Mkurugenzi
wa jiji la Arusha ameendelea kushupaa na kukandamiza demokrasia Jiji la
Arusha.Itakumbukwa kuwa jana viongozi wa CHADEMA yaani
Mbunge,madiwani,na wenyeviti wa serikali za mitaa waliandamana jana
kupinga uhuni unaofanywa na mkurugenzi na NEC wakati huu wa kuandikishwa
kwa BVR kwa wakazi wa Arusha awamu ya kwanza.
Miongoni mwa madai ya CHADEMA yalikuwa ni
1:Muda wa vituo kuwa wazi yaani iwe saa moja asubuhi hadi saa mbili usiku
2:Kuongezwa kwa mashine za BVR kwenye maeneo yenye watu wengi
3:Wananchi kuandikishwa kwa mujibu wa sheria yaani kwa mipaka ya kata na sio mitaa
4:Kukomeshwa kwa vitendo vya ubaguzi wa kikabila dhidi ya wakazi wa Arusha
5:Kuongezwa siku za uandikishaji
Mkurugenzi huyu aliahidi kuyafanyia kazi ila cha ajabu ni kuwa jana kituo cha Longdong kilivamiwa na askari na kufungwa saa kumi na mbili kinyume cha sheria.
Kama dhihaka kwa watu wa Arusha mkurugenzi ameongeza mashine nne tu kata ya sokon 1 badala ya mashine 20,kata hii ina wapiga kura 24 000 hadi jana walikuwa wameandikishwa wapiga kura 4,000tu na ni siku ya tatu.Je kwa siku nne NEC itaweza kuandikisha wapiga kura 20,000?
Kata ya Osunyai Jr ina wapigakura 19,500 hadi jana walikuwa wameandikishwa 3200 bado 16,000.
Taarifa za ndani ya NEC pamoja na mkurugenzi Id Juma zinasema kuwa wamepanga kuandikisha watu wachache maeneo ya mijini kwa njia ya kuikoa ccm na anguko kuu.Jiji la Arusha lina jumla ya wapiga kura 300,000(Laki tatu).
Hadi jana siku ya tatu kwenye awamu ya kwanza ni jumla ya wapiga kura 12,000 tu walikuwa wameandikishwa kwenye jumla ya vituo 56 kwenye awamu hii.
Ni wazi Idd Juma anatumika na anakubali kutumika kutokana na hofu ya mashaka hasa ikizingatiwa anastaafu mwakani

0 comments:
Post a Comment