RATIBA LIGI KUU TANZANIA BARA

Author

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki katika sita nchini, kwa michezo minne kucheza siku ya jumamosi na michezo mwiwili kuchezwa siku ya jumapili.
Jumamosi uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC kutoka jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Coastal Union wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatin uliopo Mlandizi.
Siku ya jumapili Stand United watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga



Uongozi wa shirikisho la masumbwi ya kulipwa nchini PST, umepigilia msumari katika maamuzi ya bondia Thomas Mashali ya kuachana na mchezo wa masumbwi kwa madai hakuna anayemjali katika tasnia hiyo.
Katibu mkuu wa PST, Anton Rutta amesema maamuzi ya shirikisho hilo yameshatolewa dhidi ya Mashali na katu hawezi kuyabadilisha licha ya taarifa za kujiondoa kwenye mchezo wa masumbwi walizisikia jana jioni kupitia Times FM (Kipindi cha Maskani).
Ruta, alisema PST imechukua uamuzi wa kumfungia bondia huyo kwa kipindi kisichopungua miezi sita, kutokana na tabia yake ya kuchukua pesa kwa mapromota na kugomea kupima uzito, na wakati mwingine kupanda ulingoni.
Alisema hatua nyingine PST waliyoichukua ni kuomba ushauri kwenye baraza la michezo la taifa BMT, ili kujua nini ambacho kinaweza kuchukuwa kama hatua za kinidhamu dhidi ya bondia huyo.
“Mchezo wa masumbwi una sheria zake, lakini hauwezi kumzuia bondia kupanda ulingoni kwa kusingizio cha kufungiwa na chama kimoja ama viwili, hivyo tunaamini BMT huenda wakatupa msimamo ambao tunaweza kuutumia kama sheria za kumdhibiti Mashali”. Alisema Rutta
 PST Yatangaza Msimamo Kwa Bondia Thomas Mashali
“Kikweli tumechoshwa na tabia za Mashali na hakuna anayeopendezwa na anachokifanya, ila tunatambua mchezo wa masumbwi ni sehemu ya maisha yake hivyo hatuwezi kumpa adhabu kali kwa kumfungia mwaka mmoja ama miwili.” Aliongeza Rutta.
Kuhusu Thoma Mashali kutangaza kuachana na masumbwi Rutta alisema hawana kipingamizi na maamuzi aliyoyachukua na wanaamini yatawasaidia katika kukamilisha adhabu waliyoitoa dhidi yake.

0 comments:

Post a Comment