Sterling: Sina Tamaa Ya Pesa, Ninahitaji Kucheza Soka

Author
Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Raheem Shaquille Sterling amezungumza kwa mara ya kwanza tangu alipokataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo siku kadhaa zilizopita.
Sterling amezungumza jambo hilo baada ya masuala mengi kuibuka ambapo baadhi ya wadau wa soka nchini England walidiridi kumpachika jina la mwenye tamaa kutokana na mkataba alioukataa kuwa na ofa ya paund laki moja kama mshahara wake kwa juma.
Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha England ambacho kilicheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Lithuania na kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza miongoni mwa mabao manne, amesema anashangazwa na tuhuma zinamuandama, ili hali ana haki ya kufanya maamuzi.
Amesema soka ndio maisha yake na linapokuja suala la mkataba hana budi kufikiria kwa kina kabla hajafanya maamuzi ya kuusaini, hivyo amesisitiza suala la kuheshimiwa katika hilo.
Sterling mwenye umri wa miaka 20, amerejesha salamu kwa wanaomponda wanaomsema vibaya kwa kuwaambia hana tabia ya tamaa na msimamo aliouweka haumaanishi kama anahitaji kikubwa zaidi kwenye mshahara wake wa juma kama wadau wengi wanavyodhani.
Amesema lengo lake ni kutaka kucheza soka na mwishowe kutwaa mataji kama ilivyokua kwa wachezaji waliopita katika mchezo huo ambao unapendwa ulimwenguni kote, hivyo jambo la pesa si chochote katika maisha yake.
APRIL 02 ------ STERLING 01
Raheem Sterling, akaongeza jambo katika mazungumzo yake wakati akihojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, kwa kusema wapo wanaomshauri mema katika maisha yake kama mama yake mzazi pamoja na wakala wake na siku zote amekua anaamini anayoambia katika mlengwa wa kulia yana mantiki maisha mwake.
Amesema wapo wengine ambao huenda wakachukizwa na ushauri ama maamuzi anyoyafanya lakini ukweli ni kwamba yeye ataendelea kuwa binaadamu ambaye anafanya, anachokitaka kwa maslahi ya soka lake na pale alipo kwa sasa.
Mkataba wa sasa wa Raheem Sterling unampa fursa ya kulipwa mshahara wa paund 35,000, kwa juma na upo mbioni kufikia kikomo hali ambayo inawapa kisulisuli viongozi wa klabu ya Liverpool.
Siku mbili zilizopita taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya habari zilieleza kwamba uongozi wa Liverpool unatarajia kumsainisha mkataba tofauti na ule wa mshaha wa laki moja kwa juma, na kinachosemekana huenda mshahara wake ukafikia paund laki moja na themanini.
Sterling: Sina Tamaa Ya Pesa, Ninahitaji Kucheza Soka

0 comments:

Post a Comment