengths). Jifunze kufanya tathmini ya maisha yako binafsi kila wakati, tathmini matendo yako ya kila siku, maneno yako ya kila siku, mitazamo yako halafu angalia wapi kuna upungufu na wapi kuna fursa zaidi.

Baadhi ya maeneo ya upungufu ambayo tunaweza kuwa nayo katika maisha ni kama vile upungufu wa kihisia, kiroho kiujuzi , kifedha na mengineyo mengi. Kumbuka, uzuri ni kwamba kila tunapoweza kutambua upungufu tunaziona fursa za kuweza kuushughulikia.

2. Uwezo wa kuwa na msimamo

Wengi wetu tumeshindwa kuyafikia malengo tuliyowahi kujiwekea kwa sababu tu hatunamisimamo katika vile tunavyoviamini , kwa hiyo inakuwa rahisi kuyumbishwa na kupeperushwa na kila upepo unaokuja upande wetu.

Ili kufikia mafanikio tunayoyatamani hatuna budi kuwa na misimamo fulani katika maisha. Naupenda msemo unaosema kama huwezi kuwa na msimamo katika chochote basi utachukuliwa na chochote.
Kama wewe ni kijana na huna msimamo katika chochote basi ni rahisi kujikuta unachukuliwa na vingine ikiwamo madawa ya kulevya. Kama wewe ni mfanyakazi na hauna msimamo katika baadhi ya mambo basi ni rahisi kujikuta unabebwa na mengi kama vile rushwa na ubadhilifu.

Ni vyema kufahamu kila wakati maishani kuwa kama hauna msimamo katika ufanisi basi utaangukia katika uzembe na kutowajibika na kama hautakuwa na msimamo katika kuhakikisha unafanikiwa basi utaangukia katika umaskini.

Kusimamia kitu fulani maana yake ni kuwa na nidhamu, kujua kanuni na kukiheshimu kitu kile unachokisimamia. Kanuni na nidhamu hizi ndizo zinazotuongoza katika maisha yetu ya kila siku katika kufikia kile tunachotamani. Amua mwenyewe ninini unasimamia na ni wapi unaiweka misimamo yako kwa sababu vile tunavyoamua kuwa na misimamo navyo ndivyo vinavyosimama kama misingi katika maisha yetu.

3. Uwezo wa kupiga hatua

Yumkini unatamani kufanikiwa na kila siku unaongelea sana mafanikio, ni vema kujua kwamba mafanikio yetu hayaji kwa kuyatamani au kuyaongelea sana bali katika uwezo binafsi wa kuamua kupiga hatua. Yawezekana uko katika chombo kizuri tu cha usafiri lakini utajikuta unapitwa na kila mtu, hata wale wenye vyombo vibovu vya usafiri nao watakupita kama utakuwa umekaa tu kwenye chombo chako pasipo kuruhusu mwendo.

Chukua hatua kuelekea mustakabali wako, angalia mbele yako unaona nini? Nini ambacho unakiona kwenye mustakabali wako? Nini ungetamani ukipate kwenye mustakabali wako? Anza kufanya kila kinachohusika ili kuiona hiyo ndoto yako ikiwa dhahiri. Anza kupiga hatua ya kwanza na hatua nyingine zitakuwa rahisi kufuatia.

Kamwe usitishike na umbali unaouona kuelekea mustakabali wako, jinsi unavyopiga hatua ujasiri wako unafunguka na kukua, kumbuka kuwa kila hatua unayoipiga hata kama ni ndogo kiasi gani inakusogeza karibu na mustakabali wako.

4. Uwezo wa kujitengenezea sura ya maisha yako

Katika maisha yetu ya kila siku ni ama uamue kuitengeneza sura ya maisha yako au kuibomoa sura hiyo, wengine wetu maisha yetu hayajawahi kuwa na sura nzuri ya kuvutia

Sisi wenyewe ndiyo wenye uwezo wak uamua kuitengeneza sura hiyo kuwa vile tunataka iwe, ukiamua kukaa tu pasipo kufanya chochote basi umekusudia kwa dhamira halisi kuiharibu sura ya maisha yako mwenyewe. Ulimwengu wa leo unabadilika kwa kasi sana, ili kuweza kubakia wenye maana na wenye umuhimu basi hatuna budi kuwezana na mabadiliko hayo.

Kama hatutoweza kuyaweza mabadiliko ya karne hii basi mabadiliko hayo yatatuweza sisi.Fahamu dhahiri kwamba karne ya 21 haijaleta tu fursa bali na changamoto tele.

Lazima tuwe na ujuzi wa kufanya tabia zetu za kila siku kuendana na mabadiliko haya, lazima kuwa kasi kama vile kasi ya mabadiliko ilivyo, lazima kuwa na uwezo wa kuendana na mazingira kwa sababu ukijaribu kukakamaa na kutokubali mabadiliko katika enzi hizi basi lazima utavunjika.

Cha msingi wote tujitahidi kufanya hata yale ambayo mara nyingine hayaturidhishi; yale ambayo tunaona yanatugharimu zaidi na kutuminya zaidi,ababu kwa kufanya hivyo unaipoteza nguvu ya kukua.

0 comments:

Post a Comment