Mbunge WA msomi amesema kwa sasa
watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kusikiliza Ukawa wanamtangaza nani
ili aweze kupeperusha bendera ya kuwania nafasi ya urais.
Mbali na hilo amesema kuchelewa kwa
upatikanaji wa jina la mgombea urais kupitia ukawa kumekuwa kukitumiwa
na watu ambao hawana nia njema na umoja huo kwa kutoa maelezo kuwa ukawa
wamesambaratika.
Amesema Ukawa ni umoja unaoendeshwa na
watu makini hivyo ni lazima kufanya mazungumzo ya kina zaidi ili
kuhakikisha inapata mgombea ambaye anauzika na anakuibalika ndani ya
umoja huo na nje ya umoja huo kwa maana naya wananchi.
Akizungumzia suala la Dk. John Magufuli
kuwa mgombea urais kupitia CCM amesema kwa sasa hakuna haja ya
kuangalia mtu bali jambo pekee la kuangalia ni mfumo.
Amesema serikali haiendeshwi na mtu
mmoja hivyo Dk.Magufuli hawezi kuwa ndiye jibu la kutatua matatizo ya
wananchi mfumo kama ni mbovu hata kama angekuja kiongozi mzuri namna
gani hawezi kubadilisha jambo lolote.
“Nikweli Dk.Magofuli ni mchapa kazi hata
kama anayo mapungufu kama ilivyo kwa binadamu wengine, lakini
kinachosumbua serikali ya CCM ni mfumo uliopo.
“Ufisadi wote unafanyika ndani ya
serikali ya CCM na ili kuondokana na ufisadi na pamoja na ubadhilifu wa
mali ya Umma ni lazimakufumua mfumo mzina .
“Sasa tujiulize ni wapi ambapo anaweza
kufumua mfumo huo, rais wa Sasa Jakaya Kikwete alijaribu kutaka kuwavua
wana CCM wenzao magamba lakini nini kilichofanyika na badala yake
magamba hayo hadi sasa anamaliza muda wake bila kuyavua,” amesema Prof.
Kahigi.
Kutokana na hali hiyo Profesa Kahigi
aliwataka watanzania kutokubali kudanganywa kwa siasa nyepesi kwa
kuhaminishwa kuwa mtu mmoja ndani ya serikali anaweza kutatua matatizo
ya wizi kama mfumo mzima haujabadilishwa.
Akisisitiza uchaguzi amesema ili kuweza
kupata viongozi waliobora ni lazima kufanya mageuzi ili mfumo mpya na
safi uchukuemadaraka .
Amesema kwa sasa ni lazima kiongozi wa
CCM atumie mikataba mibovu ambayo imetengenezwa na serikali hiyo
inayolenga kuwalinda wakubwa na kuwapatia fedha nyingi.
Amesema mfumo wa sasa unasababisha
kuwepo kwa kundi la wasiokuwa nacho kuongezeka huku kundi la wenye nacho
wakineemeka na kundi hilo ni la watu wachache mno.
0 comments:
Post a Comment