SUMATRA yatangaza nauli mpya za Mikoani

Author


Abiria wakiwa wamesongamana kituo kikuu cha mabasi cha Dar es Salaam baada ya nauli kupanda ghafla kipindi cha nyuma.
Akitangaza Viwango hivyo vipya vitakavyoanza kutumika tarehe 30 mwezi huu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Gilliadi Ngewe amesema baada ya mchakato wa kupanga bei kufanyika bei za mabasi ya Masafa ya mbali yameshuka kwa asilimia 5.8 hadi 7.8 kwa kilometa kulingana na daraja la basi.
Ngewe amesema kuwa mabasi ya daraja ya chini yamepungua kutoka shilingi 34.8 hadi 34 kwa kilometa , Daraja la kawaida toka shillingi 46.1 hadi 42.5 kwa kilometa na daraja la kati toka shilingi 53.2 hadi 50.1 kwa kilometa huku dalalada zikishuka kwa shillingi 23 lakini kwa usumbufu wa chenji Nauli zitabaki vile vile.
Kwa Upande wa wamiliki wa daladala kupitia kwa mwenyekiti wao Sabri Mabrouk wao wanataka nauli iongezeke toka 400 ya sasa mpaka 600.

0 comments:

Post a Comment