MVURUGANO
mkubwa ulizuka katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), baada ya wajumbe wanaomuunga mkono Edward Lowassa, kubaini jina
lake limekatwa.
Hali ilikuwa hivyo baada ya majina matano ya watangaza nia kutoka Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwasilishwa katika Kamati Kuu
"Lowassa hawezi kupitishwa na CCM kugombea.Hali ilikuwa hivyo baada ya majina matano ya watangaza nia kutoka Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwasilishwa katika Kamati Kuu
Taarifa ambazo kamati kuu ilipewa na kamati ya
maadili na usalama kuhusu mtu huyo hazifai na
hatuwezi kusema kila kitu" - Benjamin Mkapa
"Mimi sasa nina miaka 67. Katika umri wangu
huu kuna baadhi ya majukumu nikipewa
sitaweza. Katika umri wetu huu kuna haja gani
kujiangaisha na kazi za wananchi? Afya yangu si
imara kama zamani. Mimi nafikiri kuna umri
ukifika mtu unatakiwa kuachana na mambo haya"
- Amani Abeid Karume
"Mwaka 1995, Lowassa alikatwa kwa sababu
alikuwa na utajiri usiokuwa na maelezo. Hivi
sasa, Mwaka 2015, utajiri wake ni mkubwa kuliko
aliokuwa nao wakati ule" - Rais Kikwete
"Watu waheshimu viongozi waliomo humu ndani.
Tunao viongozi humu wametumikia Taifa kwa
juhudi na umakini mkubwa, wanaheshimika nasi
lazima tuwaheshimu na tuheshimu uamuzi
uliofikiwa ambao umeshirikisha hawa viongozi
wetu (kwenye Kamati ya Usalama na Maadili)" -
Bulembo
"Kamati Kuu lazima iwe na ujasiri. Mwenyekiti
anazo taarifa zote tena za kina, kwa hiyo lazima
wanazo sababu za msingi za kuleta humu majina
matano " - Maghji
“Tunapata wapi ujasiri wa namna hii wa kutetea
maslahi binafsi? Naona hapa ni mtu kwanza
chama baadaye, si chama kwanza mtu baadaye, Hapa hakuna mwenye taarifa za kina kama
Mwenyekiti. Ni nani huyo mwenye taarifa za kina
kumshinda Mwenyekiti? Tuna imani na uamuzi
wa Kamati ya Maadili” - Mkapa
“Ni lazima tuheshimu kiti. Lazima muwe na
uwezo wa kukubaliana na mambo
yanavyokwenda. Nashangaa watu wapo tayari
kukitishia chama, nguvu hizi za kukitisha chama
mnazitoa wapi?” - Mzee Mwinyi
“Lazima tuheshimu mamlaka, Mwenyekiti anazo
taarifa nyingi. Mimi mwaka 1995 Mwalimu
Nyerere alining’oa na akasema kama nitapewa
nafasi CCM yeye ataondoka, anakwenda
kuanzisha chama. Mimi nikanyoosha mikono na
kujitoa, Mwalimu akanifuata na kunikumbatia” -
Malecela
0 comments:
Post a Comment