Ajitosa Mtoni Kisa Mkewe Ana Sura Mbaya

Author
Raia mmoja kutoka nchini china aliushangaza ulimwengu mara baada ya kuamua kujitosa mtoni na kukacha sherehe ya harusi yake aliyotarajia kufunga ndoa na mwanadada aliyejulikana kwa jina la Sun.
Bwana harusi huyo Kangu Hu aliivuruga sherehe yao mara baada ya kutamka hadharani kwamba hajafurahishwa na ndoa yao kutokana na sura mbaya ya kutisha kutoka kwa mkewe.
Kang Hu alipenda kuchagua mke yeye mwenyewe lakini familia yake iliamua kumchagulia mke huyo ambapo ilikua kwa mara ya kwanza ndio anakutana na mke huyo.
Kutokana na tukio hilo familia ya upande wa mke ilijikuta ikichanganyikiwa kwa kutokujua nini cha kufanya, huku bwana harusi akikacha mchakato wa harusi hiyo na kukimbilia mtoni.
Hata hivyo bwana harusi huyo aliwahi kuokolewa na kuwahishwa kwenye kituo cha afya kwa ajili ya matibabu zaidi.
 Ajitosa Mtoni Kisa Mkewe Ana Sura Mbaya

0 comments:

Post a Comment