Lowassa alikuwa ni mmojawapo wa wagombea
38 walioomba uteuzi na alikuwa mmojawapo wa waliokuwa wakiusaka urais
kwa udi na uvumba lakini ndoto yake ilizimwa baada ya kuondolewa katika
kinyanganyiro hicho katika hatua za awali.
Amesema saa ya ukombozi imefika wananchi wa Monduli wajiunge na chadema ili kuleta mabadiliko na ukombozi wa kweli walioukosa kwa muda mrefu.amesema Happiness.
Nae Katibu wa baraza hilo Cecilia Ndossy
ambaye ni mtia nia katika jimbo la Monduli amesema kuwa kwa kosa
walilolifanya CCM hawapaswi kupewa ridhaa ya kuongoza wananchi hao
badala yake wachague chadema mahali ambapo sauti ya watu inaheshimiwa na kupewa kipaumbele.
Kauli hizo zilitolewa katika Mkutano wa
hadhara uliobeba ujumbe wa kumkaribisha Lowassa katika chama hicho
kwani bado milango haijafungwa kwa yeye kutimiza azma yake ya kuwatumikia watanzania walio wengi.
Katika mkutano huo Chadema waliwaachia pigo CCM kwa kuwapokea wanachama wapya 10 waliojiunga kutoka chama tawala.
Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Monduli Japhet Sironga amewakaribisha watu wa Monduli kujiunga na chama hicho kinachothamini matakwa ya watu wengi na si ya baadhi ya watu wachache kama ilivyo kwa chama tawala.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na
Diwani wa kata ya Sombetini Ally Bananga amesema kuwa anaamini kuwa
Lowassa ameondolewa vitani ila hajashindwa mapambano hivyo ana nafasi ya kushinda.
Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Arusha ,Viola Lazaro amewataka wananchi wa Monduli wa Monduli wajitokeze kwa wingi katika zoezi la uandikishaji ili wapate haki ya msingi ya kuchagua viongozi makini watakaoeleta maendeleo ya Monduli na taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment